Padre Merlo:Wazee wajue umuhimu wa kuzaa matunda
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, limeelezea umuhimu wa kipindi kiikuu na kile kinachowakilisha kwa siku zilizopita, za sasa na zijazo ambapo amesisistiza kwamba Sio bahati mbaya kwamba Ulaya inakabiliwa na vita, hasa wakati ambapo kizazi kilichokabiliana na vita awali kinatoweka. Katika uzee bado watazaa matunda" (Zab 92:15). Ni kaulimbiu ya Siku hii ya II ya Siku ya Wazee Duniani itakayoadhimishwa tarehe 24 Julai 2022 duniani kote. Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, aliwasilisha katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku hiy muhimu. Kardinali katika uwakilishi huo alitoa mwanga kwa baadhi ya mada muhimu zaidi zilizojitokeza katika Ujumbe wa Papa, zikiwemo upole, malezi na sala, zinazoelezwa kuwa nguzo tatu za hali wa utamaduni wa kutupa tunamoishi na ambao tunateseka. Ishara hizi ilikuwa ni msisitizo wa Baraza la Kipapa katika kuandaa Siku hi ina kuiishi Siku hiyo ya Dunia kwa kuadhimisha misa kwa ajili ya wazeee katika kila parokia na kutembelea wale walio peke yake.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Vittorio Scelzo, anayesimamia huduma za kichungaji kwa wazee Katika Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, ambaye pia aliwasilisha nembo ya Siku. Katika moyo wa alama hii ni kukumbatia, ishara ya mkutano na mazungumzo kati ya vizazi. Scelzo alieleza kuwa kumbatio ni kwamba kati ya vijana na wazee, wazee na wazee wengine, lakini juu ya yote, katika kipindi hiki, inawakilisha kukumbatia watu wengi amabo wamekufa kutokana na janga hilo. Giancarla Panizza na Maria Francis walichukua nafasi na kushuhudia kwamba mawazo yaliyomo katika Ujumbe ni njia ambazo kila jumuiya inaweza kuishi katika ukweli wake halisi. Giancarla Panizza, ni mratibu katika Shirika lisilo la kiserikali la Mfuko wa Aliante na amejitolea kuwakaribisha wakimbizi kutoka Ukraine kaskazini mwa Italia, huko Sartirana katika jimbo la Pavia. Hasa, alizungumza juu ya Airis, aliyezaliwa kabla ya wakati wake nchini Italia kutoka kwa mama yake ambaye alikimbia mabomu ya Urussi. Pia katika chumba hicho alikuwa Katerina, shangazi wa Iris mdogo, ambaye jina lake linamaanisha upinde wa mvua katika Kiukreni. Airis alitoka siku chache zilizopita kutoka kwa incubator ya Polyclinic ya mji mdogo wa Nordic ambao sasa ni raia kamili.
Hata hivyo, kutoka Bangalore, nchini India, Maria Francis, alisema alikuja kuwa mmishonari baada ya kujitolea kwa babu yake ambaye alipoteza mke wake, kwa miaka 60, katika ukuu wake. Mnamo Julai 2021, Maria Francis alihamasisha na kuandaa, katika maeneo mengi nchini India, ziara za vijana kwa ajili ya wazee pekee, wakati wa toleo la kwanza la Siku ya wazee. Pia katika Chumba cha Waandishi wa Habari Padre Alexandre Awi Mello, katibu wa Baraza la Walei, Familia na Maisha, ambaye akizungumza na Vatican News alieleza moja ya mambo muhimu ya ujumbe wa Papa, yaliyomo katika mada isemayo: kwamba “hata uzeeni wataendelea kuzaa matunda. Umuhimu ni kwamba, katika hatua hii ya maisha, ambayo mara nyingi haijatarajiwa na ambayo, kama Papa anavyosema, inakuja kama mshangao, wazee wanaweza kuelewa umuhimu wa kutoa matunda, na kwamba hawajatupwa, kwa kuwa wao ni watu wa kweli ambao wana ujumbe wa kutoa kwa ulimwengu, kwa familia na kwa jamii. Pia alikumbuka mawazo matatu yaliyotolewa katika ujumbe huo, yaliyorudiwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Kardinali Farrell juu ya umuhimu wa huruma, ulinzi na sala. Wao ndio nguzo za kiroho na za wazee ambao wanaweza kuzaa matunda kuanzia maisha yao ya sala, na kutoka katika utunzaji walionao sio tu kwa familia zao bali hata kwa wale watu walio katika jamii, haa wale walio wengi na wenye uhitaji".
Papa katika maandishi yake pia anazungumzia juu ya mioyo inayodhoofisha. Katibu huyo alieleza kuhusiana na suala hili kwamba katika mazingira tunayoishi, tukiwa bado tunajaribu kujinasua kutoka katika janga hili, tukijikuta na vita vya kipuuzi, Papa anatualika kuufanya moyo kuwa wa kijeshi, kuwa wazi kwa upendo, wazi kueleza huruma ambayo iko kwa kila mzee, kwa sababu wametunza maisha ya familia zao kwa miaka mingi, na sasa wanaweza pia kutufundisha umuhimu wa huruma hii”. Papa Francisko anasema jambo muhimu sana kuhusu hilo, kwa mujibu wa Padre Awi Mello kwamba alitukumbusha tena kuwa sio sio bahati mbaya kwamba Ulaya inakabiliwa na vita, hasa wakati ambapo kizazi ambacho kilikuwa tayari kimepata vita kinatoweka."Inaonekana tunasahau kwa urahisi sana fundisho ambalo maisha na historia yametupatia. Kizazi hiki lazima tukukumbushe, na kuwa kumbukumbu ya kile kilichotokea Ulaya katika karne iliyopita, na ambayo sasa tunaishi tena. Uzee, kama kila msimu, huzaa matunda. Kwa kumalizia, kilichobaki ni kusisitiza tena maana ya ukuu kama msimu, kwa maneno ya Papa Francisko: "Kila msimu una maana yake mwenyewe na hii pia ina maana nzuri: sio mwisho wa maisha bali ni wakati ambao bado ni wa kustawi na kuzaa matunda.