2022.04.18 Mattia Piccoli akiwa anasuma ushuhuda wake mbele ya Papa Francisko na kwa vijana wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro 2022.04.18 Mattia Piccoli akiwa anasuma ushuhuda wake mbele ya Papa Francisko na kwa vijana wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro 

Moyo wa mtoto

Ushuhuda wa Mattia Piccoli,ambaye amekuwa msimamizi wa baba yake mwenye ugonjwa wa Alzheimer uliwagusa vijana wa majimbo katoliki ya Italia waliokutana na Baba Mtakatifu Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro.“Ninamsaidia baba yangu kama kitendo cha upendo”,alisema mtoto wa miaka kumi na mbili ambaye hata hivyo alitunukiwa na Rais Sergio Mattarella zawadi ya utambuzi wa kujitoa kwa Jamhuri ya Italia.

Na Alessandro Ghisotti

Wakati mwingine ni watoto wadogo ambao wana upendo mkubwa na ujasiri. Katika tukio la sherehe kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo Papa Francisko alikutana na umati wa vijana wa Italia, ushuhuda wa Mattia Piccoli mwenye umri wa miaka kumi na mbili, ambaye kwa miaka kadhaa, amekuwa malaika mlezi wa baba yake mwenye ugonjwa wa Alzheimer, utabaki umeandikwa katika kumbukumbu ya kila mtu. Mattia alitunukiwa hata heshima kuu ya kujitoa wa Jamhuri kutoka kwa Rais Sergio Mattarella, wa Jamhuri ya Italia mnamo Desemba mwaka jana. Motisha wa kutunikiwa hiyo zawadi waliandika kwamba: “Kwa ajili ya upendo na utunzaji ambao yeye anafuatilia ugonjwa wa baba yake kila siku na kumsaidia kupambana nao”.

Upendo huo na utunzaji ambao, tarehe 18 Aprili 2022, Mattia alishuhudia kwa hiari yake, kijana mdogo ambaye alilazimika kukua kwa haraka kusaidia baba yake Paolo. Kwa mujibu wake alisema akiwa anasoma, mara baada ya kuomba radhi kwamba amependelea aandike hili asipate mhemko zaidi mbele yao: “Sikuwahi kufanya chochote bila kupenda au kwa kwa kulazimishwa” wakati Papa na vijana wakimsikiliza kwa makini na hisia kali, kwamba nilitaka kumsaidia baba yangu kama tendo la upendo, nikifikiria juu ya kila kitu alichonifanyia”. Mattia alisimulia kuwa utotoni alifikiria kucheza tu, lakini ghafla alianza kugundua kuwa baba yake hafanani tena naye,alionekana tofauti na wakati mwingine alisahau kufanya vitendo muhimu kama vile kwenda kumchukua shuleni.

“Sikuelewa kilichokuwa kikitokea kwa baba yangu, alisema Mattia na kuendelea “lakini mnamo tarehe 19 Desemba 2016, tulipewa habari kwamba hatua hiyo ingebadilisha maisha ya familia yangu:baba yangu aligunduliwa na Alzheimer ya mapema”. Ugonjwa mbaya sana, ambao unaonekana kutowezekana kwa sababu unalemaza akili na hisia kwa njia ya ajabu na kumpelekea mtu aliyeathiriwa na kuwa nje kabisa na hali yake, kwa kutotambua chochote hata kwa heshima ya upendo na kumbukumbu zinazopendwa zaidi ndani ya familia. Ugonjwa ambao mara nyingi hutupa familia katika mateso na huingia katika hali ya upweke. Lakini hata Alzheimer kwa upande wao haijaweza kumchukua baba kutoka kwa mtoto wake ambao, kwa upendo wa ubunifu na ukaidi, anawaweka karibu naye, hamwachi aende hivyo hivyo peke yake.

Mattia akiendelea alisema “kuanzia siku hiyo kazi yangu, bila msaada wa nje, ilikuwa kumsaidia baba yangu katika mambo ya kila siku ambayo hangeweza tena kufanya peke yake, kama vile kuoga, kufunga viatu vyake au kumpa faraja wakati hakujua yuko wapi na wala afanye nini”. Kwa maana hiyo ni mtoto anayemlinda baba yake. Inamsaidia kuchukua hatua zisizo hakika katika njia ya uzima, kama vile baba yake alivyofanya kwa miaka michache akiwa bado mdogo sana. Itakumbukwa kwamba kwa miezi michache iliyopita tulihitimisha kusherehekea mwaka maalum uliowekwa kwa Mtakatifu Joseph, shuhuda na mfano wa ubaba. Katika historia hii ya ajabu, ni kana kwamba mtoto huyu amechukua sifa bainifu za ubaba, ujasiri, huruma, kukubalika, kumlinda na kumtia moyo baba yake mwenyewe. Kama inavyoeleza Barua ya Baba Mtakatifu Francisko ya Patris Corde yaani moyo wa baba, na sasa unageuka kuonekana ndani ya hisotria hii Filii Corde yaani moyo wa mtoto

Ni wapi, hata hivyo, mtu anaweza kuuliza kwa kufaa, je, mtoto amepata nguvu hizi, upendo huu wote wa kukabiliana na jaribu kubwa zaidi kuliko yeye mwenyewe kutoka wapi? Nguvu hizi lakini alizozieleza kwa umati wa mkutano wa vijana akiwepo Baba Mtakatifu zinatoka “shukrani kwa familia yangu: kwa ujasiri wa mama yangu, kwa msaada wa kaka yangu na hata baba yangu mkubwa ambaye amesaidia watu daima na kunifundisha thamani ya mshikamano. Hata imani ya Kikristo imenisaidia mara nyingi ninapokuwa na huzuni na ninajisikia vibaya, kwa sababu ninamkumbuka sana baba yangu wa wakati ule wa zamani”, Alisisitiza.

Mattia alikumbuka wakati watu wote walipokuwa pamoja kanisani kuwasha mshumaa kuomba kwa imani kuwa maombi yetu yatajibiwa au  jinsi baba yake alivyokuwa anafurahi alipokuwa akiimba katika kwaya ya parokia. Hii ni historia ambayo, kwa upesi wa tukio lililoishi Jumatatu ya Pasaka, liligusa mioyo ya wale walioisikiliza. Kwa maneno machache, kwa dakika chache, Mattia mdogo hivyo alitoa zawadi kubwa: alishuhudia kwamba upendo wa mtoto, umoja wa familia, mshikamano wa jumuiya ya imani unaweza kusaidia kuunga mkono kila jaribu.

USHUHUDA WA MATTIA KWA PAPA NA VIJANA WA KUMTUNZA BABA YAKE
20 April 2022, 16:05