2022.03.19 Papa alitembelea watoto wa Ukraine katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, waliolazwa kutokana na majeraha makali na wenye magonjwa mengine. 2022.03.19 Papa alitembelea watoto wa Ukraine katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, waliolazwa kutokana na majeraha makali na wenye magonjwa mengine. 

Hospitali ya Bambino Gesu’:Papa awabembeleza watoto wa Ukraine!

Katika siku Kuu ya Mtakatifu Yosefu,Baba mlinzi wa Yesu,Papa Francisko amependa kutimiza tendo la upendo kwa ajili ya kuonesha ukaribu wa upendo wa kibaba kwa watoto wa Ukraine waliolazwa katika Hospitali ya Watoto ya Kipapa ya Bambino Gesù kwa sababu ya majeraha ya vita vinavyoendelea lakini pia na magonjwa mengine kama vile saratani,ambao walikimbizwa kwa dharura.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 19 Machi 2022 katika siku kuu ya Mtakatifu Yosefu, mida ya saa 10.00 za jioni hivi alikwenda katika Hospitali ya watoto ya Bambino Gesù ili kuwatembelea watoto waliolazwa kutoka Ukraine, kwa siku za  hivi karibuni tangu kuanza vita. Baba Mtakatifu Francisko alipokelewa na Rais wa Hospitali hiyo Bi Mariella Enoc, ambaye alimsindikiza katika Wadi mbali mbali za Hospitali ya Watoto.

Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine
Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine

Kwa mujibu  wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Dr. Matteo Bruni kwa waandishi wa habari  alisema kuwa kwa sasa ni watoto 19 kutoka ukraine walio katika hali ngumu na ambao wako kwenye vituo mbali mbali jijini Roma kuanzia  Gianicolo na Palidoro, kilomita chache kutoka mji mkuu, vikiwa ni sehemu ya Hospitali ya Watoto Bambino Gesu.

Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine
Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine

Waliofika mwanzoni mwa vita kutoka Ukraine walikuwa karibu watoto 50 wenye magonjwa mbalimbali kama saratani, magojwa na akili na aina nyingine za magonjwa ambao walikimbizwa mara moja baada ya kuanza kwa vita. Wengine wana majeraha makubwa. Papa Francisko alikwenda kwenye vitanda vyao na kuwatembelea wadogo hao kabla ya kurudi mjini Vatican.

Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine
Jumamosi 19 Machi 2022 Papa alitembelea watoto katika hospitali ya Bambino Gesù waliolazwa kutoka Ukraine
PAPA ALITEMBELEA WATOTO WA UKRAINE KATIKA HOSPITALI YA BAMBINO GESU'
20 March 2022, 14:04