Kard.Czerny amehitimisha ziara yake kati ya maumivu ya waathirika huko Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu tarehe 10 Machi alitembelea Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit huko Budapest, kituo cha Nyugati na kituo cha mapokezi cha Shirika la Malta, ambapo alisikia historia za kushangaza za wanawake mbali mbali kama Natalia, Tamara na watu wengine waliokimbia Ukraine. Hatimaye, salamu na vijana wa Ecuador waliohamishwa kutoka Kiev. Katika ukumbi wa jengo nje kidogo ya Budapest, ni kweli kwamba ungeweza kuhisi maumivu ambayo vita hivi vya kikatili vinaleta kwa watu hao. Waliotoa ushuhuda ni wakimbizi sita wa Kiukreni, wote wakiwa wanawake, ambao sasa wako salama kutokana na usaidizi uliopokelewa kutoka kwa timu za Shirika la Malta, na ambao wanasubiri kwa matumaini kurudia hali halisi mpya nchinimwao.
Kardinali Czerny, katika siku yake ya tatu na ya mwisho ya utume nchini Hungaria katika kituo cha michezo ambacho kimegeuzwa kuwa kituo cha mapokezi kwa siku chache akisaidiwa na mkalimani hakuacha kusikiliza historia hizi, na kuuliza maswali kwa wale wote ambao alikutan nao pia watoto. Aliweza kusalimia baadhi ya vijana wa Nigeria, waliokimbia kutoka Kiev, katika kituo cha Nyugati huku akiwazungumza kujua wanaendeleaje, na Kituo cha mwisho cha utume wake kilikuwa parokia ya Szent József, huko Esztergom, inayoongozwa na Padre András Szili mwenye umri wa miaka 35, na ambaye amekuwa kuhani wa kumi na tatu katika eneo hilo.
Kwa wiki kadhaa amekuwa akiishi katikati ya simu kama vile: “Don András? Leo kuna wengine 42. Ni vijana wakimbizi wa Equador waliohamishwa kutoka Kiev ambao, wakati wakisubiri kurudi nyumbani shukrani kwa ubalozi, wanakaa katika kituo au katika vyumba vya katekisimu. Wanakaa kwa siku chache huku wakishrikishana watu 56 kwa kompyuta moja, bafu mbili, na kuogea moja tu.
Walimkaribisha Kardinali Czerny, na aliyekuwa amemsindikiza ni Kardinali Peter Ërdo askofu mkuu wa Budapest, waliketi katika duara katika chumba. Akiazna kuzungumza alisema: “Niko hapa kwa sababu Papa anataka kueleza ukaribu na matumaini kwa Ukraine. Baba Mtakatifu anawaomba msali ili kuchangia amani”. Watoto wawili walimkaribia Kadinali ambaye aliwawapatia biskuti. Hatua za kupeana mkono ilifuatia na hatimya picha ya pamoja. Mjumbe wa Papa aliondoka huko ambapo kabla lakini aliwambia wasisahau upendo walio upokea ili watakaporudi katika nchi zao wao wenyewe waweze pia kutoa. Kardinali Czerny amefika Roma tarehe 11 Machi 2022.