Tafuta

2022.05.20 Askofu Mkuu Gallagher akisali mbele ya Kaburi la Halaiki huko karibu na Kiev nchini Ukraine. 2022.05.20 Askofu Mkuu Gallagher akisali mbele ya Kaburi la Halaiki huko karibu na Kiev nchini Ukraine. 

Askofu Mkuu Ghallagher amesali katika kaburi la halaiki&majeraha ni ya kina

Akiwa katika ziara yake kwa ajili ya ukaribu wa watu wanaotesaka nchini Ukraine,Ijumaa 20 Mei,Askofu Mkuu Ghallagher amehojiana na Stefano Leszczynski mara baada ya sala mbele ya kaburi la halaiki huko Bucha,karibu na Kiev ambapo amesema alivyoguswa na kile alichokiona na maneno ya nguvu na matumaini kwa watu walioharibiwa na vita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ziara nchini Ukraine ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Ushirikiano na Nchi, ameweza kupeleka ukaribu wa Papa Francisko kwa watu ambao wanaendelea kuteseka na vita. Yafuatayo ni mahojiano yaliyofanywa na na Stefano Leszczynski kwa Askofu Mkuu Gallagher, kuhusiana na hali halisi na uzoefu aliofanya katika maeneo aliyotembelea:

Ziara nchini Ukraine ya Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na mataifa
Ziara nchini Ukraine ya Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na mataifa

Tumetembelea maeneo ya mashahidi wa Ukraine, karibu na Kiev, Bucha, Irpen, Vorzel, haya ni maneno yaliyopata pigo kali na mauaji makubwa, na kujionea hata maeno ya mazishi ya halaiki, nyuma ya Kanisa la Kiorthodox la Ukraine...

Kwa hakika nimeguswa kwa kina na uzoefu huu, kwa sababu mmoja anakwenda katika nchi huko Bucha, kwa mfano, mji uliokuwa wa kisasa, wa kisasa kama miji mingine ya sehemu za Ulaya, na unajikuta mbele ya hali halisi, hapa wamezika mamia ya watu. Mtu hawezi kufikiria ... baadaye tukaona picha kwenye kizimba cha Kanisa la Kiorthodox, picha zilizochukuliwa wakati wa kutoa na kutambulisha miili... hii, bila shaka, inavunja moyo. Ni jambo la kutisha kwa sababu mambo haya yalifanywa na watu dhidi ya watu wengine, na yalifanywa bure, yalifanyika kwa raia, yakifanywa kwa njia ya kikatili kabisa. Na hii ni kweli ya kutisha. Sisi ni mashuhuda wa hili, wa mateso na mauaji ya nchi hii.

 Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na mataifa akitazama Picha za utambulisho wa miili
Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na mataifa akitazama Picha za utambulisho wa miili

Inawezekanaje kupata amani katika Nchi ambayo umeona hayo?

Watu wa Ukraine watapata amani kati yao, lakini majeraha ni ya kina na itachukua muda mrefu zaidi kupata amani na Urussi, pamoja na watu ambao wamehusika katika mzozo huu mbaya, katika vita hivi. Majeraha ni ya kina: ni vigumu sasa kuzungumza juu ya amani, ya upatanisho, kwa sababu katika mioyo ya watu, mateso na majeraha ni ya kina sana na hivyo muda kiukweli lazima utolewe. Inapaswa kutoa muda, inapaswa kuruhusu watu kuzungumza, pia kuelezea hisia nyingi mbaya kwa wengine. Kwa njia hiyo inahitaji kusali sana, kwamba Bwana, ambaye kwa hakika ndiye wokovu wa pekee, atupe neema ya kuponya majeraha haya na kwamba watu waweze kwenda mbele. Jambo moja ambalo limenigusa sana siku hizi ni ujasiri kiasi gani, kwa nia gani watu wa Ukreni wanajaribu kutengeneza chemchemi hii ambayo tunaona katika mashamba na misitu na vichaka, kwamba hiyo ndiyo kuzaliwa kwa upya kwa nchi hii. Hawa wanajaribu kujenga upya, kusafisha, kurejesha mambo, kwa moyo mkuu, kwa ujasiri mkubwa. Na wanastahili pongezi na heshima yetu yote.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Bucha, Vorzel, Irpen haya ni majina ya miji ambayo imekuwa ishara ya kutisha ya mzozo wa Ukraine. Maeneo ambayo Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa, ametembelea tarehe 20 Mei 2022 akifuatana na Balozi wa Vatican nchini humo. Sala ilikuwa ya kuguswa iliyofanyika mbele ya kaburi la halaiki karibu na Kanisa la Kiorthodox la Mtakatifu Andrea, ambapo kuna takriban miili 100 ambayo haikuwa na majina na kati yao kuna watoto pia. Askofu Mkuu Gallagher pia alisimama katika seminari ya Vorzel ambayo ilikuwa imechukuliwa na kuharibiwa na askari wa Kirussi. Cha kushangaza zaidi ilikuwa ni mabaki ya sanamu ya Bikira Maria, iliyoharibiwa na vipande vya bomu.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Askofu Mkuu aidha alifanya Mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Dmytro Kuleba na afla  katika ukumbusho wa waliofariki kwa ajili ya Ukraine. Kuna matarajio makubwa ya mkutano na waandishi wa habari,  utakaofuata mkutano wa kitaasisi utakaofuata mwingine ambao ulikuwa tayari umefanyika Vatican. Alhamisi 19 Mei 2022 Askofu Mkuu alikutana na Askofu Mkuu Sviatoslav Shevchuk, wa Kiev, wa Kanisa la Kigiriki-Katoliki la Kiukreni kwenye Kanisa Kuu la Ufufuko. Hii ilifuatiwa na mazungumzo mafupi ya faragha na Askofu Mkuu Shevchuk  ambaye alikumbuka siku za giza zaidi za vita na ulinzi wa kishujaa wa jiji na wenyeji wake.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Kwa njia hiyo Katibu wa Vatican wa mahusiano na ushirikiano na mataifa alitaka kusisitizia ukaribu wa Papa, unaoshuhudiwa na uwepo wake mjini Kiev na juhudi zinazofanywa kuhimiza mazungumzo yoyote yanayoweza kuleta amani. Juu ya ardhi katika mkoa wa Kiev, hali inaonekana shwari hata kama siku inasikika kengele zinazotoa tahadhali ya kujilinda dhidi ya ndege za kivita.

20 May 2022, 14:15