Tafuta

2022.04.05 Baba Mtakatifu Francisko amekabidhi Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa familia 2022.04.05 Baba Mtakatifu Francisko amekabidhi Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa familia 

Papa amekabidhi tafakari ya Njia ya Msalaba kwa Familia

Ni familia za jumuiya na vyama katoliki vya kujitolea na kusaidia ambavyo vimechaguliwa kubeba Msalaba katika njia ya Msalaba ijayo.Amesema hayo Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk.Matteo Bruni,kuhusiana na Muktadha wa Siku ya Ijumaa Kuu katika Colosseo ambapo Familia hizo zitapokezana msalaba katika vituo 12 njia ya msalaba.Ni katika fursa ya Mwaka wa 5 wa Amoris laetitia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya mwaka wa Familia ambapo Mama Kanisa anaadhimisha miaka mitano ya Wosia wa Kitume wa Amoris laetitia, Papa Francisko ameamua kuwakabidhi tafakari na sala kwa ajili ya vituo vya Njia ya Msalaba, kwa siku ya Ijumaa Kuu trehe 15 Aprili kwa baadhi ya familia. Amesema hayo Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni, akieleza kuwa hizo ni familia ambazo zimefungamanishwa na jumuiya na vyama katoliki vya kujitolea na kutunza. Katika mantiki ya uchaguzi, watakuwa ni familia ambazo zitabeba msalaba kati ya kituo na kituo kingine. Kama ilivyokuwa ikwisha tajwa mwezi Machi kuhusu, Njia ya Msalaba kurudi kufanyika  katika eneo la kiutamaduni la Colosseo mara  baada ya miaka 2 ya kusimamishwa na kufanyika ibada hiyo katika Uwanja wa Mtakatifu Pero kwa sababu na virusi vya Uviko.

Mnamo 2021 walioandaa tafakari walikuwa ni watoto wa kikundi cha Scout- Agesci wa “Foligno  (Umbria) na wa Parokia moja ya Roma ya Watakatifu Mashaidi wa Uganda. Watoto walikuwa wamesimulia mateso yao,  makubwa na madogo kwa mtindo wao ambayo yanasindikiza maisha yao ya kila siku, kuanzia na giza hasa kuachwa na upweke, uzoefu wa vikwazo, kuanza  kwa upya shule mara baada ya karantini, kugombana na wazazi  wao hadi kufikia hofu ya kuenea kwa virusi vya Covid ambavyo waliona wananyimwa sana muda wa kukaa na marafiki

Na mnamo mwaka 2020, maarufu kwa usaambaji mkali sana wa virusi, waliotoa tafakari walikuwa ni wafungwa wa kizuizini, wa  “Due Palazzi”huko Padua, Italia ambao waliandaa Njia ya Msalaba. Katika tafakari yao,ilisikika uchungu wa familia iliyokuwa imepoteza mpendwa kwa sababu ya mauaji, au mtoto wa mwanaume aliyefungwa kifungo cha maisha; mateso ya mama mfungwa na matumaini ya Padre aliyekuwa amehukumiwa na baadaye kupata haki baaada ya miaka 8 ya mchakato wa mahakama.  Mhusika wa elimu katika magereza na mwanasheria mlinzi. Kazi ya Katekista, Ndugu wa kujitolea,  Polisi wa Magereza. Kwa ujumba zilikuwa ni hali mbali mbali za maisha ambazo zinapelekwa kwenye Njia ya msalaba na ambazo zimegeukuwa kuwa kweli  Njia ya Msalaba.

08 April 2022, 17:06