Kard.Krajewski yuko Ukraine kupeleka upendo wa Papa kwa watu wanaokimbia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna njia nyingi za kukaa karibu na wale wanaoteseka kama vile kwa msaada wa kimwili au wa kiroho, kwa wito rahisi au kwa wazo. Katika sehemu hii ya sauti wapo wanaojifungua kusikiliza hata walio mbali na wanaokaribisha uchungu wa wanawake. Kardinali Konrad Krajewski, Msimamzi wa Sadaka ya Kitume ya Papa, sasa yuko nchini Ukraine kupelekea msaada na ukaribu wa Baba Mtakatifu Francisko. Kwa mujibu wa Kardinali amefafanua amebainisha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu amemtuma kuonesha upendo wake kwa watu wanaoteswa, watu wanaopaswa kuhama, watu wanaopaswa kukimbia makazi yao, majimbo na miji yao. Papa anataka kuwakumbatia wote na kuwa karibu nao na kuwaambia kwamba anawapenda.
“Ninaleta Baraka yake, lakini tayari uwepo hapa katika nchi ambayo kuna vita ni muhimu sana. Ninapokutana na watu, ambao kiukweli wanajua kuwa wanatoka Vatican kwa niaba ya Baba Mtakatifu ambacho ni kielelezo cha yote, mara nyingi ninaona macho yakilenga kwa sababu wanatambua kuwa Papa yuko karibu sana ”, amesema Kardinali. Katika utume huo wa Kardinali Konrad Krajewski amezungumzia Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuk, wa Jimbo Kuu la Kiev-Halyč la Kanisa Katoliki la Kigiriki-Kiukreni, katika ujumbe wake kawaida kwa njia ya video.
“Leo tunataka kumkaribisha mgeni wetu kwa heshima na kumsaidia kuona majeraha ya Ukraine. Kanisa liko na litakuwa pamoja na watu wake, mahali ambapo uwepo wetu umeombwa sana, ili kuwakumbatia watu na kuwasaidia kupunguza mateso yao na hatimaye, asante kwa askofu Antonyj Cosha wa Chisinau, kwa msaada wa kipekee na ukaribisho wa wahamiaji wetu, watu waliokimbia"kutoka Ukraine hadi Moldovia”.
Padre Pavlo Vyshkovkyi ni Mwanashirika wa Maria Mkingwa dhambi ya Asili na Paroki wa Kanisa la Mtakatifu Nicholas huko Kiev. Yeye amesimulia juu ya ahadi ambayo waamini wengi na watu wa kujitolea wanafanya kusaidia idadi ya watu katika shida, ambao wanalazimika kutumia masaa mawili mfululizo kwnye mstari wakisubiri kupata mkate. Padre huyo ameeleza kwamba katika nyakati hizi za shida wengi wamekaribia sakramenti, wamejifungua wenyewe katika imani. “Bwana anafanya kazi hata katika wakati mgumu”. Na kuna mengi ya wakati huu, ambapo mtu anapata hofu ya vita, mtu anapata kuishi matokeo ya madhara makubwa. Kuna watoto 900 ambao ni walemavu kutokana na mzozo. Matumaini yapo katika maombi ili, jinamizi hili liweze kusiha na kuwapokea.