Padre John Mbinda,C.S.Sp,ni Askofu Mpya wa Jimbo katoliki Lodwar,Kenya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo katoliki la Lodwar nchini Kenya, Mhsh, Padre John Mbinda, C.S.Sp., aliyewahi kuwa Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu nchini Kenya na Sudan. Padre Mbinda alizaliwa mnamo tarehe 5 Mei 1973 huko Machakos, katika jimbo hilo. Baada ya majiundo yake katika Seminari ndogo ya Papa Paulo VI, Jimbo la Machakos (1989-1992), alijiunga na Shirika la Roho Mtakatifu na kufunga nadhiri za Milele mnamo tarehe 12 Oktoba 2001. Aliendelea na mafunzo ya Falsafa kati ya (1993-1996) katika Seminari ya Kimisionari nchini Tanzania na Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Tangaza nchini Kenya mnamo (1997-2002).
Alipewa daraja la upadre 2002 na kushika nyazifa za utume kichungaji
Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 18 Mei 2002, na baadaye akashika nyadhifa zifuatazo: Padre wa Utume katoliki Tangulbei (2002-2004) na Paroko wa Utume Katoliki wa Kositei kwa Jimbo Kuu katoliki la Nakuru (2004-2008); Shahada ya Uzamili katika Mafunzo ya Maendeleo katika Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo ya Kimmage, Ireland mnamo (2008-2010); Mchungaji wa Parokia ya Mtakatifu Austine katika Jimbo Kuu la Nairobi na Mkuu wa Ofisi ya Maendeleo ya Shirika lake (2010-2015); Vile vile amekuwa Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu nchini Kenya na Sudan mnamo (2015-2021). Tangu Agosti 2021 hadi wakati wa utezui huo alikuwa katika mwaka wa mapumziko katika Jimbo Kuu la Southwark, Uingereza, na wakati huo huo akijishughulisha na shughuli za kichungaji kama Msaidizi wa Parokia katika Parokia ya Mtakatifu Chad, iliyokabidhiwa kwa Mababa wa Kiroho. Vile vile aliwahi kuwa Profesa katika Chuo Kikuu cha Tangaza (2014-2017); Rais wa Umoja wa Miduara ya Shirika la Roho Mtakatifu Afrika Mashariki(UCEAF) mnamo (2015-2016) na Mshauri wa Jimbo Kuu la la Nairobi (2016-2020).