AdobeStock_132978739.jpeg Tahariri

Kwa ajili ya maisha, daima

Ni matarajio kwamba uamuzi wa Mahakama kuu ya Marekani itakuwa fursa ya kutunga sheria zinazolinda maisha,haki za wanawake na uzazi.

Na Andrea Tornielli.

Uamuzi wa Mahakama kuu ambayo baada ya nusu karne inafuta uhalalishaji wa Shirikisho la utoaji mimba nchini Marekani, kwa kurudisha suala hilo katika  majimbo binafsi kitivo cha kutunga sheria, inaweza kuwa fursa ya kutafakari maisha, juu ya ulinzi wa wasio na ulinzi na kutupwa, juu ya haki za wanawake, juu ya ulinzi wa uzazi.

Ni mada ambayo tangu mwanzo wa Upapa wake, Baba Mtakatifu Francisko ameieleza kwa bidii yote na bila mashaka yoyote. Katika Waraka wa  “Evangelii gaudium”, Hati inayoelekeza ramani ya barabara ya Askofu wa sasa wa Roma, inasomeka: “Miongoni mwa watu hawa dhaifu, ambao Kanisa linataka kuwatunza kwa upendeleo, pia kuna watoto ambao hawajazaliwa, ambao ni wengi zaidi, wasio na ulinzi na wasio na hatia kwa wote, ambao leo hii wanataka kukataliwa hadhi ya  binadamu ili waweze kufanya wanachotaka, kuwaondoa maisha yao na kuendeleza sheria kwa namna ya kwamba  hakuna mtu anayeweza kuzuia. Mara kwa mara, kwa kudhihaki kwa Kanisa ambalo linakuwa na utetezi wa maisha ya watoto ambao hawajazaliwa, msimamo wake unawasilishwa kama kitu cha kiitikadi, kifikra na kihifadhi. Hata hivyo utetezi huu wa maisha ambayo bado hajazaliwa unahusishwa kwa karibu na utetezi wa haki yoyote ya binadamu. Ni uthibitisho wa imani kwamba mwanadamu daima ni mtakatifu na hawezi kukiukwa utakatifu huo katika hali yoyote na katika hatua yoyote ya maendeleo yake. Na mwisho wenyewe na kamwe sio njia ya kutatua shida nyingine”

Tafakari ya dhati na ya pamoja juu ya maisha na ulinzi wa uzazi ingehitaji kuondokana na mantiki ya itikadi tofauti na kutokana na mgawanyiko wa kisiasa ambao mara nyingi, na kwa bahati mbaya, unasindikiza mjadala juu ya suala hili, kwa kuzuia mazungumzo ya kweli. Kuwa upande wa maisha, daima, inamaanisha kuwa na wasiwasi, kwa mfano, ikiwa viwango vya vifo vya wanawake kutokana na uzazi: nchini Marekani, kulingana na takwimu katika ripoti ya Shirika la shirikisho la “Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa”,  ilitoka vifo vya wanawake  20.1 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2019 hadi kufikia vifo 23.8 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2020. Na inashangaza kwamba mwaka 2020 kiwango cha vifo vya uzazi wa wanawake weusi vilikuwa vifo 55.3 kwa 100,000 waliozaliwa wakiwa hai, mara 2.9 kwa wanawake weupe.

Kuwa upande wa maisha, daima, kunamaanisha kujiuliza ni jinsi gani ya kuwasaidia wanawake kukumbatia maisha mapya, kwani kulingana na takwimu nchini Marekani, takriban asilimia 75 ya wanawake wanaotoa mimba wanaishi katika hali ya umaskini au wana mishahara midogo. Na ni asilimia 16 tu ya wafanyakazi wa sekta za kibinafsi wanaopata likizo ya kulipwa ya uzazi, kulingana na utafiti uliochapishwa katika Uchunguzi wa Harvard wa Psychiatry, yaani wa Chuo kikuu cha Harvard kuhusu masuala ya akili, mnamo tarehe 9  Machi 2020. Karibu mama mmoja kati ya wanne waliojifungua ambao hawana haki ya likizo ya kulipwa wanalazimika kuingia kazini ndani ya siku kumi baada ya kujifungua. Kuwa upande wa maisha, kila wakati, pia inamaanisha kuyalinda kutokana na tishio la bunduki, ambalo kwa bahati mbaya limekuwa sababu kuu ya vifo vya watoto na vijana Nchini Marekani (USA).

Kwa maana hiyo inategemewa kwamba mjadala kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani hautapunguzwa na kuwa na tofauti ya kiitikadi, bali utatoa mwanya wa kuhoji mbali na ng'ambo na pia upande huu wa bahari juu ya  nini maana ya kukaribisha maisha, kuyatetea na kuhamasisha katika sheria zinazotosheleza.

25 June 2022, 15:41