2022.04.06 Kardinali  Sandri katika Misa ya kwa Walinda Usalama wa Fedha Italia. 2022.04.06 Kardinali Sandri katika Misa ya kwa Walinda Usalama wa Fedha Italia. 

Kard.Sandri: Watendao maovu wanajifanya kuwa na nguvu katika mshikamano kwenye maovu

Kardinali Sandri,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki ameongoza misa takatifu katika Kanisa Kuu la Orvieto na wanafunzi Kitengo cha Ukaguzi wa Kitaifa wa Fedha na kuzuia ugaidi ambao wako tayari kuajiliwa kwenye Kitengo hicho cha Ukaguzi:'Vita vinaonesha hekima ya Waraka wa Fratelli tutti wa Papa,katika kujenga ustaarabu ambao unajua kuheshimu kila mtu".

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali alipofika katika kambi hiyo aliweza kufanya kwanza mkutano na wanafunzi 140 pamoja na maofisa wanaohusika na mafunzo yao kwa tafakari na majadiliano juu ya hali ya sasa ya Makanisa ya Nch za Mashariki kwa kuzingatia hasa hali ya Iraq, Siria na kwa bahati mbaya mzozo wa umwagaji damu nchini Ukraine. Baadaye aligusia baadhi ya vipengele vya mahusiano kati ya serikali ya Italia, Jamhuri ya Italia na Vatican. Baadaye, jumuiya ilihamia kwenye Kanisa Kuu la Orvieto ambako Kardinali Sandri alikaribishwa na kulakiwa na Askofu, Mkuu Gualtiero Sigismondi, Bassetti ma Rais wa Baraza la Maaskofu Italia aliwasilisha kwa ufupi hali ya jimbo na ukuu wake. Baadaye Kardinali aliongoza Ibada ya Misa Takatifu, iliyohudumiwa na kuhuishwa na wanafunzi wa shule ya mafunzo ya Walinda Fedha Kitaifa na Ugaidi hizi. Akianza mahubiri amesema “Ninyi ni watu ambao mmejiweka katika utumishi wa Taifa na jumuiya yake, na wakati huu wa maisha yenu mnajitolea kwa malezi na mafunzo maalum. Katika altare hii mnaleta pamoja mkate na divai maisha yenu, mazingirayenu ya asili, familia zenu, wapendwa wenu, wale waliowahudumia na mtakaokwenda kuwahudumia kwa kutoa ujuzi na taaluma inayokutofautisha (... )”.

Uzoefu endelevu na dhana ya mwanadamu

Kardinali Sandri amesema Neno la Mungu ambalo limesomwa linawafanya wakutane na uzoefu wa watu wa Israeli jangwani, ambao wakati fulani waliaanza kulalamika kwa Musa na hatimaye kuja kumkosoa Mungu mwenyewe: ni uzoefu endelevu ambao unakuwa dhana ya Mwanadamu kupitia nyakati (...) “Hata katika nyakati zetu, miongoni mwa mataifa yenye nguvu, kuna wale ambao wamepofushwa na mtazamo wa zamani wa mamlaka ya kibeberu, na kutiwa sumu na maono haya, wana uwezo wa kueneza kifo na uharibifu, kukanyaga maisha na hadhi ya wale wanaoshambuliwa, lakini hatimaye pia wale wanaoombwa kwa utii kufanya uhalifu huo wa kutisha”. Kardinali Sandri amesema jinsi gani maneno ya Baba Mtakatifu yalivyokuwa ya busara na ya kinabii yaliyoongozwa na Mtakatifu Francisko katika ‘Waraka wa Fratelli’ tutti yaani ‘Wote ni ndugu’ kwa ajili ya kujenga ulimwengu mpya usio na upotovu tena, kila mara ya kiangazi na kutetea utu wa kila mtu na udugu, na kwa njia hii kujenga ustaarabu mpya ambapo amani, kuheshimiana, upatanisho na mazungumzo vinatawala na kuishi kila siku.

Yesu alijua kujikabidhi kwa baba na kuwasamehe watesi wake

Kardinali Sandri aidha amesema Yesu katika Injili, katika moja ya mazungumzo ya karibu na wapinzani wake ambao mwishowe wataamuru hukumu yake ya kifo, Kardinali alibainisha jinsi ambavyo linaweka mbele ya changamoto kuu: Yeye kwanza alijisika kwa kina na kuamua uhusiano wake na Baba, na pia juu ya Msalaba; katika uchungu huo mkubwa na mateso itajikabidhi kwake akisema “Baba, uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo” na: “Baba mikononi mwako naiweka roho yangu”. Wale watendao maovu wanajifanya kuwa na nguvu katika mshikamano katika maovu, kama itakavyokuwa kati ya maadui wa kihistoria Pilato, Gavana wa Kirumi, Mfalme Herode, na viongozi wa Baraza kwa kuamua kumsulubisha Yesu: kiukweli moyo wa kila mmoja wao umezama ndani, shimo la upweke, aliyekata tamaa, vile vile Yuda ambaye mwishowe hatapinga kwa kuchagua kujitoa uhai wake mwenyewe. Hata hivyo, Yesu atatoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu pia akiwasamehe adui zake, akitoa wokovu bila kujibakiza, mradi kila mmoja ajifunze kutazama, kuinua macho yake kwake.

MAHUBIRI YA KARD. SANDRI KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA
07 April 2022, 16:42