Askofu Maguengue ni askofu wa Jimbo la Inhambane,Msumbiji
Kufuatia na kung’atuka katika shughuli za kichungaji kwa maombi yaliyo wakilishwa na Askofu Adriano Langa,(O.F.M) wa Jimbo Inhambane nchini Msumbiji,Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Ernesto Maguengue,aliye kuwa Askofu msaidizi wa Nampula.
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung’atuka katika shughuli za kichungaji za Jimbo katoliki la Inhambane, Msumbiji, yaliyowakilishwa na Askofu Adriano Langa, (O.F.M), na wakati huo huo akamtesua Askofu wa Jimbo hilo hilo, Askofu Ernesto Maguengue, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Nampula.
04 April 2022, 16:02