Kardinali Peter Turkson ni Kansela Mpya wa Taasisi za Kipapa za Elimu za Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Elimu za Sayansi za Kijamii. Kardinali Peter Turkson ni Kansela Mpya wa Taasisi za Kipapa za Elimu za Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Elimu za Sayansi za Kijamii.  

Kard.Turkson ni Kansela wa Taasisi za Kipapa za Elimu ya Sayansi

Papa Francisko amemteua Kardinali Turkison kuongoza Taasisi ya Elimu ya Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi za Kijamii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Vatican, ameteuliwa Kansela wa Tassisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi zakijamii, Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, mwenye umri wa miaka 73 na ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Kardinali Turkson anachukua nafasi ya Askofu Marcelo Sánchez Sorondo wa Argentina, ambaye mnamo tarehe 8 Septemba atafikisha miaka 80 na ambaye amefunika nafasi hizo tangu mwaka 1998.

Huduma ya muda mrefu kwa Kanisa

Askofu Mstaafu wa Jimbo la Cape Coast, Turkson alikuwa ni Kardinali wa kwanza mzaliwa kutoka Ghana. Alipata daraja kwa upadre mnamo tarehe 20 Julai 1975 kwa ajili ya jimbo la Cape Coast, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis wa Sales. Baadaye aliendelea na masomo kuhusu Maandiko Matakatifu katika Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia,  Roma kwenye miaka ya 1976-1980, kwa Leseni na katika miaka ya 1987-1992 akaendelea kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu. Aliteuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa askofu mkuu wa mji mkuu wa Cape Coast mnamo tarehe 6 Oktoba 1992, na kupewa daraja la uaskofu tarehe 27 Machi 1993.

Kardinali Turkson aliwahi kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ghana kuanzia 1997 hadi 2004 na baada ya kushika nyadhifa mbalimbali katika Kanisa lake Ghana, tarehe 24 Oktoba 2009 mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa II wa Sinodi ya Maaskofu Afrika ambayo alikuwa Mjumbe Mkuu, Papa Mstaafu Benedikto XVI alimteua kuwa rais wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani. Tarehe 24 Septemba 2013, Baba Mtakatifu Francisko alimthibitisha kuwa mkuu wa Baraza hilo ambalo baadaye likageuzwa kuwa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu na tangu tarehe Mosi Januari 2022 amekuwa Mwenyekiti Mstaafu.

04 April 2022, 15:26