2022.06.24 Wenzi wa Ndoa kutoka Cameroon walioshiriki Mkutano wa X wa Familia duniani. 2022.06.24 Wenzi wa Ndoa kutoka Cameroon walioshiriki Mkutano wa X wa Familia duniani.  

Mkutano wa X wa Familia Duniani:Familia ni chombo muhimu cha uinjilishaji

Wanandoa kutoka nchini Cameroon,walikuwa kwenye Mkutano wa X wa Familia Duniani,Roma.Hawa waliwakilisha familia na Waratibu wa Utume wa Maisha ya Familia kwa Jimbo.Wakihojiwa na Vatican News walitoa ushuhuda wao wa kwanza wa sinodi.Kanisa sio suala la askofu au kasisi tu.Mchakato wa sinodi utasaidia watu wengi kushiriki katika maisha ya Kanisa na kuelewa kuwa Kanisa ni la kila mtu,pamoja na walei.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Nereus na Marcelline Nganfor ni wenzi wa ndoa wenye watoto kutoka jiji la kaskazini-magharibi mwa  Bamenda nchini Cameroon. Imani yao katoliki ni kitovu cha maisha ya familia na jumuiya, na wajibu wao kama waratibu wa Utume wa Maisha ya Familia katika Jimbo kuu la Bamenda umewaleta mjini Roma kushiriki katika Mkutano wa Kumi wa Familia  duniani kuanzia tarehe 22 -26 Juni 2022 wakiwa  pamoja na Askofu Mkuu Andrew Fuanya Nkea wa jimbo kuu hilo.  Wakizungumza na Radio Vatican, Nereus na Marcelline walieleza furaha yao kwa kuwa na fursa ya kuhudhuria  Mkutano huo Roma kwa sababu, Nereus alisema, “mazungumzo yanaboresha na yanafaa na tunafikiri mkutano huo utatusaidia kuimarisha shughuli tuliyo nayo ambayo inafanyika katika jimbo kuu letu”.

Askouf Mkuu wa Jimbo Kuu la Bambenda nchini Cameroon ameshiriki Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.
Askouf Mkuu wa Jimbo Kuu la Bambenda nchini Cameroon ameshiriki Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.

Kila siku ya Mkutano huo,  walituma muhtasari nyumbani kwao ambao ulikuwa ukipokelewa katika miundo ambayo imewekwa katika Jimbo Kuu kwa kila ngazi ya mpango wake wa kichungaji kwa familia, kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinamfikia kila mtu. “Kiukweli imekuwa tukio la ajabu na tunafikiri itachukua hatua ndefu ili kuimarisha kile tunachofanya katika majimbo yetu” walithibitisha Nereus na Marcelline wakiangazia  na uzoefu wa kusisimua wa mchakato wa Sinodi nchini Cameroon ambapo wanashiriki kwa kina.

Marcelline alieleza kwamba tangu Baba Mtakatifu Francisko alipoanzisha  mchakato wa Sinodi ya miaka miwili kuelekea Sinodi ya Maaskofu kuhusu Sinodi ya mwaka 2023, katika Jimbo la Bamenda wamepitia shughuli nyingi kuanzia mikutano hadi taarifa zinazolenga jinsi ya kweli kuishi maisha ya sinodi.” Nereus alionesha maoni yake kwamba Mkutano huo Familia duniani  unazingatia sana muktadha kwa maana hiyo wakitazama ushauri w Papa Francisko  wa Amoris Laetitia, kuna kipengele hicho cha wito na utume wa familia. Ikiwa kipengele hicho kitatekelezwa vyema katika ngazi ya familia, alisema, itasaidia sana kuongeza ushiriki wa familia katika mchakato wa sinodi.

Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.
Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.

Jambo moja ambalo tafakari ya sinodi imeleta, wenzi hawa walisema, ni kwamba Kanisa sio tu suala la askofu au kasisi. Na kwa maana hiyo wanaamini kwamba mchakato huu wa sinodi utasaidia watu wengi kushiriki katika maisha ya Kanisa na kuelewa kwamba Kanisa ni la kila mtu, ikiwa ni pamoja na walei. Marcelline alionesha kwamba familia yao wenyewe tayari inaishi sinodi kwa sababu washiriki wake wote wanajua kwamba kukusanyika pamoja kama familia ni muhimu sana katika maisha yao  ya kiroho na kwa mikutano yao ya Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristo, na kwamba kila shughuli nyingine kama familia ni muhimu sana, na hivyo wanaamini  kwamba ikiwa familia zitafanya hivyo, sinodi itakuwa suala la vitendo.

Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.
Mkutano wa X wa Familia duniani Vatican.

Kwa upande wa Nereus  hata hivyp alionya dhidi ya kudharau umuhimu wa mapadre na watawa katika maisha ya familia, juu ya haja ya kutafuta msaada pale inapobidi na kupata muda wa kujumuika nao katika nyanja zote za maisha. Alipoulizwa ni changamoto zipi kuu anazokabiliana nazo katika huduma yake. Nereus alisema, kuhusu ndoa, katika Sura ya 2 ya Waraka wa Amoris Laetitia, inaangazia changamoto nyingi zinazokabili familia leo: “Na hizo ndizo changamoto tunazokabiliana nazo. Ndiyo maana hati hiyo ni halali sana na inatuhusu sana. Tunajua kuwa 'ndoa na familia' vinashambuliwa kutoka pande zote, hadi ufafanuzi wao.”

Akitafakari juu ya migogoro ya kijamii na kisiasa ambayo Jimbo kuu la Bamenda linakumbana nalo kwa sababu ya ugomvi katika eneo la lugha ya Cameroon Nereus alisema: “unaposikia tunapitia shida, ni familia inapitia shida hiyo, ambayo inamaanisha kuwa kuna shida,  na kazi nyingi ya kufanywa katika eneo hilo ili kusaidia familia, kuziongoza, kuzishauri, na labda kutafuta njia za kutosheleza baadhi ya mahitaji yao na  kwa kusaidia mahitaji ya kimwili.

Ziara ya Kardinali Parolin Katibu wa Vatican katika Jimbo Kuu Bamenda nchini Cameroon
Ziara ya Kardinali Parolin Katibu wa Vatican katika Jimbo Kuu Bamenda nchini Cameroon

Wakitazamia kurejea kwao Cameroon baada ya Mkutano wa  X wa Familia Duniani Familia ya Nganfor wanakubali kwenda nyumbani wakiwa wametajirishwa, na kutokana na malezi na taarifa walizopokea jijini  Roma, watakuwa wamejitayarisha vyema zaidi kama watu binafsi, kama wanandoa na kama waratibu wa Utume wa Maisha ya Familia, katika Jimbo kuu la Bamenda. Kwa kuhitimisha, Nereus na Marcelline walionesha imani yao thabiti kwamba familia na kwamba ni kitengo chenye nguvu cha kueneza injili ambacho kinajibu hitaji la dharura  ya Kanisa. “Ni kama hazina inayochimbwa,  na chombo muhimu sana cha kueneza Injili  na kuwaleta pamoja  watu wa Mungu kwenye Ufalme wake”.

WENZI WA NDOA KUTOKA JIMBO KUU BAMENDA NCHINI CAMEROON KATIKA MKUTANO WA FAMILIA
26 June 2022, 13:38