Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon tarehe 28 Aprili 2022 amekutana na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon tarehe 28 Aprili 2022 amekutana na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. 

Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon Akutana na Papa Francisko Mjini Vatican

Papa Francisko na Rais wa Gabon wamegusia kumbukizi la Miaka 25 ya Mkataba wa Pamoja na kwamba wameonesha nia ya kutaka kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizi mbili. Wamelipongeza Kanisa kwa mchango wake katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Gabon, hususan kwenye sekta ya elimu. Wamejadili pia masuala ya kikanda na kimataifa

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi, tarehe 28 Aprili 2022 amekutana na kuzungumza na Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon, ambaye baadaye amebahatika kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu na Rais wa Gabon wameridhishwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya Nchi hizi mbili.

Viongozi hawa wameridhishwa na mahusiano ya kidiplomasia kati yao.
Viongozi hawa wameridhishwa na mahusiano ya kidiplomasia kati yao.

Viongozi hawa pia wamegusia kumbukizi la Miaka 25 ya Mkataba wa Pamoja na kwamba, viongozi hawa wameonesha nia ya kutaka kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizi mbili. Wamelipongeza Kanisa kwa mchango wake katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Gabon, hususan kwenye sekta ya elimu. Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko pamoja na mgeni wake, wamejielekeza pia katika masuala ya kiuchumi na kijamii nchini Gabon bila kusahau masuala ya Kikanda na Kimataifa yanayoendelea kushika kasi kwa wakati huu.

Papa Rais wa Gabon
28 April 2022, 15:10