Tafuta

2019.08.10 Jengo la  Niccolò V, Makao ya  Ior 2019.08.10 Jengo la Niccolò V, Makao ya Ior 

IOR inafunga taarifa za kifedha ya 2021 kwa faida halisi ya Euro milioni 18.1

Kwa mwaka wa kumi mfululizo,Taasisi ya Shughuli za Kidini imechapisha Ripoti yake ya Mwaka

Vatican News

Kwa mwaka wa kumi mfululizo, Taasisi ya Shughuli za Kidini  (IOR) imechapisha Ripoti yake ya Mwaka iliyo na taarifa za fedha kwa mwaka  2021 iliyoundwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya uhasibu vya IAS-IFRS. Taarifa hizi za fedha zilipata ripoti "isiyo na sifa" kutoka katika kampuni ya ukaguzi ya Mazars Italia S.p.A. na 26 Aprili 2022, iliidhinishwa kwa kauli moja na Bodi ya Usimamizi wa Taasisi na, kwa mujibu wa Mkataba, kutumwa kwa Tume ya Makardinali.

Tume ya Makadinali, baada ya kukiri usahihi wa data ya kifedha ya taarifa za fedha za 2021 na bila kuathiri mahitaji ya mtaji ya Taasisi, ilitatua kwa azimio lake juu ya maendeleo ya faida. Katika mwaka wa 2021, Taasisi ilipata matokeo yafuatayo kulingana na mpango mkakati:

• Euro milioni 18.1 ya faida halisi

• + 15% ya kiasi cha riba, + 22% ya kamisheni halisi, + 4% ya mali inayosimamiwa

• Uwiano wa TIER 1 wa 38.54%

• 59% uwiano wa gharama / mapato

Mapato yanalingana na matarajio, na mtindo mpya wa biashara wa HTCS (Held To Collect and Sell, yaani inashughulikiwa Kukusanya na Kuuza) iliyopitishwa kwa uwekezaji na kwa wasifu wa umakini wa hatari. Ukuaji wa mali zilizo chini ya usimamizi unaonesha matokeo mazuri ya usimamizi wa mali kwa wateja, unaopatikana kwa kufanya kazi kulingana na kutumia kanuni za Mafundisho Jamii ya Kanisa, na asilimia 70% ya mwelekeo wa usimamizi juu ya kiwango cha miaka 5.

Uwiano wa gharama/mapato unaonesha udhibiti wa gharama unaokubalika mbele ya chaguo la Taasisi la kuendelea kuweka huduma za wateja kidijitali, kuimarisha zana za ulinzi wa TEHAMA na kuajiri rasilimali mpya zenye wasifu tofauti wa ukuu na taaluma. Taasisi iliendelea kudumisha dhamira ya kufuata sheria na kanuni zote zinazotumika kama kipaumbele, kuthibitisha mabadiliko yake ya kitamaduni. Uwakilishi bora zaidi wa utamaduni huu dhabiti wa kufuata na kudhibiti hatari umetolewa katika ripoti ya Moneyval kuhusu Vatican 2021.

08 June 2022, 16:47