Tafuta

2022.05.12 Mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya uwakilishi wa Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani 2022 2022.05.12 Mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya uwakilishi wa Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani 2022  

Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi 2022:Ujenzi wa mustakabali wao pasipo ubaguzi!

Katika ujumbe wa Papa Francisko katika Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani 2022,umewakilishwa katika Ofisi za vyombo vya habari Vatican.Kardinali Montenegro,Askofu Mkuu Mstaafu wa Agrigento amebainisha kuwa:“Wahamiaji leo hii ni milioni 260.Ni bara la sita la sayari,haliwezi kupuuzwa.Hakuna muda wa kupoteza,mchango wa kila mtu unahitajika.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maadhimisho ya Siku ya 108 ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2022 yanaongozwa na kauli mbiu “Kujenga mustakabali na wahamiaji na wakimbizi” iyakayoadhimisha tarehe 25 Septemba 2022. Katika ujumbe huo Papa Francisko anakazia kusema kwamba kazi yao uwezo wao wa kujisadaka, ujana wao na shauku yao inatajirisha Jumuia nyingi ambazo zinawakaribisha. Ujumuushaji wa watu walio katika mazingira magumu ni hali msingi wa lazima kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Kwa maana hiyo Uwepo wa wahamiaji na wakimbizi bila shaka ni uwezo mkubwa unaopaswa kutambuliwa na kuthaminiwa. Hayo yamesisitizwa na Padre Fabio Baggio, Katibu msaidizi wa Kitengo cha Baraza la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Binadamu mwenye dhamana ya Sehemu ya Wahamiaji na Wakimbizi na kwa ajili ya mipango maalum, akiwasilisha  katika Ofisi ya Habari ya Vatican, kwa waandishi wa Habari, Ujumbe wa Baba Mtakatifu wa Siku ya wahamiaji na  wakimbizi, ambayo itaadhimishwa Dominika  tarehe 25 Septemba 2022.

Kujenga mustakabali: kutambua mchango wa wahamiaji na wakimbizi

Katika ulimwengu ulioangaziwa sana na janga na dharura za zamani na mpya za kibinadamu alisema Padre Baggio  Papa Francisko anathibitisha kwa nguvu dhamira ya pamoja ya kujenga mustakabali unaojibu zaidi na zaidi mpango wa Mungu, mustakabali wa amani na ustawi, ufalme wa Mungu”. Mustakabali utakaojengwa na wahamiaji na wakimbizi amesisitiza Baba Mtakatifu ni pamoja na wakazi wote wa pembezoni, waliotupwa na waliotengwa, ili mtu yeyote asitengwa. Ujumuishaji huu, kwa mujibu wa Padre Baggio ni hali halisi na msingi. Zaidi ya hayo, kujenga  pia inamaanisha kutambua na kuhamasisha mchango wa wahamiaji na wakimbizi kwa kazi hii ya ujenzi, kwa sababu ni kwa njia hiyo tu dunia inaweza kujengwa ambayo inahakikisha hali ya maendeleo ya binadamu ya wote.  Padre Baggio katika kuhitimisha uwakilishi wake, amesoma sala ya Papa Francisko ambayo inatoa mwangwi wa Sauti ya sala ya Mtakatifu Francis wa Assisi  kuhusu "kuwa vyombo vya amani, furaha, faraja, matumaini  na nuru penye giza".

Hakuna muda wa kupoteza mchango wa kila mmoja unahitajika

Naye Kardinali Francesco Montenegro, Askofu MkuuMstaafu wa Agrigento na mjumbe wa Baraza la Kipapa la Huduma za Maendeleo ya Binadamu, akifafanua hali halisi ya matukio haya ya uhamiaji na ukimbizi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari amesema: "Kila kitu kilichotokea Lampedusa kwa kuwasili mara kwa mara kwa wahamiaji kimetikisa sio tu jumuiya ya parokia na ya Agrigento lakini ni dunia nzima. Wahamiaji leo hii ni milioni 260. Hili ni bara la sita la sayari, haliwezi kupuuzwa. Hakuna muda wa kupoteza, mchango wa kila mtu unahitajika”. Haya ni maelezo ya 

Mwanzo wa Udugu unawezekana

Kardinali Montenegro aesema: “Nini cha kufanya mbele ya maelfu ya watu wanaofika kila siku na magari ya kubahatisha? Nini cha kufanya wakati kama mwaka wa 2013  mamia kadhaa yao walizama mita chache kutoka pwani na kupoteza maisha?" Kardinali Montenegro alijiuliza: “Unapokabiliwa na ukweli huu  alisema  unatambua kuwa mwanzo tu ya udugu inaweza kukusaidia. Ukiweza kumtazama mwanaume huyo, huyo mwanamke au mtoto huyo machoni, unaelewa kuwa ni sawa na wewe, kwamba ni ndugu yako. Papo hapo, tofauti zote, mizozo ya kisiasa, mantiki ya nambari au kanuni za hii au nchi hiyo huanguka.

Hadhi na utu wa mwanadamu kwanza bila kujali nchi au dini

Kardinali amesema “Macho hayo yanakuambia hadhi ya mtu huyo hapo awali na zaidi ya kuwa mtu wa nchi 'X' au dini 'Y'. Kujenga siku mstabali wa siku zijani kunahitaji mtazamo huu kwa upande mwingine, bila ubaguzi wowote na upendeleo wowote”.  Kadinali alikumbuka kuwa,  Papa, anasisitiza sana ukweli kwamba tazamio hili laweza kuthibitika kuwa fursa ya ukuzi kwa wote. Historia inatufundisha kwamba ambapo wakati ujao umejengwa katika mantiki jumuishi, mwishowe, kila mtu amepata, sio tu kwa heshima, bali pia kiuchumi na kiutamaduni”.

Hakuna wengine bali sisi pamoja

Kwa kusisitiza zaidi amebainisha kwamba “Hata kauli mbiu ya siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani inasema: “Kujenga mustakabali na wahamiaji na wakimbizi” ambayo kwa hakika inatualikakupita kutoka mantiki ya kukubalika kwa urahisi kwenda katika mantiki ya Uinjilishaji wa udugu wa ulimwengu ambamo yule mwingine na hasa maskini  ni ndugu na ambaye niko naye, na kuitwa kutembea naye”. Kwa maana hiyo ndipo “Hakuna wengine wanaokaribisha na wengine wanaokaribishwa bali ni ndugu wote ambao tunapaswa kupendana, kujifunza kufanya tofauti za kitamaduni, kidini au kijamii kuwa fursa nzuri kwa ukuaji kwa wote”, amesisitiza Kardinali Montenegro katika uwasilishaji wa Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 2022.

UWAKILISHI WA UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA WAKIMBIZI 2022
12 May 2022, 16:05