Tafuta

Papa Francisko Papa Francisko  Tahariri

Ubatizo na utume,ni funguo mbili za upatanisho za Praedicate Evangelium

Uhusiano wa katiba mpya kwenye Curia Romana na Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kuhusu kipaumbele cha uinjilishaji na jukumu la walei.

NA ANDREA TORNIELLI

Katiba ya kitume Praedicate Evangelium  ya Sekretarieti Kuu 'Curia Romana' iliyochapishwa Jumamosi tarehe 19 Machi 2022 inapanga mchakato wa mageuzi yanayotokana na mjadala wa kabla ya mkutano mkuu wa 2013 na ambao tayari umetekelezwa kwa kiasi kikubwa katika miaka tisa iliyopita. Ni andiko linalokita kwa kina na kufanya miongozo ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Kiekuemene wa Vatican, ambao kama madhumuni yake ya awali ulikuwa na jibu la swali kuu kuhusu jinsi gani ya kutangaza Injili katika enzi ya mabadiliko ambayo baadaye yangejidhihirisha, kama Papa Fransisko mara nyingi amesisitiza kuwa na mabadiliko ya zama. Kuunganishwa kwa Mabaraza mawili kuwa moja kwa kuongozwa moja kwa moja na Papa wa kale na lenye muundo Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa Watu na lile la Uhamasishaji wa Unjilishaji Mpya ni kunaonesha kipaumbele kilichotolewa kwa uinjilishaji kilichooneshwa katika hati moja kwa moja kutoka katika kichwa chake.

Jinsi gani ya kushuhudia uzuri wa imani ya Kikristo kwa vizazi vipya ambavyo havizungumzi wala kuelewa lugha za zamani? Je, tunawezaje kuhakikisha kwamba chachu ya Injili inarudi ili kuchachua unga wa jumuiya zilizowahi kuwa za Kikristo na zile jumuiya ambazo bado hazimjui Yesu Kristo? Kanisa linalojishughulisha na mazungumzo ili kuinjilisha limekuwa ndiyo mwaliko wa mapapa wa mwisho na sasa kipengele hiki kinasisitizwa zaidi pia katika muundo wa Sekretarieti Kuu 'Curia Romana'. Curia ambayo si chombo tofauti, nguvu ya serikali juu ya Makanisa mahalia, lakini ni muundo katika huduma ya Askofu wa Roma, ambayo inatenda kwa jina lake, kwa maelekezo yake  na inayotumia "mamlaka ya ukarimu” ya yule  Kharifa wa Kristo.

Kipengele cha pili muhimu cha katiba mpya ni kukuzwa kwa matakwa yaliyopo katika maandishi ya Mtaguso kuhusu jukumu la walei. Papa Francisko anakumbuka katika Dibaji kwamba “Papa, Maaskofu na wahudumu wengine waliowekwa wakfu sio watangazaji Injili pekee yake katika Kanisa ... Kila Mkristo, kwa sababu ya Ubatizo, ni mfuasi wa kimisionari kwa kiwango ambacho amekutana na upendo wa Mungu katika Yesu Kristo”. Kutokana na hilo unapatikana ushiriki wa walei  wa kike na kiume katika majukumu ya utawala na wajibu. Iwapo “mshiriki yeyote wa waamini” anaweza kusimamia Baraza la kipapa au muhimili wowote wa Sekretarieti Kuu ' Curia Romana' “kwa kuzingatia umahiri fulani, mamlaka ya utawala na kazi ya waamini” ni kwa sababu kila taasisi ya Curia Romana inatenda kwa mujibu wa mamlaka aliyokabidhiwa na Papa. Hii ni hatua ambayo ilikuwa tayari katika vitendo, ambayo inakita katika taalimungu ya Mtaguso kuhusu walei.

Uthibititisho wa yaliyomo katika katiba mpya ya kitume inaweka wazi kwamba Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa  au katibu wa Baraza au  wawe maaskofu hawana mamlaka hayo, bali ni kwa kadri wanavyotumia mamlaka waliyopewa na Askofu wa Roma. Na nguvu hiyo, katika muktadha wa Curia Romana, ni sawa  sawa  na napopokelewa na askofu, Padre, Mtawa, kike na kiume, mlei wa kike au  kiume. Kwa maana hiyo, yameondolewa maelezo yaliyomo katika kifungu cha 7 cha Katiba ya Kitume ‘Pastor Bonus yaani ‘Mchungaji mwema’, ya mageuzi ya mwisho ya kimuundo wa Sekretarieti Kuu 'Curia Romana'  yaliyofanywa wakati wa Upapa wa Mtakatifu Yohane Paulo II, ambapo ilisomeka kuwa: “Shughuli inayohitaji mazoezi ya utawala, ni lazima iwekwe kwa ajili ya wale waliopewa daraja  takatifu”. Kwa njia hii, yale ambayo yameanzishwa na Mtaguso na ambayo tayari yametekelezwa na sheria za Kanoni yanatimizwa kikamilifu, ambapo “inatambulika kwamba kwa nguvu ya ubatizo kati ya waamini wote kuna usawa wa kweli katika hadhi na katika kutenda”.

21 March 2022, 18:18