Tafuta

Matokeo ya vita yana athari juu ya kuongezeka kwa bei ya chakula na malighafi, na yanatishia kuzalisha mivutano mipya ya asili ya kijamii kutokana na uhaba wa chakula. Matokeo ya vita yana athari juu ya kuongezeka kwa bei ya chakula na malighafi, na yanatishia kuzalisha mivutano mipya ya asili ya kijamii kutokana na uhaba wa chakula. 

Chica Arellano:kuna hitaji la dharura kukabiliana na lishe katika mazingira magumu

Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika FAO,IFAD na WFP,ambaye alizungumza katika Mkutano wa 33 wa FAO wa Kikanda barani Ulaya huko Łódź, Poland alisema:"Matokeo ya vita yana athari juu ya kuongezeka kwa bei ya chakula na malighafi na yanatishia kuzalisha mivutano mpya ya asili ya kijamii kutokana na uhaba wa chakula,uchumi na lishe kwa walio katika mazingira magumu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maombi yasiyokoma ya mwisho wa uhasama"na amani irudi yameelezwa na  Monsinyo Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la FAO, Ifad na WFP, akizungumza kuhusu matakwa ya Papa kwa ajili ya Ukraine katika kikao cha 33 cha Mkutano wa FAO wa Kikanda wa Ulaya huko Łódź, nchini Poland. Tukio hilo lililofunguliwa tarehe 10 na litakamilika siku ya  Ijumaa  tarehe 13 Mei 2022. Katika hotuba yake, aliyoitoa mbele ya mamlaka ya serikali ya Poland na utawala wa eneo la Łódź, Mwakilishi huyo alianza kwa kuthibitisha kwamba kinachotokea karibu na mipaka ya Poland, katikati mwa Ulaya, na pia katika mazingira mengine yaliyo sambaratishwa na utumiaji wa jeuri usio na maana, ukatili na usio na sababu, inamtia uchungu sana Papa.

Chanzo cha uchungu wa Vatican, alisema Monsinyo Chica Arellano, pia ni kutelekezwa kwa mashamba ya kilimo na shughuli za kijeshi, uharibifu mkubwa unaosababishwa na mazao, ukosefu wa kazi ya kilimo kutokana na kuhama kwa watu wote, uharibifu wa asili, rasilimali na miundombinu. Matokeo yao, aliongeza, husababisha kuzorota kwa minyororo ya ugavi, kuathiri ongezeko la bei ya chakula na malighafi, na kutishia kuzalisha mivutano mipya ya kijamii kutokana na uhaba wa chakula na kutopatikana. Pia vita hivyo vina athari mbaya kwa nchi zilizo na uchumi dhaifu ambao unategemea mauzo ya nje ya Kiukreni na Urussi.

Kwa mwakilishi huyo wa Vatican amebainisha kuwa huu sio upepo wa kiafya ambao unaathiri idadi ya watu maskini zaidi kwenye sayari, ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya vijijini na wameathiriwa zaidi na upanuzi wa mgawanyo usio sawa wa maliasili na malighafi, na ongezeko la matokeo  katika viwango vya umaskini uliokithiri na wa wastani na kuongezeka kwa njaa. Kwa njia hiyo hali ambayo tayari haikubaliki ya kanda nyingi zina hatari ya kuwa na mzunguko mbaya wa migogoro na umaskini.

Monsinyo Chica Arellano akiendelea pia alielezea matumaini ya Vatican kwamba mataifa yarejee kwenye mazungumzo na michakato ya mazungumzo na kwamba nchi zote zifanye kazi kwa mshikamano kushughulikia mahitaji ya haraka ya lishe ya watu wote walio katika mazingira magumu, hasa wakimbizi, wazee, walemavu na watoto. Kwa maana hiyo shukrani kwa nchi zote ambazo zimeiga dhamira na ukarimu wa taifa la Poland, kwa mshikamano ambao wanatoa misaada ya kibinadamu kwa wale ambao wamelazimika kukimbia ardhi yao kutokana na wazimu wa vurugu potovu.

11 May 2022, 18:17