Kard.Parolin Ulaya iendelea kuwa mpango wa amani
Na Angella Rwezaula –Vatican.
Ulaya ambayo, licha ya hofu ya mzozo unaoendelea nchini Ukraine, bado inaendeleza mpango wa amani ambao ulikuwa msukumo na hamu ya Robert Schumann, na mpango ulio ibuka kutoka kwa vifusi vya Vita vya Kidunia vya pili. Ndivyo alisema Katibu wa wa Vatican Kardinali Pietro Parolin na ndiyo matumaini yake kwamba unaendelea mustakabali wa Bara la Kale. Alisema hayo Kardinali Paroli wakati wa Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Sofia mjini Roma, kwa kuadhimisha Siku ya Ulaya ifanyikayo kila tarehe 9 Mei yak ila mwaka.
Katika Kanisa hili la Mtakatifu Sofia kwa Wa ukrane, tangu kuzuka kwa vita kimekuwa kituo cha kukusanya misaada kwa watu, ambapo Kardinali Parolin akikaribishwa na nyimbo za kiliturujia alikumbuka vifo vingi kwa kile ambacho Papa Francisko amefafanua kuwa ni vita vya kikatili na vya kukufuru. Tunaomba kutoka kwa Mungu zawadi ya amani kwa Ukraine, faraja ya kimwili na ya kiroho kwa waathirika wa vita na hasa kwa wakimbizi, kwa watoto, kwa wale ambao wamepoteza kila kitu, kwa wale walioachwa peke yao. Bwana aangazie mioyo ya watawala ili wafanye kazi ya kurejesha amani na maelewano, alisema kardinali, mbele ya mabalozi wengi walioidhinishwa na Vatican.
Katika mahubiri yake, Katibu wa Vatican alitoa maoni yake juu ya neno la Mungu lililopendekezwa na liturujia ya siku, linalojaa mawazo ya thamani ambayo alisema “yanatusaidia kuingia kwa undani katika fumbo la Pasaka ya Bwana”. Alifafanua aidha maana kifo, cha Kristo, Mchungaji Mwema, anayerudisha uzima. “Kwa njia ya Pasaka Bwana Yesu hutufungulia milango ya uzima wa milele. Mauti haina nguvu tena, imeshindwa katika mwili wa Mkombozi. Yesu anatufungulia njia kuelekea Ule wa Milele, Yeye ndiye njia, mlango wa kupitia ili kuingia katika uzima wa kweli”. Hata hivyo, ushindi wa Kristo “unaonekana kung’ang’ana kuonyesha ushindi wake”, karibu “kufifia” katika ulimwengu huu ambamo “dhambi na mauti vinaonekana kutawala”.
Matukio yanayotoka Ukraine alisema yanatukumbusha kila siku. Mbele ya kukabiliana na majanga yaliyosababishwa na vita, Kardinali Parolin anakumbuka roho ambayo ilihuisha Azimio la kukumbukwa la Robert Schumann, ambapo mnamoo tarehe 9 Mei 1950, miaka mitano baada ya mzozo ulioenea zaidi na wa umwagaji damu ambao Ulaya ilikuwa imejua hadi wakati huo. Wakati huo huo aliye kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Schumann alielewa kuwa njia pekee ya kuepusha hatari ya mzozo mpya haikuwa kuzuia, wala katika kujenga amani ya silaha kama Vita Baridi; badala yake alihisi kwamba ni mshikamano wa pande zote na kugawana rasilimali pekee ndio kunaweza kuleta upatanisho wa kweli. Na hivi ndivyo njia ya kuelekea shirikisho la Ulaya ilianza kufuatiliwa, na hivi ndivyo hatima ya kanda ambayo kwa muda mrefu ilijitolea kwa utengenezaji wa zana za vita ilibadilika.