Papa atuma salamu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Angelo Sodano
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametuma salamu za rambi rambi kufutia na kifo cha Kardinali Angelo Sodano, Katibu Mstaafu wa Vatican na Dekano Mstaafu wa Baraza la Makardinali aliyeaga Dunia jioni tarehe 27 Mei 2022. Papa anamkumbuka mwanaume aliyependwa wa Kanisa, ambaye aliishi kwa ukarimu wa ukuhani wake kwanza jimbo Kuu la Asti na baadaye katika maisha yake marefu katika huduma ya Vatican. Anamkumbuka shughuli zake akiwa karibu na Mapapa wawili Watangulizi wake ambao walimkabidhi majukumu muhimu ya kidiplomasia ya Vatican hadi kufikia Ofisi ya Katibu wa Vatican. Aliweza kuwakilisha Vatican nchini Equador, Uruguay na Chile na kujikita kwa dhati katika wema wa watu huku akihamasisha mazungumzo na mapatano.
Papa Francisko katika salamu hizo amebainisha jinsi alivyoweza kufaidika kwa huduma yake adhimu katika utume wake hasa wakati alikuwa Dekano wa Baraza la Makardinali. Na kwa kila jukumu Palilikabidhiwa Papa amesema alionesha kama mwanaume wa Kanisa, mwenye nidhamu, wa upendo wa kichungaji kwa kuongozwa na utashi wa kuendeza kila mahali chachu ya Injili. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anainua kwa Mungu Baba wa Huruma sala zale kwa ajili ya roho ya Kardinali huyo ili ampokee katika Umilele. Na wakati huo houo ameelezea ukaribu wake kwa familia na jumuiya nzima ya Asti na kuwatumia baraka zake wale wote wanaoshiriki uchungu wa kuondokewa naye, na kwa namna ya pekee watawa wa Mtakatifu Marta na wale ambao walimsindikiza kwa upendo.
Wasifu wa Kardinali Sodano
Kardinali Angelo Sodano, ameaga dunia Ijumaa Jioni 27 Mei 2022 akiwa na umri wa miaka 94. Alikuwa ni Katibu wa Vatican wakati wa Upapa wa Mtakatifu Yohane Paulo II na Papa Mstaafu Benedikto XVI na Dekano Mstaafu wa Baraza la Makardinali. Kardinali tang tarehe 9 Mei alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Columbus- Gemelli Roma kufuatia na kuambukizwa na Uviko. Kardinali alishika wadhifa wa Katibu wa Vatican kuanzia mwaka 1991 hadi 2006 na alikuwa Dekano wa Baraza la Makardinali kuanzia mwaka 2005 hadi 2019. Yeye ni Mtoto wa pili kati ya watoto sita, na alizaliwa kisiwa cha Asti, Mkoa wa Piemonte mnamo tarehe 13 Novemba 1927. Wazazi wake Giovanni na Delfina Sodano walikuwa familia ya vijiji vya Piemonte, familia ambayo ilitoa mchango mkubwa kwa maisha ya Kanisa na Serikali. Baba yake pia alikuwa mjumbe wa Bunge la Italia tangu 1948 hadi 1963, kwa mihula mitatu. Angelo akiwa kijana alimaliza masomo yake ya falsafa na taalimungu katika seminari ya kiaskofu ya Asti, lakini huko Roma ndipo alipata shahada yake ya mara mbili: ya taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na katika sheria ya Kanoni katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano.
Mnamo tarehe 23 Septemba 1950 ni tarehe ya kupewa daraja la kikuhani, iliyopokelewa katika Kanisa Kuu la Asti. Mafundisho ya taalimungu ya kweli na utume kati ya vijana wanafunzi ni sifa ya miaka ya kwanza ya huduma yake. Tayari mnamo 1959 aliitwa na Kadinali Angelo dell'Acqua, wakati huo akiwa Msaidizi wa Sekretarieti Vatican, katika huduma ya Vatican. Alihudhuria kozi za Chuo cha Kipapa cha Kikanisa, na baadaye akatumwa kwenye Ofisi za Ubalozi wa Vatican huko Equador, Uruguay na Chile, kama katibu wa Ubalozi. Mnamo mwaka 1968 alirejea Roma ambako kwa muongo mmoja alihudumu katika Baraza la Masuala ya Umma kwa Kanisa. Mjumbe wa Tume za Vatican kwa kutembelea Nchi za Romania, Hungaria na Ujerumani Mashariki.
Tarehe 30 Novemba 1977, Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa askofu mkuu wa Nova ya Cesare na Balozi wa Kitume nchini Chile. Wiki chache baadaye, tarehe 15 Januari 1978, alipata daraja la uaskofu katika mikono ya Kardinali Antonio Samorè katika Kanisa la Mtakatifu Secondo, huko Asti. Katika nchi ya Amerika ya Kusini alifanya kazi kwa miaka kumi: alitembelea karibu majimbo yote na alishirikiana katika hitimisho la mafanikio la upatanishi wa kipapa kati ya Chile na Argentina. Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 1988 alimwita kuchukua nafasi ya Kardinali Achille Silvestini katika ofisi ya Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa na kujikita wakati huo kwa namna ya pekee na Tume ya Kipapa ya Urussi, ambayo alikuwa rais wake.
Amewakilisha Vatican katika mikutano mbalimbali ya kimataifa kama vile mikutano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Mkutano wa Usalama na Ushirikiano barani Ulaya(OSCE). Mnamo Desemba 1990 alishika wadhifa wa Katibu Msaidizi wa Vatican na kuwa Katibu wa Vatican mnamo tarehe 29 Juni 1991, siku moja baada ya kuundwa kuwa Kardinali. Mwaka 2002 alichaguliwa kuwa Makamu wa Baraza la Makadinali. Alishiriki katika mkutano wa mwaka 2005 ulioweza kumchagua Papa Mstaafu Benedikto XVI, ambaye, baada ya kukaa kwenye kiti cha upapa, akamteua tena kuwa Katibu wa Vatican mnamo tarehe 30 Aprili 2005 na kuidhinisha kuchaguliwa kwake kama Dekano wa Baraza la Makardinali, nafasi aliyoshikilia hadi hapo wakati ambapo Joseph Ratzinger mwenyewe miezi michache baadaye Papa alikubali kujiuzulu kwake kutoka wadhifa wa Katibu wa Vatican. Alifuatiwa na Kardinali Tarcisio Bertone. Mnamo 2019 Papa Francisko alikubali maombi ya kung’atuka kwake Sodano kutoka wadhifa wa Dekano wa Baraza la Makardinali. Hapo awali kwa kuteuliwa na Papa alishiriki mwaka 2014 katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu “Changamoto za kichungaji katika familia katika muktadha wa uinjilishaji” na mwaka mmoja baadaye katika Sinodi ya XIV wenye kaulimbiu “Wito na utume wa familia katika Kanisa na katika ulimwengu wa sasa”.
Kwa kifo cha Kardinali Angelo Sodano, Baraza la makadinali linaundwa na makadinali 208 ambapo 117 ni wapiga kura na 91 sio wapiga kura.