Vatican:Kwa ajili ya mchezo wa kidugu,mshikamano na jumuishi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wanariadha Vatican, kituo rasmi cha michezo cha Vatican, kwa makubaliano na waandaaji, ilipendekeza kuzindua upya maadilimsingi ya michezo ya udugu na ushirikishwaji, mfano wa uzoefu wa watu kama vile mbio za marathon, hasa katika Jiji la Milele. Kwa maana hiyo siku ya Alhamisi tarehe 24 Machi Marathon ya Roma itatoa chakula, kwa watu maskini wanawenda katika kituo cha mapokezi kilichofunguliwa Kwenye Jumba la Miglior na upendo wa kitume na kukabidhiwa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na kwa Masista Wafransiskani wa Mateso.
Wanariadha, waandaaji na watu maskini watashirikishana sio tu chakula bali pia historia zao. Na ili mkutano huu usibaki kuwa wa pekee, watapeleka chakula na mahitaji mengine msingi Kituoni kama ishara ya urafiki kuendelea. Kituo cha Jumba la Miglior kilichofunguliwa kibinafsi na Papa, mnamo tarehe 15 Novemba 2019, kama ishara kamili ya umakini kwa ajili ya maskini katika moyo wa Roma ambacho kipo karibu na nguzo za Uwanja wa Mtakatifu Petro: kwa maana hiyo, kwa kiasi kikubwa, katika kilomita ya 16 za njia ya Marathon. Wanariadha wa Vaticana imefanikisha mpango huo, uliopendekezwa na Mbio za Marathon za Roma, pamoja na kikundi cha michezo cha Fiamme Gialle", kuzindua upya ushirikiano wa karibu uliopo tayari kusaidia walio hatarini zaidi.
Siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi, 2022 saa kumi na mbili jioni, itafanyika Misa ya kiutamaduni kwa ajili ya Wanariadha wa Marathon itatayoadhimishwa katika Kanisa la wasanii (Santa Maria huko Montesanto) katika Uwanja wa Watu (Piazza del Popolo). Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Nchi ndiye ataongoza Misa hiyo. Mapadre wengi wa mataifa tofauti watashiriki ambao pia watakimbia marathon siku inayofuata. Itakuwa fursa kwa ajili ya maombi ya amani na kuzindua kwa upya mchezo kama uzoefu wa mazungumzo.
Masomo na maombi yaluyoandaliwa wakati wa Misa Takatifu yatakabidhiwa kwa wanariadha wenye taaluma na wasio na ujuzi na mwishowe itasomwa Sala ya Mkimbiaji wa Marathon Kutakuwa na baraka za kusisimua za wanariadha, makocha, mameneja na familia zao. Jumapili tarehe 27 ndiyo siku rasmi ya kukimbia kilomita 42 pia kupeana kijiti kwa sababu ya kusaidia Zahanati ya Watoto ya Mtakatifu Marta, Vatican. Kwa maana hiyo kutakuwa na zaidi ya wanariadha 30 wa Vatican katika. Hasa, kutakuwa na relay 4 ya kupokezana vijiti vya mshikamano ambavyo vitapita katika mitaa ya Roma ili kukusanya fedha za kusaidia familia maskini na watoto, zikisaidiwa na Zahanati ya Mtakatifu Marta. Mbio za kupokezana vijiti zimepewa jina baada ya Nyaraka tatu za Papa Francisko na mafundisho yake ya kitume kwa vijana: Lumen fidei, Laudato si ', Fratelli tutti na Christus vivit. Kati ya mgogoro wa kijamii uliozidishwa na janga na vita vya Ulaya Mashariki, kwa washiriki zaidi ya 10,000, nusu yao sio wasio Waitaliani, kutoka mataifa 100 kwenye toleo la 27 la Marathon ya Roma, iliyowasilishwa katika Manispaa kwani isingekuwa chochote cha maana ya kukimbia iwapo si ujumuishwaji huo.