2022.03.11 Il cKardinali  Krajewski anaingia ndani zaidi ya Ukraine. 2022.03.11 Il cKardinali Krajewski anaingia ndani zaidi ya Ukraine. 

Kard.Krajewski:shukrani kwa nchi zilizo karibu kuwakabirisha watu nyumbani mwao

Kutoka Rivne, kaskazini-magharibi mwa Ukraine,Msimamizi wa Sadaka ya Kitume anathibitisha tena:”imani inaweza kuhamisha milima”.Kwa mujibu wa Makilishi wa Papa amesema Papa Francisko anajua mateso ya watu wa Kiukrene,anajua kwamba wanakimbia na kwa hivyo anaomba kila siku na yuko karibu nao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ujumbe wa Papa Kupitia Kardinali Konrad Krajewski wa ukaribu na msaada unaendelea. Kwa maagizo ya Papa aliyemtuma  nchini Ukraine, Msimamzi wa sadaka ya kitume anaendelea na ziara yake kwa watu wanaoteseka na leo hii, baada ya kusimama huko Lviv, alifika Rivne, kaskazini-magharibi, ambapo alitembelea baadhi ya jumuiya za Kikatoliki za mji huo kwa kushiriki katika sala ya kiekumene kwa ajili ya amani na kukutana na watu wa wanaojitolea kukidhi mahitaji ya watu.

Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenza huko Zhovka karibu na Leopoli
Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenza huko Zhovka karibu na Leopoli

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Kadinali alisisitiza juu ya ukaribu wa Papa Francisko kwa  Ukraine, kwamba anataka kusema kkuwa anaipenda Ukraine, anaiombea Ukraine na kuunganisha ulimwengu mzima na  Ukraine”.  Akikumbuka ziara ya Papa Francisko kwenda kwenye Ubalozi wa Urusi siku ya kwanza ya mzozo, Kardinali Krajewski amesema kuwa Papa alikwenda kuomba huruma, ili watu wasife. Baba Mtakatifu anafuata mantiki ya Injili, hii ina maana kwamba imani inaweza kuhamisha milima. “Silaha yetu ni imani. Ikiwa  tunaamini tu, tunaweza kupata huruma na amani yake kwa ajili ya Ukraine kutoka kwa Mungu”.

Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenzo huko Zhovka karibu na Leopoli
Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenzo huko Zhovka karibu na Leopoli

Kardinali Krajewski baadaye alisisitiza kwamba Papa anasali kila siku kwa ajili ya Ukraine, na  kwamba dhamira yake ni kuwajulisha kuwa: “Baba Mtakatifu anafahamu kila kitu kinachotokea Ukraine: anajua jinsi watu wanavyoteseka, jinsi anavyotoroka na jinsi kila mtu anavyoteseka na kukaribishwa Ulaya. Hivyo shukrani kwa nchi jirani kwa sababu wanakaribisha watu wa Ukraine katika nyumba zao. “Mungu ibariki Ukraine”, salamu yake ya mwisho.

Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenzo huko Zhovka karibu na Leopoli
Kardinali Krajewski katika Parokia ya Mtakatifu Lorenzo huko Zhovka karibu na Leopoli
12 March 2022, 17:13