Baba Mtakatifu amemteua Padre  Matthew Yitiereh kuwa Askofu wa Jimbo la Yendi nchini Ghana. Baba Mtakatifu amemteua Padre Matthew Yitiereh kuwa Askofu wa Jimbo la Yendi nchini Ghana. 

Padre Matthew Yitiereh ni Askofu mteule wa Jimbo la Yendi,Ghana

Padre Matthew Yitiereh alizaliwa mnamo tarehe Mosi Januari 1961 katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi,Jimbo Katoliki la Wa.Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 22 Julai 1995 kwa ajili ya Jimbo Kuu katoliki la Tamale.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi ya kung’atuka katika shughuli za kichungaji kwa  Jimbo katoliki  la Yendi, nchini (Ghana), lililowakilishwa na Askofu Vincent Sowah Boi-Nai, S.V.D. na wakati huo huo, Baba Mtakatifu akamteu Askofu wa jimbo hilo hilo, Mweshimiwa  Padre  Matthew Yitiereh, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Vika wa Jimbo Kuu katoliki la Tamale.

Padre Matthew Yitiereh alizaliwa mnamo tarehe Mosi Januari 1961 katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi, Jimbo Katoliki la Wa.  Majiundo yake ya Ukasisi,  ni kuanzia Seminari Ndogo ya Mtakatifu Francis Xavier huko Wa, hadi Seminari Kuu ya  Kumasi na  Seminari Kuu ya Tamale. Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 22 Julai 1995 kwa ajili ya Jimbo Kuu katoliki la Tamale.

Baada ya kuwekwa wakfu wa kikuhani alishika nyadhifa zifuatazo: Kama  Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu huko Chamba (1995-1997) na wa  Watakatifu Petro na Paulo (1998-2003); Mkurugenzi wa Idara ya Vijana wa Jimbo (1998-2003); Mwalimu wa Taalimungu aliyebobea katika Liturujia ya Kichungaji, nchini Ireland (2002-2004); Mshereheshaji wa Jimbo Kuu na Rais wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Tamale ya Mafunzo ya Kiutamaduni (2004); Msimamizi wa Kanisa Kuu la Kupashwa Habari huko Tamale (2004-2015); tangu 2015 ,Rais wa Jumuiya ya Mapadre wa Jimbo Kuu la Tamale na tangu 2016 hadi sasa Padre Matthiew alikuwa ni Vika wa  Jimbo Kuu la Tamale na Paroko wa Kanisa la Sakramenti Takatifu.

03 June 2022, 16:46