Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre John Bogna Bakeni wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, Nigeria kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, nchini Nigeria. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre John Bogna Bakeni wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, Nigeria kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, nchini Nigeria. 

Askofu Msaidizi John Bogna Bakeni wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, Nigeria

Askofu mteule John Bogna Bakeni alizaliwa tarehe 15 Machi 1975 huko Kiri, Jimbo Katoliki la Maiduguri. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Agosti 2002 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa: Paroko na Mkurugenzi wa Kituo Cha Katekesi Kaya. Kuanzia mwaka 2020 hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Padre Mshauri wa kiroho Chuoni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre John Bogna Bakeni wa Jimbo Katoliki la Maiduguri, Nigeria kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Maiduguri. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni mshauri wa maisha ya kiroho Chuo Kikuu cha Maiduguri. Askofu mteule John Bogna Bakeni alizaliwa tarehe 15 Machi 1975 huko Kiri, Jimbo Katoliki la Maiduguri. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Agosti 2002 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa: Paroko na Mkurugenzi wa Kituo Cha Katekesi Kaya.

Kati ya Mwaka 2007-2012 alitumwa kujiendeleza kwa masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thoma wa Akwino, Angelicum, Roma na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu. Baadaye mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya St. Joseph huko Gashua. Na kuanzia mwaka 2013 alipangiwa majukumu mbalimbali ikiwemo Msimamizi wa Parokia ya Kanisa kuu la Maiduguri, Dekano, Mshauri wa Jimbo, Msarifu mkuu wa Jimbo na Rais wa Tume ya Majadiliano ya Kidini Jimbo Katoliki la Maiduguri. Kuanzia mwaka 2020 hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Padre Mshauri wa maisha ya kiroho Chuo Kikuu cha Maiduguri.

Uteuzi Nigeria

 

12 April 2022, 15:28