Tafuta

2022.03.26 Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Burundi Bwana Evariste Ndayishimiye. 2022.03.26 Papa amekutana na Rais wa Jamhuri ya Burundi Bwana Evariste Ndayishimiye. 

Papa Francisko akutana na Rais wa Évariste Ndayishimiye,wa Burundi

Tarehe 26 Machi 2022,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Burundi Bwana Évariste Ndayishimiye katika Jumba la Kitume Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 26 Machi 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la Kitume la Rais wa Jamhuri ya Burundi Bwana Évariste Ndayishimiye, ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Uhusiano na Ushirikiano na Nchi.

Papa akizungumza na Rais wa Burundi
Papa akizungumza na Rais wa Burundi

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Vatican, wakati wa mazungumzo na Katibu wa Vatican  wamepongezana kuwa na mahusiano mema kati ya Vatican na Burundi, na mchango wa Kanisa katoliki unaotolewa  katika maisha ya Nchi na kwenye sekta mbali mbali za kijamii. Katika mazungumzo hayo pia wamegusia kuhusu hali za sera za kisasa na kijamii katika Nchi na wamekabiliana na mantiki zenye tabia za kikanda.

Papa amekutan a na Rais wa Burundi
Papa amekutan a na Rais wa Burundi

Hata hivyo kama kawaida ya utamaduni wa mikutano hiyo, hawakukosa kubadilishana zawadi kati yao ambapo Baba Mtakatifu Francisko amempatia rais wa Burudini Medali ya shaba yenye mchro wa Malaika wa amani; vitabu vya hai za kipapa, Ujume wa amani kwa mwaka 2022 ; Hati ya Udugu wa Kibinadfamu, Kitabu kuhusu ‘Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020 kilichoandaliwa na Duka la vitabu la Vatican, ambacho kinaonesha siku maalumu ya sala ya Papa akiwa peke yake kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro, tukiwa katikati ya kipindi kigumu cha Janga la uviko.

Rais wa Burundi akizaungumza na Katibu wa Vatican
Rais wa Burundi akizaungumza na Katibu wa Vatican

Na kwa upande wa zawadi za Rais wa Burundi kwa Papa vilikuwa ni vyombo vya muziki wa asili nchini Burundi na Uthibitisho wa mchango wa ujenzi wa kanisa nchini Burundi.

Rais wa Burundi akizaungumza na Katibu wa Vatican
Rais wa Burundi akizaungumza na Katibu wa Vatican
26 March 2022, 18:11