Tafuta

2022.03.21 Papa Francisko amekutana na Rais Michel Aoun, wa Jamhuri ya Lebanon. 2022.03.21 Papa Francisko amekutana na Rais Michel Aoun, wa Jamhuri ya Lebanon. 

Papa Francisko akutana na rais Michel Aoun wa Lebanon

Jumatatu tarehe 21 Machi 2022,Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa Jamhuri ya Lebanon,Michel Aoun,ambapo mara baada ya mkutano huo amekutana pia na Katibu wa Vatican,Kardinali Parolin akiambata na Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusinao na Ushirikano na Nchi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 21 Machi 2021, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Lebanon, Bwana Michel Aoun. Baada ya Mkutano huo pia amekutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin akiambata na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican na Mahusiano na ushirikiano wa Nchi. Katika mazungumzo yao wamesisitiza juu ya umuhimu wa uhusiano mwema wa kidiplomasia uliopo ambapo mwaka huu unatimiza miaka 75 tangu kuanza kwake.

Papa amekutana na Rais wa Lebanon
Papa amekutana na Rais wa Lebanon

Baadaye wamezungumzia masuala ya matatizo ya kijamii, kiuchuni ambayo yameikumba nchi hiyo na juu ya hali ya wakimbizi, huku wakiwa na tumaini la kupata msaada wa Jumuiya ya kimataifa, vile vile wamjikita, juu ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na mageuzi ya lazima ambayo yanaweza kuleta mchango mkubwa wa kuongeza nguvu za amani kati ya dini mbali mbali zilizomo katika Nchi ya mwerezi.

Rais wa Lebanon amekutana na Kardinali Parolin Katibu wa Vatican, mara tu baada ya kukutana na Papa
Rais wa Lebanon amekutana na Kardinali Parolin Katibu wa Vatican, mara tu baada ya kukutana na Papa

Zaidi ya mazungumzo yao wametaja hata matokeo mabaya ya janga la kulipuka kwa moto katika bandari ya Beirut uliotokea tarehe 4 Agosti 2020 ambapo wamebainisha juu ya kuendeleza mchakato wa kutafuta haki na ukweli ambao unaombwa na familia za waathirika.

Rais wa Lebanon akibadilishana zawadi na Papa Francisko wakati wa mkutano wao
Rais wa Lebanon akibadilishana zawadi na Papa Francisko wakati wa mkutano wao
21 March 2022, 16:45