Papa Francisko kwa Mama Maria. Papa Francisko kwa Mama Maria.  Tahariri

Sala kutoka katika moyo wa utamaduni mkubwa wa Maria

Imechapishwa sala kwa ajili ya siku ya kuwekwa wakfu kwa Moyo Safi wa Maria ambayo Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Watu wa Mungu wakiongozwa na Maaskofu na Mapadre duniani kote, watasali kwa pamoja Ijumaa tarehe 25 Machi 2022.

Na Andrea Tornielli

Sala ya pamoja, ambayo inaliunganisha Kanisa zima, ili kuomba amani na kuwaweka wakfu wanadamu wote hasa Urussi na Ukraine kwa Moyo Safi wa Bikira Maria, huku kwa bahati mbaya mapigano na mabomu yanayowaua wahanga yangali yanaendelea kwa wananchi wa Ukraine. Ishara rahisi, ya unyenyekevu ya wale wanaoamini na kuamini katika nguvu ya sala na sio katika silaha. Maandiko ya tendo la kuwekwa wakfu na kukabidhi, ambayo Baba Mtakatifu Francisko atafanya, karibu muda wa saa 12.30 jioni, siku ya Ijumaa tarehe 25 Machi, katika Sikukuu ya Kupashwa Habari Kwa Bikira Maria, mwishoni mwa adhimisho la kitubio katika Kanisa kuu la Vatican. Haya ni maandishi yaliyounganishwa na nukuu kutoka katika mapokeo makuu ya Maria, ambayo yatatamkwa ulimwenguni kote na watu wa Mungu wakiongozwa na maaskofu na mapadre. Yafuatayo ni baadhi ya marejeo.

Mama wa Mungu, ni sifa ambayo Mashariki na magharibi wanaheshimu Mama, iliyotangazwa na Dogma ya Mtaguso wa Efeso kuwa fundisho la mafundisho ya dini. Mama wa huruma ni usemi unaojirudia pia katika sala ya “Salamu Malkia”.  Yeye aliyetupatia wewe na aliweka katika Moyo wako Safi kimbilio kwa Kanisa na kwa wanadamu. Maneno haya yanaibua ufunuo wa Fatima: “Mungu ameamua kudumisha ibada katika Moyo wangu Safi...” na “Moyo wangu Safi utakuwa kimbilio lako”. Japokuwa fundisho la Maria Mkingiwa dhambi ya Asili lililotangazwa na Mwenyeheri Pio IX mnamo 1854, ni la Kanisa Katoliki, lakini Makanisa ya Kiorthodox yana shirikisha imani hii sawa. Mtaalimungu Sergey Bulgakov wa Kiorthodox wa Urussi, kwa mfano, anasema kwamba: “katika Uorthodox, imani ya kutokuwa na dhambi binafsi ya Mama wa Mungu ni kama uvumba, kama wingu la sala ambalo ibada na uchaji wa Kanisa huzingatia na ibada za Kanisa hujikita nayo na kupaa juu. Zaidi ya hayo, rejeo la kimbilio linafanya sala ya zamani ya Maria “Sub tuum praesidium”, yaani ,“tunaukimbilia ulinzi wako”, isikike.

Kwa maana hiyo tunakimbilia kwako, na kwako tunabisha mlango wa Moyo wako, watoto wako, wapendwa ambao wewe huchoki kuwatembelea na kuwaalika kwenye njia ya uongofu. Hapa tunaweza kuona wito wa maonesho ya Maria. Unarudia kwa kila mmoja wetu: “Je, mimi siko hapa, Mama yako ni nani?”. Huu ni usemi ambao Maria alijifunua kwa Mhindi mmoja Juan Diego, katika tokeo la Guadalupe.  “Wewe unajua jinsi ya kufungua mafundo ya mioyo yetu na mafundo ya wakati wetu”. Unaweza kusoma rejeo la Mama anayefungua mafundo katika, picha ya Maria ambayo Papa Francisko anatoa ibada sana. Wewe, “nchi ya Mbinguni”, unaleta upatanisho wa Mungu duniani. Usemi wa “nchi ya Mbinguni” umechukuliwa kutoka katika wimbo wa kimonaki wa Byzantine-Slavic, na kwa ushairi huo unamaanisha muungano kati ya mbingu na dunia ambao tunaweza kutafakari kwa mama Maria aliyepalizwa Mbinguni akiwa hata na mwili wake. Machozi uliyotutolea yafanye kuchanua bonde hili ambalo chuki yetu imekauka. Hapa unaweza kuelewa dokezo jingine la sala ya “Salamu Malkia” ambayo inazungumza juu ya “bonde la machozi”.

Tazama mimi hapa iliyoibuka kutoka katika Moyo wako ilifungua milango ya historia kwa Mfalme wa Amani; tunatumaini kwamba tena, kupitia Moyo wako, amani itakuja. Katika maneno haya tunapata dokezo lililofichika mwanzoni mwa “Mkataba juu ya ibada ya kweli” ya Mtakatifu wa Montfort, kwa mujibu wake kwamba Mungu, alipoingia ulimwenguni kwa njia ya Maria, hivyo kupitia kwake anataka kuendelea kutawala ulimwenguni. Nywesha ukavu wa mioyo yetu, wewe ambaye “ni chemchemi hai ya matumaini”. Hii ni nukuu kutoka kwa sala ya Mtakatifu Bernard, “Mama Bikira, Binti wa Mwanao”, aliyepo kwenye wimbo wa mwisho (XXXIII) wa Dante Alighieri (Mtungo wa Divine Comedy). Umesuka ubinadamu kwa Yesu. Ni usemi uliochochewa na baadhi ya mababa wa mashariki (kwa mfano Mtakatifu Ephrem wa Siria). Picha ya Maria kama “mfumaji” inapatikana katika picha za kwanza za Kikristo zilizoko kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu na katika milenia yote ya kwanza.

Kujikabidhiwa kwa Maria ni wa kiinjili.  Kwa hakika, katika Injili ya Yohane tunasoma kwamba Yesu, kutoka msalabani, alimkabidhi mama yake kwa mtume pekee aliyekuwepo pale Kalvari: “Mama, tazama huyo hapo mwana wako!”. Na mara baada ya kusema hayo akamweleza Yohane: “Tazama huyo ni mama yako!”.  Kufuatia na tendo la kuwekwa wakfu au kujikabidhi kwa Maria, tunapata alama karibu kuanzia karne ya nane, pamoja na Yohane Damascene, Mtaalimungu Mwarabu wa imani ya Kikristo na Mwalimu wa  Kanisa, mzaliwa wa Damasco. Ni yeye ambaye alitunga sala ya kwanza ya kuwekwa wakfu kwa Mama Yetu: Hata sisi leo hii tunabaki karibu na wewe, ee Mwenyezi. Ndiyo, ninarudia tena, Ee Mwenye Enzi Kuu, Mama wa Mungu na Bikira. Tunazifunga nafsi zetu kwa tumaini lako kama nanga thabiti na isiyoweza kukatika kabisa, tukiweka wakfu akili, nafsi, mwili na utu wetu wote na kukuheshimu, kadiri inavyowezekana, 'kwa zaburi, na nyimbo na tenzi za kiroho' (Efe 5:5.19)”.

23 March 2022, 16:47