2022.03.21 Uwakilishi wa Katimba mpya ya Kitume "Praedicate Evangelium" tarehe 21 Machi 2022. 2022.03.21 Uwakilishi wa Katimba mpya ya Kitume "Praedicate Evangelium" tarehe 21 Machi 2022. 

Praedicate Evangelium,Semeraro:Mageuzi ya Curia hayaishi!

Mwenyikiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu,Mellino,Katibu wa Baraza la Makardinali na Ghirlanda,Mwanasheria ya Kanoni wameonesha kwa waandishi wa habari Vatican kuhusiana na mapya na mambo mengine yanayohusu Katiba Mpya ya Kitume,iliyochapishwa tarehe 19 Machi wakati wa kuiwakilisha 21 Machi 2022.Kuanzia na nafasi ya walei,mapambano dhidi ya nyanyaso hadi uhusiano na tamaduni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

 “Curia semper reformanda” yaani, Sekretarieti Kuu daima katika mageuzi. Mtazamo wa kale juu ya njia ya milele ya mageuzi ya Kanisa unakwenda vizuri na mchakato wa kuundwa upya kwa Sekretarieti Kuu ‘Curia Romana’, iliyotiwa muhuri lakini, kiukweli, haijahitimishwa na kutangazwa, tarehe 19 Machi 2022 kwa katiba ya kitume  yene jina: ‘Praedicate Evangelium’, yaani 'Hubirini Injili'. Akiwasilisha katika Chumba cha Waandishi wa Habari hati itakayoanza kutumika tangu tarehe 5 Juni 2022, na ambayo ni  tunda la  matokeo ya karibu miaka kumi ya kazi ya tafakari, mashauriano, tathmini ya Papa pamoja na Baraza la Makardinali na ukweli mbalimbali wa kikanisa, Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu  na ambaye kwa miaka saba alikuwa ni Katibu wa Baraza la Makardinali, Jumatatu tarehe 21 Machi 2022 alieleza jinsi ambavyo katiba mpya kwamba inafunga tu njia moja bali inafungua njia mpya kwa siku zijazo.

Mwendelezo wa Katiba za zamani Regimini Ecclesiae universae(1967)na Pastor Bonus(1988)

Kwa maana hiyo kunaweza kuwa na ubunifu mwingine mpya kwa kuongeza wale ambao tayari wameanzishwa kama vile (walei  kuwa wakuu wa mabaraza ya kipapa  au Mabaraza kuunganishwa), amebainisha Kardinali. Ikiwa kuna mabadiliko mengine, Papa atayafanya, alisema Kardinali akikumbuka kwamba kiukweli hii ilitokea kwa Mtakatifu Paulo VI na Yohane  Paulo II, ambao ni waandishi wa katiba mbili:  “Regimini Ecclesiae universae (1967)” na Pastor Bonus (1988). Ni msingi ambao kwa hatua umepelekea Papa Francisko katika Hati ya mpango wa utume wake kuhusu Wosia wa ‘Evangelii Gaudium ambapo  alifupisha kwa usemi huu: “Wakati ni mkubwa kuliko nafasi”, alisisitiza Kardinali Semeraro. Hii inaruhusu kufanya kazi kwa muda mrefu, bila kushtushwa na matokeo ya haraka. Inasaidia kuvumilia hali ngumu na mbaya kwa uvumilivu, au mabadiliko katika mipango ambayo nguvu ya ukweli inaweka.

Praedicate Evangelium inafanya Mtaguso wa II kustawi tena

Kanuni nyingine muhimu inayofuatwa katikauandishi wa waraka huo ni ile ya mapokeo, yaani, “uaminifu kwa historia na mwendelezo wa mambo yaliyopita”. Ingekuwa inapotosha (pamoja na ya kufikiria) kufikiria mageuzi ambayo yangevuruga muundo mzima wa sekretarieti Kuu, alifafanua kardinali Semeraro. 'Praedicate Evangelium' inafanya kustawi matumaini na matarajio ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Na hili ni jambo zuri ambalo linatukumbusha dhana yenyewe ya mageuzi kwamba “kulikuwa na hofu ya kutumia neno hili kwa sababu ya mabishano ya kizamani”

Nafasi kwa walei

Wakati huo huo, Katiba mpya ya Kitume inatoa mambo ya kiubunifu yaliyoamuliwa kuhusiana na siku za nyuma. Moja juu ya yote, ni ukweli kwamba walei wanaume na wanawake katika Sekretarieti Kuu, ‘Curia Romana’ wanaweza kuchukua uongozi wa Mabaraza au miili mingine. Kiukweli, tayari imetokea kwa kuteuliwa kwa mlei, Dk. Paolo Ruffini, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. "Huo haukuwa ni uamuzi uliotolewa hivi hivi tu na Papa; kinyume chake, ulifanyiwa utafiti muhimu kwa mchango wa mamlaka husika”, amefafanua. Na kwamba hii ilikuwa ianatarajiwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican ambao ulindwa kukuza Taalimungu ya Walei." Katika nuru hiyo inapaswa kufikiria hata chaguzi za uundaji mpya wa katika ya kuongeza mabaraza, ambayo yalianzia enzi Papa Sixtus wa Tano, ambaye alidhani kwamba wanaoshikilia urais wa “mabaraza ya Kikaka walikuwa ni Makardinali pekee. Hiyo sasa haitakuwa hivi tena. Neni Baraza lina maana kwamba kimsingi wote waliobatizwa wanaweza kutekeleza ofisi hiyo: mapadre, watu waliowekwa wakfu, na walei ”.

Mwamini yeyote anayeteuliwa anatimiza wajibu kwa mamlaka aliyopewa na Papa 

Jambo la kufurahisha ni kwamba, Padre Mjesuit Gianfranco Ghirlanda, ambaye ni mwanasheria wa Kanoni na profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, alibainisha katika hotuba yake ukweli kwamba mwamini  yeyote anayeteuliwa kuwa mkuu wa Baraza hana mamlaka kwa sababu ya cheo cha daraja anachoteuliwa, lakini kwa mamlaka anayopokea kutoka kwa Papa. Ikiwa mwenyekiti wa Baraza  na katibu wa Baraza ni maaskofu, hii haipaswi kusababisha kutokuelewana kwamba mamlaka yao yanatokana na daraja walilopokea, kana kwamba wanatenda kwa nguvu zao wenyewe. Mamlaka ya kutekeleza jukumu la kofisi ni sawa ikiwa linapokelewa kutoka kwa askofu, Padre, Mtawa au mlei.” Uthibitisho zaidi kwamba nguvu ya utawala katika Kanisa haitokani na sakramenti ya Daraja Takatifu, lakini kutoka katika utume wa kisheria. Kwa maana hiyo, usawa wa kimsingi kati ya wote waliobatizwa unathibitishwa tena, hata kama katika utofautishaji na ukamilishano wake ni tofauti, alisema Ghirlanda na kuongeza kwamba hiyo inajikita msingi wake wa Sinodi.

Uteuzi na tathmini

Lakini je, walei wanaweza kuteuliwa kuwa wakuu wa Mabaraza yoyote, ikiwa ni pamoja na Sekretarieti Kuu kwa vile katiba inamzungumzia katibu wa nchi ambaye si lazima awe Kardinali? Kuna mabaraza ambayo ni rahisi kuwemo watu Walei amesisitiza tena  mchambuzi huyo wa kisheria na  akitoa mfano Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambalo linajumuisha sekta ambazo walei wanaishi na ambazo wana uzoefu. Hakuna uzuizi uliowekwa, kwa mujibu wa  Ghirlanda. Wakati huo huo, katika kesi ya Mahakama, katiba haibatili Sheria ya Kanoni ambayo inaweka wazi kwamba katika masuala yanayowahusu mapadre ni mapadre wenyewe ambao wanahukumu ... Kanisa linabaki na uongozi. Kazi ya kuhani au askofu haiondolewi, inategemeana na  hali tofauti”. Katika mada hiyo hiyo hata hivyo Monsinyo Marco Mellino, ambaye tangu 2022 ni Katibu  wa Baraza la makardinali alifafanua kuwa iwe mlei atateuliwa au la kutokana na umahiri mahususi la Baraza hilo. Kwa hivyo inahitaji tathmini ya juu: Sio kitu kinachoanzishwa kiautomatiki”.

Mzunguko na sio vituo vya madaraka

Wakizungumzia juu ya ujuzi, baadhi ya waandishi wa habari wameona jinsi muda wa miaka mitano uliowekwa kwa maafisa wa Mabaraza baada ya hapo wanapaswa kurejea majimboni au, zaidi, kuthibitishwa tena kwa miaka mingine mitano, inaweza kupunguza kwa kukuza ujuzi wa kitaaluma. Padre Ghirlanda alijibu  kwamna ni  “Ni kweli uzoefu unatokana na kufanya mazoezi, lakini ikiwa mtu huyo katika miaka hiyo mitano hajafanya maendeleo yoyote au unaona kwamba anakaribia kupanda ngazi, na haifai kuifanya kwa upya. Ikiwa, kwa upande mwingine, katika miaka hiyo mitano imezaa matunda, inawezekana kuthibitishwa tena. Na sio mara moja tu, lakini kwa muda mrefu kama inachukuliwa kuwa inafaa ”. Ni hakika, alisema Mjesuit huyo, kwamba “watu wanaokaa katika nyadhifa za utawala kwa muda mrefu sana wanaweza kuendeleza vituo vya mamlaka. Na katika Kanisa hilo  kamwe haifai. Kwa maana hiyo mzunguko unapelekea kuleta mawazo mapya, ujuzi mpya, na uwazi ".

Mapambano dhidi ya nyanyaso

Katika mkutano na waandishi wa habari pia kulikuwa na mtazamo kuhusu suala la mapambano dhidi ya nyanyaso, ambapo sasa inafungamanishwa kutoka Tume ya Kipapa ya Kulinda Watoto kwenda Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Nidhamu ya Sakramenti. “Tume hiyo ina jukumu la kuzuia uhalifu wa namna hiyo; sehemu ya Nidhamu ya Sakrametni ya Baraza la Kipapa, ni ile ya kufanya 'hatua ya jinai dhidi yao, alielezea Mjesuit huyo. Kuunganishwa huko ni ishara ya  kuona ni kiasi gani Kanisa linafanya kazi ya kuzuia uhalifu huo mkubwa usiendelee kutendwa  na mapadre, watawa au walei wanaofanya kazi katika Kanisa.  Kwa maana hiyo n muhimu kufanya kujua maoni ya umma upamoja wa juhudi zinazoendelea kuongeza na muhimu ambazo Kanisa limeelezea katika miaka ya hivi karibuni kuhusu ulinzi wa watoto, alisema Mjesuit, huku akilalamikia kwa msisitizo mwingi wa vyombo vya habari juu ya kashfa, kuliko kuzingatia afya na jinsi ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, ambai hau tu  katika Kanisa, lakini pia katika jamii kwa ujumla..

Jukumu la Mabaraza ya Maaskofu

Hatimaye, wametaja kwa ufupi suala la mamlaka ya majisterio yaMabaraza ya Maaskofu, kwa kuzingatia kanuni ya wingi lakini pia juu ya umuhimu mkubwa unaotolewa kwa kila uaskofu. Kwa maana hiyo walibainisha kuwa kila Baraza la Maaskofu linaweza kuchukua maamuzi kwa uhuru wake. Hii ina maana kwamba kinachoanzishwa na Baraza la maaskofu hakiwezi kupingana na majistrio ya  ulimwengu, vinginevyo kinatuweka nje ya umoja wa kikanisa, alisema Monisnyo Ghirlanda. Katiba mpya iko kwenye kiwango cha umoja wa kikanisa kati ya maaskofu, bila kujali kama ni kitendo cha kutunga sheria au tafsiri ya kimafundisho. Ni muhimu kwamba umoja wa kina uwepo kati ya maaskofu na Baraza la Maaskofu, na aliunga mkono Kardinali Semeraro, kwa kubainisha kwamba alikuwa amehudhuria mkutano wa Baraza la Maaskofu ambapo ndani huo alijionea pande mbili wazi kama vyama. Hili halipaswi kutokea katika Kanisa”.

MKUTANO NA WAANDISHI KUHUSU MAELEZO YA KATIBA MPYA YA KITUME
22 March 2022, 17:22