Tafakari ya tano ya Kwaresima 2022 Tafakari ya tano ya Kwaresima 2022 

Kard.Cantalamessa:Kielelezo cha huduma ya upendo wa unyenyekevu ni kusaidiana!

Fanyeni hivi kama nilivyofanya mimi.Yesu anaanzisha diakonía,yaani,huduma,akiinua sheria msingi zaidi,kwa mtindo wa maisha na kielelezo cha mahusiano yote.Yesu anasema Mimi nimewapa mfano.Je ametupatia mfano wa nini?Je miguu ya ndugu inapaswa kuoshwa kila tunapoketi mezani? Kwa hakika sio hiyo tu! Jibu la Injili:“Ni tafakari 5 ya Kwaresima ya Kardinali Cantalamessa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ndugu msikilizaji wa Vatican news, katika tafakari ya tano na ya mwisho wa kipinid cha Kwaresima 2022 ambayo imekuwa na mwendelezo wa mada ya Ekaristi, Ijuma tarehe 8 Aprili 2022, Kardinali Raniero Cantalamessa, Mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa aliendelea kutoa mahubiri yake kwa wajumbe wa Curia Romana kwa uwepo wa Baba Mtakatifu katika ukumbi wa Paulo VI.  Kardinali Cantalamessa alianza na swali:  Je kwanini Yohane katika simulizi ya Karamu ya mwisho hazungumzii sana juu ya Ukaristi na kinyume chake anaweka mwanga zaidi  juu ya kuosha miuguu wakati ni yeye mwenyewe aliyekuwa amekita sura nzima akiwandaa mitume juu ya kula mwili na damu yake?  Kwa kujibu wa Kardinali alisema sababu ni kwamba kila kitu kinachotazama Pasaka na Ekaristi, Yohane anajaribu kuonesha zaidi ya tukio la Sakramenti, kwamba linakuwa na maaana ya ishara. Kwake yeye Pasaka mpya haikuanzia na Karamu Kuu, ambayo baadaye itakuwa ni kufanya kumbu kumbu, kinyume chake inaanzia na msalaba mahali ambapo pia inatimizwa na ambayo lazima kufanya kumbukumbu. Hapo ndipo panatokea njia ya Pasaka ya kizamani na ile ya mpya. Kwa maana hiyo Yohane anasisitiza kuwa Yesu akiwa msalabani:“Hapana mfupa wake utakaovunjwa”. Kwa maana ilikuwa imandikwa hivyo kwa mwanakondoo wa Pasaka (Yh 19,36; Kut 12,46).

Maana ya kuosha miguu

Kardinali Cantalamessa amesema ni muhimu kuelewa vizuri maana ya ishara ambayo Yohane anaionesha ya kuosha miguu. Katiba mpya ya hivi karibuni ya kitume ya ‘Praedicate Evangelium’ inafafanua na kutaja katika Dibaji yake, kama picha ya huduma ambayo lazima iainishe kazi yote iliyorekebishwa ya Curia Romana. Hiyo inatusaidia kuelewa jinsi Ekaristi inavyoweza kufanywa katika maisha hivyo kuiga maisha ya kile kinachoadhimishwa altareni. Tunakabiliana na moja ya vipindi hivyo (nyingine ni ile ya kuchomwa ubavu), ambamo mwinjili Yohane anaweka wazi kwamba kuna fumbo chini yake ambayo linapita zaidi ya ukweli wa kawaida ambao unaweza kuonekana kuwa haufai. Yesu anasema Mimi nimewapa ninyi mfano.  Je Ametupa mfano wa nini? Je miguu ya ndugu inapaswa kuoshwa kila tunapoketi mezani? Kwa hakika sio hiyo tu! Jibu lipo katika Injili: “Yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza wenu atakuwa mtumwa wa kila mtu. Kwa hakika Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mk 10, 44-45). Katika Injili ya Luka, hasa katika muktadha wa Karamu ya Mwisho, kuna neno la Yesu ambalo linaonekana kutamkwa mwishoni mwa kuosha miguu, kwamba:“Ni nani aliye mkubwa zaidi, ni nani anayeketi mezani au anayetumikia? Je, si yule anayeketi mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama mtumishi”(Lk 22:27).

Kuosha miguu ni mfano wa Yesu katika huduma

Kwa mujibu wa Mwinjili, Yesu alisema maneno haya kwa sababu, mjadala ulikuwa umezuka kati ya wanafunzi kuhusu ni nani kati yao angeweza  kuwa mkuu zaidi (rej. Lk 22:24). Labda ilikuwa hali hii hasa ambayo ilimsukuma Yesu kuosha miguu, kama aina ya kuonesha mfano kwa vitendo. Wanafunzi wote wakiwa na shughuli nyingi wakijadiliana na kubishana wao kwa wao yeye aliinuka kimya kimya kutoka mezani, akatafuta beseni la maji na kitambaa, kisha alirudi na kupiga magoti mbele ya Petro ili kuosha miguu yake, kwa kueleweka atamtia mkanganyiko mkubwa zaidi, maana Petro alisema “Bwana, wewe waniosha miguu yangu?” ( Yoh 13, 6 ). Katika kuoshwa kwa miguu, Yesu alitaka kuonesha jinsi ya kufanya muhtasari wa maana yote ya maisha yake, ili iweze kubaki vizuri katika kumbukumbu za wanafunzi na siku moja, wakati wangeweza kuelewa zaidi ya nini maana ya “Ninachofanya, hamuelewi sasa, lakini mtaelewa baadaye”(Yn 13:7). Ishara hiyo, iliyowekwa mwishoni mwa Injili, inatuambia kwamba maisha yote ya Yesu, tangu mwanzo hadi mwisho, yalikuwa ni kuoshwa kwa miguu, yaani, kutumikia wanadamu. Ni kama mfafanuzi fulani anavyosema kuwa “ ilikuwa ni kuwepo”, kwa kuwepo kwa maisha katika kupendelea wengine. Yesu alitupatia kielelezo cha maisha yaliyotumika kwa ajili ya wengine, maisha yaliyotengenezwa, mkate umemegwa kwa ajili ya ulimwengu”. Kwa maneno haya ya “Fanyeni hivi  kama nilivyofanya mimi”, kwa upande wa Yesu anaanzisha diakonía, yaani, huduma, akiiinua kwa sheria  msingi, au, bora zaidi, kwa mtindo wa maisha na kielelezo cha mahusiano yote katika Kanisa. Hii ni kana kwamba alikuwa akisema, hata kuhusu kuosha miguu, yale aliyosemwa katika kuanzishwa  kwa Ekaristi: “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu!”.

Roho ya Huduma

Kardinali Cantalamessa akiendelea alisema, ni lazima tuongeze maana ya“huduma” ili tuweze kuitekeleza katika maisha yetu na tusiishie kwa maneno tu. Utumishi sio, usio na fadhila. Katika orodha yoyote ya wema au matunda ya Roho, kama Agano Jipya linavyoziita, tunapata neno diakonía, maana yake huduma. Hakika, kuna hata mazungumzo ya utumishi wa dhambi (rej. Rm 6, 16) au sanamu (taz 1Kor 6, 9) ambayo kwa hakika si huduma nzuri. Huduma ni kitu cha kawaida  kinachoonesha hali ya maisha, au njia ya kuhusiana na wengine katika kazi ya mtu, kuwa tegemezi kwa wengine. Inaweza hata kuwa kitu kibaya, ikiwa imefanywa kwa kulazimishwa (kama utumwa), au kwa maslahi tu. Kila mtu leo hii anazungumzia  juu ya huduma; kila mtu anasema yuko kwenye huduma: mfanyabiashara huwahudumia wateja; mtu yeyote ambaye ana nafasi katika jamii, inasemekana kwamba anatumikia, au ni utumishi. Lakini ni dhahiri kwamba huduma ambayo Injili inaizungumzia ni kitu kingine kabisa, hata kama yenyewe haiondoi, utumishi kama inavyoeleweka  katika ulimwengu. Tofauti ipo yote katika motisha na katika mtazamo wa ndani ambao huduma hiyo inafanywa.

Sakramenti ya Mamlaka

Kwa sababu hiyo, huduma ya kiinjili, kinyume na ile ya ulimwengu ambayo pia sio ya chini  kwa wahitaji wake, kwa wale wasio na kitu; bali ni mali ya aliye nayo, na ya aliye wa juu. “Kwake yeye aliyepewa vingi, ataombwa vingi” katika suala la utumishi (rej. Lk 12:48). Kwa sababu hiyo, Yesu anasema kwamba, katika Kanisa lake, juu ya wote“atawalaye” ndiye anayepaswa kuwa“kama mtumishi”( Lk 22:26 ); Yeyote aliye“wa kwanza” lazima awe “mtumishi wa wote”. (Mk 10 , 44).   Kardinali Cantalamessa amesema, Mwalimu wake, profesa wa Freiburg  alitoa fafanuzi kuwa “kuoshwa miguu ni sakramenti ya mamlaka ya Kikristo”. Kando ya huduma inaeleza sifa nyingine kuu ya agápe ya kimungu, ya unyenyekevu. Maneno ya Yesu aliyosema: “Lazima mtaoshana miguu ninyi kwa ninyi” yanamaanisha ni lazima kutoleana huduma za upendo wa unyenyekevu. Na (upendo na unyenyekevu), kwa pamoja, vinaunda ile huduma ya kiinjili.  Yesu alisema wakati mmoja kwamba: “Jifunzeni kwangu kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo (Mt 11:29). Kwa njia hiyo  alifanya nini kujiita mnyenyekevu?  Yeye alishuka, kutumikia! Tangu wakati wa kutungwa kwa mimba, hakufanya lolote zaidi ya  kushuka, hadi kufikia hatua hiyo ya nguvu sana, na ambapo tunapomwona akiwa amepiga magoti, akiosha miguu ya mitume wake. Ni msisimko ulioje kati ya malaika, kuona jinsi Mwana wa Mungu alivyoshushwa chini, ambaye hawakuthubutu hata kumkazia macho(taz. 1 Pt 1, 12), amesisitia Kardinali Cantalamessa.

Kristo hakujaribu kujifurahisha

Matunda ya tafakari hiyo yanapaswa kuwa mapitio ya kijasiri ya maisha yetu, amesisitiza Kardinali na kwamba  tabia, kazi, saa za kazi, mgawanyo na matumizi ya muda, kuona ikiwa ni huduma kweli na ikiwa, katika huduma hiyo, kuna upendo na unyenyekevu. Jambo la msingi ni kujua ikiwa tunawatumikia akina ndugu, au badala yake tunawatumia ndugu kwa manufaa yetu. Kuwatumia ndugu na kuwanyonya wale ambao, pengine, huwatendea wengine, kama wasemavyo, lakini katika kila jambo analofanya yeye hajali, anatafuta, kwa namna fulani, kibali, makofi au kuridhika, kuhisi moyoni mwake, mahali pake na mfadhili. Injili inawasilisha, juu ya hatua hiyo, kwamba : “Mkono wako wa kushoto usijue mwingine wa kulia  unafanya nini” (Mt 6: 3). Yote ambayo yamefanywa, kwa uangalifu na kwa sababu nzuri, kuonekana kwa wanadamu, kupotea. Christus non sibi placuit: Kristo hakujaribu kujifurahisha mwenyewe! (Warumi 15:3): hii ndiyo kanuni ya utumishi. Ili kufanya utambuzi wa roho, yaani, nia zinazotusukuma katika utumishi wetu, inafaa kuona ni huduma zipi tunazofanya kwa furaha na zile tunazojaribu kuepuka katika njia zote. Tazama, pia, ikiwa mioyo yetu iko tayari kuacha, ikiwa itaombwa kutoka kwetu kufanya huduma bora, ambayo inatoa mng'aro, kwa mnyenyekevu ambayo hakuna mtu atakayeithamini. Huduma salama zaidi ni zile tunazofanya bila mtu yeyote, hata wale wanaopokea,  kutambua, lakini ni Baba tu aonaye sirini.

Kanuni ya utumishi inabaki kuwa hivyo

Inawezekana kabisa huyu mtu, ni sisi hasa! Ikiwa kuna shaka kidogo kwa maana hiyo itakuwa vizuri tukiuliza kwa dhati wale wanaoishi karibu nasi na kuwapa fursa ya kujieleza bila hofu. Ikitokea kwamba sisi pia tunafanya maisha kuwa magumu kwa mtu mwenye tabia zetu, lazima tukubali kwa unyenyekevu ukweli na kufikiria kwa upya huduma yetu. Roho ya utumishi pia inapingwa, kwa upande mwingine, kwa kushikamana kupita kiasi kwa tabia na starehe za mtu. Kwa kifupi, roho ya upole. Hawezi kuwatumikia kwa uzito wengine ambao daima wana nia ya kujifurahisha mwenyewe, ambaye hufanya muungu wa kupumzika kwake, wakati wake wa bure, wa ratiba yake. Kanuni ya utumishi daima inabaki vile vile: ‘Kristo hakujaribu ujifurahisha mwenyewe’. Ikiwa kwa Wakristo wote kutumikia inamaanisha kutoishi tena kwa ajili yao wenyewe (rej. 2 Kor 5:15), kwa wachungaji inamaanisha: ‘kutojichunga”: Nabii Ezekieli anasema:“Ole wao wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe! Je, wachungaji hawapaswi kulisha kundi?(Ez 34, 2). Kwa ulimwengu, hakuna kitu cha asili na cha haki zaidi kuliko hiki, yaani, yeyote ambaye ni bwana (dominus) domini, ndiye Bwana. Miongoni mwa wanafunzi wa Yesu, hata hivyo, si kama hii, lakini “yeyote aliye bwana lazima kutumikia.” “Hatutaki kuwa mabwana juu ya imani yenu”, anaandika Mtakatifu Paulo; “badala yake sisi ni washiriki wa furaha yenu” (2 Kor 1, 24). Mtume Petro anapendekeza jambo lile lile kwa wachungaji: “Msiwatawale watu waliokabidhiwa kwenu, bali iweni vielelezo vya kundi” (rej. 1 Pt 5:3). Si rahisi, katika huduma ya kichungaji, kuepuka mawazo ya bwana wa imani; iliingizwa mapema sana katika dhana ya mamlaka. Katika mojawapo ya hati za kale sana za huduma ya maaskofu (Didascalia ya Kisiria) tayari tunapata dhana inayomtambulisha askofu kama mfalme, ambaye ndani yake hakuna kitu kinachoweza kufanywa, wala na wanadamu wala na Mungu, bila kupitia kwake.

Ulimwengu unahitaji vifaa vikubwa

Kwa wachungaji, na kama wachungaji, mara nyingi ni juu ya hatua hii kwamba tatizo la uongofu linaamuliwa. Jinsi maneno hayo ya Yesu yanavyosikika kwa nguvu na kutoka moyoni baada ya kuoshwa kwa miguu:“Mimi Bwana na Mwalimu...!”. Yesu kwa maana hiyo anasema Mtakatifu Paulo:“Naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; ( Flp 2:6 ), yaani, hakuogopa kuvunja utukufu wake wa kimungu, kupendelea ukosefu wa heshima wa wanadamu, na kujivua mapendeleo yake na kujionesha kwa mtu wa nje katikati ya watu wengine (kama sawa na watu). Yesu aliishi kwa urahisi. Urahisi wake umekuwa tangu mwanzo na ishara ya kurudi kiukweli kwa Injili. Tendo la Mungu halina budi kuigwa. Tertullian aliandika  kuwa:“Hakuna kitu kinachoonesha tendo la Mungu bora kuliko tofauti kati ya urahisi wa njia za nje na njia anazofanya kazi na ukuu wa matokeo  kiroho anazopata”. Ulimwengu unahitaji vifaa vikubwa vya kutenda na kuvutia; lakini Mungu hapana. Hata huduma ya kiinjili inadhoofishwa leo hii na hatari ya kutokuwa na dini. Inachukuliwa kwa urahisi sana kwamba kila huduma inayotolewa kwa mwanadamu ni huduma ya Mungu. Mtakatifu Paulo anazungumza juu ya huduma ya Roho (diakonía Pneumatos) (2Kor 3:8), ambayo wahudumu wa Agano Jipya wanafanya, iliyokusudiwa. Roho ya utumishi lazima ioneshwe kwa wachungaji kupitia huduma ya Roho! Ambaye, kama kuhani, kwa wito, ameitwa kwa huduma hiyo ya "kiroho", hawatumikii ndugu zake ikiwa anawatolea huduma zingine mia moja au elfu, lakini anapuuza huduma moja tu ambayo mtu ana haki ya kutarajia kutoka kwake na kwamba yeye peke yake anaweza kutoa. Imeandikwa kwamba kuhani huwekwa kwa  ajili ya faida ya wanadamu katika mambo ya Mungu” (Ebr 5: 1). Tatizo hili lilipotokea kwa mara ya kwanza katika Kanisa, Petro alilitatua kwa kusema: “Sio sawa sisi kulipuuza neno la Mungu kwa ajili ya huduma ya meza... Tutajitolea kwa sala na huduma ya Neno” (Mdo 6:2-4).

Wachungaji ambao wamerudi Kantini

Kuna baadhi ya wachungaji ambao, kiukweli, wamerudi kwenye huduma ya canteens, Kantini ametoa mfano Kardinali Canalamessa. Akiwa na maana kwamba wao wanashughulika na aina zote za nyenzo, kiuchumi, kiutawala, wakati mwingine hata za kilimo, shida zilizopo katika jamii yao (hata wakati mwingine wangeweza kuachia  wengine), na wanapuuza huduma yao ya kweli, isiyoweza kutengezwa tena au kubadilishwa. Kwa maana hiyo huduma ya Neno inahitaji masaa ya kusoma sana na maombi. Mara tu baada ya kuwaeleza mitume maana ya kuosha miguu, Yesu aliwaambia“Kwa kuyajua hayo  yote na kuyaweka katika matendo mtabarikiwa” (Yn 13:17). Sisi pia tutabarikiwa, ikiwa hatutaridhika tu na kujua mambo haya yaani kwamba Ekaristi inatusukuma kwenda katika  huduma na kushiriki  lakini tukayaweka katika vitendo, ikiwezekana kuanzia leo hii. Ekaristi si fumbo tu la kuwekwa wakfu, kupokelewa na kuabudiwa; pia ni fumbo la kuiga mfano. Hata hivyo, kabla ya kuhitimisha Kardinali Cantalamesssa alisema, ni lazima tukumbuke ukweli ambao tumeusisitiza katika tafakari zote kuhusu Ekaristi, yaani, tendo la Roho Mtakatifu! Tuwe waangalifu tusipunguze zawadi kwa wajibu wetu! Hatujapokea tu amri ya kuosha miguu yetu na kujitumikia sisi wenyewe: tumepokea neema ya kuweza kufanya hivyo. Utumishi ni karama na kama karama zote ni“udhihirisho fulani wa Roho kwa faida ya wote” (1Kor 12:7); Kila mmoja anaishi kulingana na kipawa chake  (charisma!) Imepokelewa, kwa kuiweka katika huduma ya wengine, anasema mtume Petro katika Waraka wake wa Kwanza (1 Pt 4:10). Zawadi hutangulia wajibu na hufanya utimilifu wake uwezekane. Hii ndiyo habari njema. Injili ambayo kama  Ekaristi ni kumbukumbu ya kila siku ya kufariji.

TAFAKARI YA MWISHO YA KIPINDI CHA KWARESIMA YA KARD.CANTALAMESSA
09 April 2022, 11:35