Malta:Nafasi ya tatu ya ushindi kihistoria kwa Mataifa madogo ya Ulaya!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mara ya kwanza ya kihistoria, kwa Wanariadha Vatican, kupata nafasi ya tatu ya ushindi. Ni wa kwanza Kimataifa kwa kutumia muda w 17'09"77 , kwa Sara, mwenye umri wa 27, mtoto wa Giancarlo Carnicelli, mfanyakazi wa Vatican ambaye alitanguliwa na Lilia Fisikovoci, aliyewakilisha nchi ya Moldavia kwa dakika (16'42"11), na mwingine wa Iceland, Iris Anna Skuladottir kwa (17"09"10).
Katika nafasi ya tatu ya Sara Carnicelli ilifanya kuwa na maana ya uwepo wa mchezo wa kimataifa wa Riadha ya Vatican ambapo kwa kufuata maelekezo ya Papa Francisko, inazindua fursa ya Udugu kwa ajili ya ujenzi wa uhusiano wa amani kati ya Watu.
Kwa misingi ya makubaliano ya Riadha Vatican, Chama cha Riadha cha Ulaya na Chama cha Mataifa Madogo ya Ulaya (kwa sasa wako mbioni kufikia hatua ya mwisho ya kutambuliwa kuwa katika Riadha Kimataifa( World Athletic). Hata hivyo Sara Carnicelli hakupanda kwenye jukwaa kupokea zawadi badala yake aliacha zawadi na nafasi hiyo kwa ajili ya Roberta Schembri (17'23"66) wa nchi ya Malta,
Kwa maana ya makubaliano na mtindo mpya na wa dhati wa utamaduni wa michezo kindugu wa Riadha ya Vatican, ambao umepata kukubaliwa na Papa Francisko tangu mwaka mmoja uliopita katika fursa ya toleo la Mshindi wa Mataifa Madogo ya Ulaya huko San Marino.