Davos:Kupambana dhidi ya ukosefu wa usawa na msaada wa Laudato si’
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) 2022 linajikita na changamoto za kijiografia ambazo hazijawahi kushuhudiwa duniani ambazo serikali zinakabiliana nazo hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kufufuka kwa uchumi baada ya janga la UVIKO-19, mgogoro wa Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Mkutano huo, unaoongozwa na kauli mbiu: "Historia katika hatua ya Mabadiliko: Sera za Serikali na Mikakati ya Kibiashara," ambalo lilifunguliwa mnamo Dominika tarehe 22 - 26 Mei 2022 huko Davos, nchini Uswiss.
Mazungumzo huko Davos ili kuweza kupambana na ukosefu wa usawa kwa ngazi za Ulimwengu, katika ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi duniani Oxfam ambalo ni Shirikisho la Kimataifa la Mashirika 20 yasiyo ya Kiserikali linalofanya kazi na washirika katika mataifa zaidi ya 90 kwa lengo la kukomesha dhuluma zinazosababisha umasikini, limeomba kuweka kodi kubwa kwa makundi makubwa na urithi mkubwa. Kwa mujibu wa Oxfam, linasema matokeo ya janga na kuongezeka kwa bei haraka kunaongezea umaskini zaidi. Sambamba na mazungumzo ya Davos, muungano wa Global Solidarity Fund" yaani ‘Mfuko wa mshikimano ulimwenguni” kwa sasa unaandaa mabaraza ya majadiliano. Dominika 22 Mei jioni, miongoni mwa mambo mengine, yalikuwa ni umuhimu wa waraka wa Laudato si ' ambapo ulijadiliwa na zaidi katika fursa ya Juma la Laudato Si lililozinduliwa 22 Mei na Papa Francisko. Maonesho ya picha pia yaliwasilishwa, ambayo yaliyotungwa na mwandishi wa Italia Lia Beltrami. Maonesho hayo tayari yalitembelewa mnamo Februari mwaka huu chini ya nguzo za Uwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican. “Kwa picha hizo tulitaka kuangazia dhuluma nchini Bangladesh”, Lia Beltrami, alisema kwa mwandishi wa Vatican News aliyeko Davos. Kwa kuongezea alisema "Picha zinaonesha athari za matokeo mabaya ambayo tayari Papa Francisko alishutumu".
Na Katibu mtendaji wa Umoja wa Mama Wakuu wa Mashirika ya kitawa (UISG), Sista Patricia Murray, katika mahojiano na Vatican News alieleza jinsi ilivyo muhimu kwa jumuiya za kitawa kufanya mazungumzo na wanauchumi. “Ikiwa tu tunaweza kufanya mazungumzo tunaweza kufikia kitu, alisema mtawa, na baadaye akatangaza kwamba anathamini sana mazungumzo haya ya Davos kwa sababu katika vikao hivyo ivya majadiliano mtu anaweza kuzungumza moja kwa moja na wale wanaohusika. “Wako wazi sana kwa maombi yetu, Sr. Murray alisema. Naye Mkurugenzi mtendaji wa "Global Solidarity Fund" yaani Muungano wa Mfuko wa mshikamano Ulimwenguni, Bi Marta Guglielmetti, alisisitiza katika vipaza sauti vya Vatican kwamba wanauchumi wanapendezwa sana na ujumbe wa Papa Francisko. "Katika Waraka wake Papa Francisko, alisema Guglielmetti anaonesha matatizo madhubuti na pia anatoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo".
Hata hivyo Waandaaji wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) wamebainisha kwamba baada ya kusimama kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la UVIKO-19, ikifuatiwa na mgogoro wa Ukraine na changamoto zingine za uchumi kijiografia, jukwaa linalofanyika kwa wakati huu ambao ni muhimu. Jukwaa hilo linawakutanisha pamoja viongozi na wataalam karibu 2,500 kutoka duniani kote, kwa nia ya kuunganisha tena, kubadilishana maarifa, kupata mitazamo mipya na suluhisho za mapema. Jukwaa la mwwaka 2022 kwa maana hiyo ni la kwanza linalowakutanisha pamoja viongozi wa Dunia katika hali hii mpya ya Dunia kuwa na usawa wa nguvu miongoni mwa nchi hususani zile kubwa kutokana na janga la UVIKO-19 na vita kwa mujibu wa Klaus Schwab, mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF).
Na katika ukweli kwamba washiriki hao wanatoka katika nyanja tofauti za siasa, mashirika ya kiraia ya kibiashara na vyombo vya habari ambapo wanaokutana ana kwa ana, inaonesha hitaji la jukwaa la kimataifa linaloaminika, lisilo rasmi na lenye mwelekeo wa kuchukua hatua kukabiliana na masuala katika Dunia inayoongozwa na mgogoro. Zaidi ya wakuu wa nchi na serikali wapatao 50 wanashiriki, kwa mujibu wa WEF. Na zaidi ya viongozi 1,250 kutoka sekta ya kibinafsi pia wanashiriki, pamoja na Wavumbuzi wa Kimataifa na Waanzilishi wa Teknolojia wanaofikia 100. Kwa maana hiyo WEF imesema, ajenda ya jukwaa hioyo inazizingatia mada sita, ikijumuisha: kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda; kufanikisha kufufuka kwa uchumi na kutengeneza zama mpya ya ukuaji; kujenga jamii zenye afya na usawa; kulinda tabianchi, chakula na mazingira ya asili; kuendesha mageuzi ya sekta ya viwanda; na kutumia nguvu ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.