Maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu 2022. Maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu 2022. 

Kuwepo umakini katika maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu 2022!

Katika barua kutoka kwa Baraza la Kipapa la Ibada ya Mungu na Nidhamu ya Sakramenti inasisitizwa kwamba, wakati wa janga, ni muhimu kuepuka tabia zinazoweza kuwa za hatari kwa afya. Pia mwaliko wa kuiombea Ukraine na kwa ajili ya vita vyote vinavyotokea katika sehemu nyingine za ulimwengu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hakuna miongozo ya ziada kwa ajili ya maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu ya mwaka huu 2022. Na ndicho kinasomeka katika mwongozi wa Barua kutoka kwa Baraza la Kipapa la Ibada ya Mungu na Nidhamu ya Sakramenti inayoelekeza jinsi ya kuadhimisha kipindi cha Pasaka ya Bwana. Katika miaka ya nyuma, iliyokuwa imegubikwa na hali ngumu ya janga la uviko, miongozi kadhaa ilitolewa kusaidia maaskofu katika kazi yao ya kutathmini hali halisi ili kufurahiya vyema Juma Kuu  Takatifu,ambacho ni kitovu cha mwaka mzima wa kiliturujia. Kwa maana hiyo mwaka huu mwaliko ni kuwa waangalifu, ili kuepuka ishara na tabia ambazo zinaweza kuwa za hatari. Kila tathmini na uamuzi yanapaswa kuzingatiwa kila wakati kwa kushirikiana na Baraza la Maaskofu, ambalo litazingatia kanuni ambazo mamlaka za kiraia zenye uwezo zitakuwa nazo katika nchi mbalimbali.

Kuombea watawala wa dunia

Katika barua hiyo ikirejea kuhusu ombi la Papa Francisko kwa ajili ya   kuomba ili kukomesha vita nchini Ukraine na ambavyo ni vya kuchukiza, Baraza hili limekumbusha hata migogoro mingine mingi  ambayo ipo katika nchi nyingi za ulimwengu, kama vita vya tatu vya dunia vilivyo gawanyika vipande vipande. “Katika maombi ya ulimwengu wote tutamwomba Bwana kwa ajili ya watawala (sala ya IX) aangazie akili na mioyo yao kutafuta manufaa ya wote katika uhuru wa kweli na amani ya kweli, na kwa wale walio katika majaribio (Sala ya X) ili wote waweza kupata furaha na  msaada wa huruma ya Bwana”.

Pasaka iweze kuleta tumaini kwa kila mtu

Kwa mujibu wa maelekezo ya barua inasema "Tangu mwanzo sala hii iweze kutimika kwa wote kwa ajili ya kaka na dada wote wanaosumbuliwa na kuteseka na ukatili wa vita, hasa nchini Ukraine”. Hatimaye, inakumbusha kwamba “ikiwa ni hitaji kubwa la umma, askofu wa jimbo anaweza kuruhusu au kuthibitisha kwamba nia maalum inaongezwe”. Sherehe ya Pasaka iweze kuleta kwa kila mtu tumaini linalokuja kutoka katika ufufuo wa Bwana tu”, wamehitimisha.

26 March 2022, 16:59