Siku Kuu ya Bikira Maria wa Fatima
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kila mwaka Mama Kanisa tarehe 13 Mei ya anaadhimisha Kumbukumbu ya Bikira Maria wa Fatima. Kwa mwaka 2022, Kanisa linafanya kumbu kumbu ya Miaka 41 tangu Jaribio la kutaka kumuua Mtakatifu Yohane Paulo II lilipofanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican mnamo tarehe 13 Mei 1981. Baada ya kupona Mtakatifu Yohane Paulo II alikiri kwa imani kwamba, Bikira Maria wa Fatima ndiye aliyeokoa maisha yake wakati wa jaribio la kutaka kutoka katika uso wa dunia lililofanywa na Mehmet Ali Ağca. “Kuwa hapa tarehe 13 Mei ina maana hasa kujibu wito wa maelfu na maelfu ya mahujaji wanaokuja kusali kwa kina kwa moyo safi wa Bikira Maria,kwa ajili ya ulimwengu ulijruhiwa na mateso kwa sababu ya kukosa amani. Ndivyo amesema Askofu Mkuu Edgar Peña Parra katika mahubiri yake katika Madhabau ya Fatima katika siku kuu ya kumbu kumbuka kutokewa kwa Bikira Maria kwa watoto wachungaji watatu.
Katibu msaidizi wa Vatican amekumbuka mwito wa Papa wa kusali rosari takatifu kila siku kwa ajili ya Amani, kwa maana ndiye Malkia wa amani na mama wa Mfalme wa amani ambaye analeta maisha mapya katika ulimwengu ambao Maria mwenyewe alitokea tena”. Aidha amesisitiza ukuu msingi wa kusikiliza katika maisha ya kikristo. Hata kwa ngazi ya kimataifa, “ tunafikiaria jinsi ambavyo ingekuwa muhimu kusikiliza sababu za wengine, na kutoa kipaumbele cha majadiliano na mchakato wa mazungumza ambayo ni njia pekee ya kufikia amani thabiti na ya kudumu badala ya kuchukua njia za ukatili, uchu na hila za haraka kwa manufao binafsi”, amesisitiza. Kusikiliza kwa maana hiyo , kunafanya katika kimya ambacho kinafungua moyo, husaidia kuondokana na hasira, chuki na kuweza kupata njia za amani. Wengi wanapenda ukimya unaosikika Fatima. Ni ukimya wa kusikiliza ambao unakufikisha katika imani, kupenda, na kulinda kila siku ni neema ya kuomba kwa Bikira Maria.
Kuelekea Siku ya Vijana (WYD )ya 2023
Hatimaye, alikumbuka Siku ya Vijana Duniani, ambayo itafanyika nchini Ureno mwaka 2023 kwa kuongozwa na kauli mbiu: Maria aliondoka na kwenda haraka (Lk 1:39) na kumalizia akisema “Kaka na dada, tuamke na twende, haraka ili kufikia maisha ya wale wanaotuzunguka: kwa ajili yao tunaota na kwa msaada wa Mungu, tunajenga Kanisa lenye uso kijana na mzuri, ambalo linang'aa linapokuwa la kimisionari, likaribisha, lililo huru, aminifu, maskini wa mali na tajiri wa upendo (rej. Mahubiri ya papa Francisko huko Fatima, 13 Mei 2017).
Kujikabidhiwa upya kwa Maria
Alhamisi tarehe 12 Mei 2022 usiku, Askofu Mkuu Peña Parra aliongoza maandamano ya kiutamaduni ‘aux flambeaux’ wakiwa na mishumaa mikubwa katika eneo la Madhabahu katika mazingira ya furaha baada ya miaka miwili ya kufungwa na usumbufu kutokana na janga la uviko-19. Pia katika tukio hilo alikariri kwamba kutoka kwa Fatima kuna sala isiyokoma kwa ajili ya zawadi ya amani katika Ukraine na katika dunia nzima: “Hija yetu hii pia ni ishara ya amana yetu ya kina na upya kwa Mariamu, Mwanamke wa Ufufuo na Mama wa Tumaini na, kupitia wewe, katika Bwana, ambaye hakuna lisilowezekana kwake!