2022.03.23 Nembo rasimi ya Ziara ya Papa nchini Sudan Kusini (5-7 Julai 2022) 2022.03.23 Nembo rasimi ya Ziara ya Papa nchini Sudan Kusini (5-7 Julai 2022) 

Papa,Sudan Kusini:Kauli mbiu:“Ninawaombea ili wote wawe na umoja"

Nembo na kauli mbiu ya ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Suda Kusini imechapishwa ambapo inaongozwa: "Ninawaombea Wote wawe na umoja",kifungu kutoka Injili ya Yohane (Yh17).

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Jumatato tarehe 23 Machi 2022, imetolewa Kauli mbiu inayoongoza ziara ya Kipapa ya Sudan Kusini kunzia tarehe 5 hadi 7 Julai 2022 isemayo: “Ninaomba ili wote wawe na umoja”,  ambayo imetolewa katika  kifungu cha sala ya kikuhani ya  Injili ya Yohane 17. Nembo ya ziara hiyo ina Njiwa ambapo imezungukwa na ramani ya Sudan Kusini kwa rangi za bendera yake, Msalaba na mikono miwili iliyoshikana na   Pembeni mwa bendera ya Sudan Kusini ametua Njiwa ambaye amebeba tawi la mzeituni unaowakilisha shauku ya amani kwa anjili ya Nchi.

Mikono iliyoshikana kuwakilisha upatanisho

Juu ya Bendera ametua Njiwa inayonesha Sudan Kusini katikati ya baendera kuna mikono miwili liyoshikana inawakilisha upatanisho wa makabila ambayo yanaunda Taifa moja.

Msalaba urithi wa historia na ishara ya mateso 

Kulia kuna msalaba uliosimama na ambao unawakilisha urithi wa Nchi na historia yake ya Mateso. Karibu na msalaba kuna neno lilioandikwa “Papa Francisko nchini Sudan Kusini na tarehe ya ziara yake ya kitume 5-7 Julai 2022.

23 March 2022, 15:34