Tafuta

Maadhimisho ya Siku Kuu ya Vesak kwa Wabudha ulimwenguni Maadhimisho ya Siku Kuu ya Vesak kwa Wabudha ulimwenguni 

Ujumbe wa Sikukuu ya Vesak: Wabudha na Wakristo pamoja kwa ustahimilivu

Katika kuadhimisha Siku Kuu ya Wabudha 2022 iitwayo Vesak kwa waamini wa Kibudha inayokumbusha kuzaliwa,kifo na kuangazwa kwa Budha,Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini wametuma ujumbe wao.Inawezekana kusaidia ubinadamu kugeuka wastahimilivu wa kupeleka mwanga katika tunu zilizofichika za tamaduni zote za kiroho.Kwa Wabudha,Njia tukufu inaweza kuendelezwa huruma na hekima kwa jitihada za masuala ya kijamii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Siku kuu ya Vesak kwa mwaka 2022 ambayo ni kumbu kumbu ya kuzaliwa, Siku ya Mwanga na kifo cha  Gautama Budha, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya  kidini wameandika ujumbe wao kwa jumuiya nzima ya Wabudha ulimwenguni ili kutoa salamu ya dhati katika fursa hiyo. Katika Ujumbe huo unabainisha jinsi wameandika ujumbe huu wakati ubinadamu unakabiliana na migogoro mingi. Kwa mwaka wa tatu mfululizo, watu wote ulimwenguni bado wamezuiwa na mgogoro unaondelea wa kiafya kutokana na UVIKO-19. Majanga ya asili yanayoendelea ambayo yanahusiana na ikolojia, yameakisi udhaifu wa wazalendo katika dunia shirikishi. Migogoro ambayo inazidi kumwaga damu ya wasio na hatia na kusababisha mateso mengi yaliyotawanyika. Kwa bahati mbaya bado kuna kutumia jina la dini ili kuhalalisha vurugu. Kama alivyobainisha Papa Francisko kwa huzuni kubwa kuwa: “ubinadamu unajivunia na maendeleo yake katika sayansi na katika wazo, katika mambo mengi mazuri,  lakini kwa kurudi nyuma katika suala la kuleta amani…. Hii inatufanya tujionee aibu kwa wote (Hotuba kwa washiriki wa Mkutano wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki 18 Feb 2022).

Viongozi wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini wamebainisha jinsi wanavyoona kuibuka kwa ishara za mshikamano katika kujibu mabalaa yaliyosababishwa na migogoro hii na shughuli ya kutafuta suluhisho ndio inabaki kuwa  msingi. Tamaa ya kutafuta utajiri wa zana na kuacha thamani kubwa za kiroho zimepelekea kushuka kwa maadili ya kizazi katika jamii. Kama ilivyo kwa Wabudha na Wakristo, maana ya uwajibikaji wa kidini na kimaadili unapaswa hutoe chachu kubwa ya kusaidia ubinadamu katika harakati zake za kupata upatanisho na ustahimilivu. Watu wadini zote kwa kuongozwa na misingi thabiti yao, wanapaswa kuongeza nguvu ya kuwa taa za matumani ambazo hata kama ni ndogo zinaweza tena kuangaza mchakato wa safari ambayo inapelekea ubinadamu kushinda utupu wa kiroho ambao unasababisha mabaya mengi na mateso mengi.

Hata kama katika mitindo tofauti, Budha na Yesu Kristo wanaelekeza wanafunzi wao thamani kubwa.  Ukweli mtukufu wa Budha unaeleza asili na sababu ya mateso na kuelekeza mara nane njia inayoongoza kwenye kukomesha mateso. “Ni kufifia na kukoma kwa tamaa hiyo hiyo bila kubaki kitu; kuachilia, na kutokushikamana nayo” (Dhammacakkappavattanasutta, 56.11). Fundisho hilo likifanyiwa zoezi ni tunu msingi kwa ajili ya kutoshikamana na  tamaa na mchezo wa madaraka. Injili haishauri kamwe vurugu kama jibu. Heri za mlimani zilizotangazwa na Yesu zinaonekana jinsi ustahimilivu ulivyo muafaka kwa ajili ya thamani za kiroho katikati ya dunia iliyomegeka vipande vipande. “Heri maskini, heri, wapole, heri wenye mgororo, heri wahudumu na wapatanishi wa amani (Mt 5,1-12).  Hawa wamebarikiwa licha ya matatizo ya sasa, ambao wanajikabidhi juu ya ahadi ya kimungu ya furaha na wokovu.

Viongozi hao wa Majadiliano ya Kidini wamebainisha jinsi ambavyo inawezekana kusaidia ubinadamu kugeuka wastahimilivu wa kupeleka mwanga katika tunu zilizofichika za tamaduni zote za kiroho. Kwa Wabudha, Njia tukufu inaweza kuendeleza huruma na hekima kwa jitihada za masuala ya kijamii. Na kwa wakristo moja ya tunu hiyo ni tumaini. Kama asemavyo Papa Francisko: “Tumaini linaweza kutufanya kujua kuwa kuna njia moja daima ya kuondokana na ambayo  kweli tunaweza daima kuilekeza katika hatua zetu, na tunaweza daima kufanya lolote kwa ajili ya kutatua matatizo yetu ( rej. Laudato Si’, 61).

Viongozi wa majadiliano ya Kidini wanaamini kwamba tumaini linatuokoa tusikate tamaa. Na katika pendekezo hilo, wametaka kushirikishana hekima ya Mtumishi wa Mungu Thich Nhat Hanh  kuhusu “umuhimu wa tumaini ambalo linaweza kufanya wakati wa sasa usiwe mgumu kustahimili. Ikiwa tunaamini kwamba kesho itakuwa bora zaidi, tunaweza kuvumilia ugumu huo leo hii” (Peace is Every Step, 1991, 41-42). Kwa maana hiyo viongozi hawa  wameomba kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kesho iliyo bora! Kwa kuhitimisha ujumbe wao, Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, MCCJ, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya  Kidini na Katibu wake Monsinyo  Kodithuwakku K. Indunil J,  wamewatakia sikukuu yao ya Vesak idumishe uhai wa tumaini na kuzaa matendo bora ya ukarimu na kukabiliana na shida zinazosababishwa na migogoro ya sasa.

UJUMBE WA BARAZA LA KIPAPA LA MAJADILIANO YA KIDINI KWA FURSA YA SIKU KUU YA VESAK
01 May 2022, 14:43