Papa Francisko amemshukuru Bikira Maria kwa safari ya Malta
Baba Francisko amekwenda na kusali kwa kushukuru mbele ya picha ya Bikira Maria kurudi salama kutoka ziara yake ya kitume, na ambaye kabla ya kuondoka alikuwa amekwenda hapo kukabidhi Mama Maria Hija ya 36 ya kitume kimataifa.
VATICAN NEWS
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu asubuhi tarehe 4 Aprili 2022 , mara baada ya kumaliza ziara yake ya kitume ya 36 kimataifa, amekwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu na kusali mbele ya picha ya Bikira Maria Salus Populi Romani.
Kwa mujibu wa msemajki wa Vyombo vya Habari Vatican, amethibitisha kuwa, Baba Mtakatifu amemshukuru Bikira Maria kwa ziara hiyo na ambaye alikuwa tayari amemkabidhi ziara hiyo kabla ya kuondoka kama kawaida ya kwenda nje ya Italia mchana tarehe Mosi, Aprili 2022. na baada ya ziara yake hiyo ya sala katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, Papa amerudia jijini Vatican.
04 April 2022, 16:15