Ijumaa Kuu ni Njia ya Msalaba na Papa anarudi tena Colosseo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu tarehe 21 Machi 2022 imetachapishwa ratiba ya Baba Mtakatifu Francisko katika miezi ijayo kuanzia tarehe 2-3 ambapo atakuwa na ziara ya kitume kwenda Malta. Na ratiba za vipindi vya Kiliturujia kuanzia tarehe 10 Aprili ambayo ni Dominika ya Matawi, misa Takatifu ikiwa ndiyo mwanzo wa kuingia katika Jua Kuu la Mateso na kifo cha Bwana Yesu yetu Kristo, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican saa 4.00 asubuhi. Hii ni siku ambayo inakumbusha kuingia kwake Bwana wetu katika mji wa Yerusalemu na mfalme wa wa Wafalme wakiimba nyimba za kumtukuza.
Mnamo tarehe 14 Aprili 2022,itakuwa ni Kuu Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa 3.30 asubuhi Misa ya Kubariki Mafuta matakatifu ya Krisma. Tarehe 15 Aprili 2022 siku ya Ijumaa Kuu, inayotukumbusha Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, saa 11.00 kamili jioni, Ibada ya Mateso ya Bwana wetu Yesu. Vile vile usiku itafanyika Njia ya Msalaba katika Colosseo, ambapo inarudi kwa mara nyingine tena kufanyika usiku saa 3.15.
Tarehe 16 Aprili 2022, ni siku ya Jumamosi Kuu Mateso na Kifo cha Bwana, usiku wa Mkesha wa Pasaka, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 1.30 usiku itaanza Misa Takatifu, itakayotanguliwa na Mkesha. Tarehe 17 Aprili 2022 Dominika ya Ufufuko wa Bwana, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.00 asubuhi kutakuwa na misa Takatifu ya Pasaka ya Bwana ambapo mara baada ya misa saa 6.00 kamili Baba Mtakatifu Francisko atatoa Baraka ya “Urbi et Orbi”.
Tarehe 24 Aprili ikiwa ni Dominika ya II ya Pasaka, kiutamaduni inajulikana Dominika ya Huruma ya Mungu, Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, saa 4. 00 kamili asubuhi itaadhimishwa misa takatifu. Tarehe 15 Mei, katika Dominika ya Pasaka saa 4.00 kamili asubuhi Misa Takatifu inatarajiwa kufanyika katika Kikanisa cha Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza wenyeheri wapya wafuatao: Titus Brandsma, Lazzaro, aliyejukiana Devasahayam, César de Bus, Luigi Maria Palazzolo, Giustino Maria Russolillo, Charles de Foucauld, Maria Rivier, Maria Francesca wa Yesu Rubatto, Maria wa Yesu Santocanale, Maria Domenica Mantovani.