Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
ROZARI TAKATIFU KWA KILATINI
Ratiba Podcast
Msikiti wa Mtakatifu Sofia huko Uturuki Msikiti wa Mtakatifu Sofia huko Uturuki 

Ujumbe wa Ramadhani:Wakristo na waislamu tunashirikishana furaha na uchungu!

Waislamu na wakristo tushirikishane pamoja furaha na uchungu ndiyo mada ambayo inaongoza ujumbe wa Ramadhani kutoka Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya Kidini.Janga na matokeo ya maisha ya kila mmoja yanatakiwa kukabiliwa kwa uhakika kwamba upendo wa Mungu unakumbatia kila mtu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mara nyingine tena, dharura ya kiafya inakuwa fursa ya kuweza kutafakari kuhusu janga hili lilivyo badili namna yetu ya kuishi maisha. Katika Ujumbe wa mwezi mtukufu wa Ramadhani uliotiwa saini na Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya Kidini Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, na Katibu Monsinyo Indunil Kodithuwakku Janakaratne Kankanamalage, unaongozwa na mada: “Wakristo na waislamu: tunashirikishane furaha na uchungu”. Katika hati hiyo inabainisha wazi juu ya umuhimu wa kuishi kwa pamoja katika kipindi cha giza lakini pia hata kile cha mwanga kwa sababu, upendo wa Mungu unakumbatia kila mmoja na ulimwengu wote.

Shukrani kwa Mungu kwa kulinda watu wake 

Wakati wa kipindi cha mfungo mtukufu wa Ramadhani ambayo kwa kawaida uhitimishwa na siku kuu ya ‘Id al-Fitr, wazo la viongozi hao wa baraza la Kipapa, wanamshukuru Mungu Mwenyezi kwa uwezo wake wa kulinda watu wote kwa wema wake. Ujumbe unabainisha pia jinsi ambavyo wanasali kwa ajili ya marehemu, wagonjwa kwa uchungu na tumaini.  Janga limepelekea hata kufikiria ushirikishwaji si tu wa mali lakini hata uwepo wa mambo kama hewa, maji, maisha, chakula, nyumba na hata matunda ya maendeleo katika uwanja wa madawa na tiba, matokeo ya maendeleo ya kisayansi na kiufundi katika nyanja mbali mbali. Ushirikishwaji na hasa kukaa pamoja na mwenye kuhitaji, ambayo ni sawa na uwajibikaji hasa hasa kwa mtazamo wa wale ambao wamepoteza kazi au wenye matatioz ya kiuchumi, kwa sababu hasa ya virusi vya vuko.

Ushirikishwaji unapata nafasi kwa sababu ya utambuzu wa sisi ni nani

Ushirikishwaji, unapata nafasi kuu na sababu yake kuu katika utambuzi kuwa kile ambacho sisi ni… na kile ambacho tunacho ni zawadi ya Mungu ambayo matokeo yake  tunapaswa kuweka talanta zetu katika huduma kwa ajili ya wote, kwa kaka na dada, kwa kushirikisha na wao kile tulicho nacho. Kati ya furaha hata sikukuu za kidini, tunashirikishana nao furaha kwa ajili ya kusheherekea siku kuu bila kulazimika kujitengenezea mwelekeo wa kidini wa tukio linaloadhimishwa. Katika uchungu lakini, kuna haja kubwa ya ukaribu na mshakamano wa marafiki. Katika matumaini ambayo ni kuendelea na kushirikishana na katika ishara ya umoja wa ubinadamu, na udugu ambao unatokana na hili. Ujumbe wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Mazungumzo ya Kidini, wanahitimishwa kwa kuwatakia amani na mafanikio ya mfungo mwema wa Ramadhani na furaha ya kusheherekea ‘Id al-Fitr”.

UJUMBE KUTOKA MABARA ZA KIPAPA LA MAZUNGUMZO YA KIDINI KWA MWEZI RAMADHANI
09 Aprili 2022, 17:02
Prev
February 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
232425262728 
Next
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031