2022.06.07 Uwasilishaji wa Stabat mater katika gereza. 2022.06.07 Uwasilishaji wa Stabat mater katika gereza. 

“Stabat Mater” ya wafungwa jijini Vatican

Filamu fupi iliyozungushwa na 'Electra Teatro' katika gereza la Pistoia iliwasilishwa katika Maktaba ya Filamu Vatican.Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk.Ruffini amebainisha kwamba Baraza hilo limekuwa makini kila mara hadi mwisho,kwa kutaka kufafanua kuhusu mizunguko mizuri ya kizuizini.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Kuna uchungu wa Mama, kukata tamaa mbele ya Mtoto aliyekufa, kukata tamaa hadi kufikia kukataa baraka ya kutoona neema pamoja na kuona akiteseka, ili asilazimike kumzika. Na baadaye kuna uwezekano, daima, wa fursa ya pili na labda hata ya tatu au ya nne, kwa sababu kamwe haijaisha hadi imekwisha kabisa. Yote haya yapo katika dakika 33 zenye nguvu, zenye kugusa na zenye uwezo zinazozungumza katika tumbo na moyo, ambapo wimbo wa “Stabat mater” wa 'Electra Teatro 'umetungwa, uliozungushwa  na Giuseppe Tesi na kufasiriwa kwa ustadi na waigizaji wawili wa kitaalamu, Melania Giglio na Giuseppe Sartori na kwaya ya kipekee ambayo imeundwa na wafungwa wapatao kumi kutoka gereza la Pistoia, nchini Italia.

Stabat Mater katika Gereza
Stabat Mater katika Gereza

Uchungu wa kifo, hata hivyo, kwa imani inatufundisha, daima kwamba inafuatwa na tumaini na mwanga wa Ufufuko. Kwa maana hiyo: “Kuwasiliana kwa matumaini kunamaanisha kuona mambo kwa kina,  kwenda zaidi, kwani zaidi ya maumivu yote kuna uwezekano wa ukombozi. Mara nyingi sanaa, kama ilivyo katika kesi hii, husaidia imani kuona kile ambacho hatuoni kwa macho yetu. Kama Papa Francisko anavyo sema: inatufanya tuone kwa macho ya moyo”. Kwa hiyo, hii ndiyo maana ya kweli na ya kina zaidi ya kufanya uchungaji wa gerezani, kwa kutambua umungu  ulio ndani ya kila mtu, ndani ya kila mmoja wetu na kuuleta juu ya uso” Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano  Dk. Paulo Ruffini wakati wa uwasilishaji wa Filamu hiyo.

Stabat Mater katika Gereza
Stabat Mater katika Gereza

Kazi hiyo ni matokeo ya maabara ya maonesho iliyoanzishwa katika muundo wa 2018, na baadaye kuingiliwa na kufungwa kutkana na janga na baadaye kukamilishwa kwa uchungu katika nyakati ngumu za janga la UVIKO  ambalo gereza lilikuwa mbali zaidi, mahali pa pekee zaidi.  Hata hivyo kutokana na ugumu uliokuwapo kwamba gereza la , Pistoia halikuwa muafaka wa kwenda  wageni, hivyo kurudi huli kulikuwa kwa juu kila wakati kwa mujibu wa mkurugenzi wa mtunzi wa filamu hiyo,  ambaye sio kwa bahati alichagua mtindo wa filamu fupi pia kuelezea uzoefu wa wafungwa ambao wanahusishwa kikamilifu na ile ya hisotria ya Mama, katika ushiriki wa uchungu: “Katika jela halikuwezi kuwa na uvivu tu, nilihisi kama ukosefu wa maendeleo, alisema, mfungwa mmoja katika filamu. Lakini pia kuna uchungu  ambao huwa tumaini kwa sababu “Niliamua kuanza tena kutoka hapa, kutoka gerezani, na nikaanza njia ya shule, kwa mujibu wa mfungwa mwingine.  Na hatimaye: “Gereza kimsingi ni kifungu cha ufahamu, maisha yamenifundisha kuwa kuna ukweli mbaya zaidi”, alisema mfungwa mwingine.

08 June 2022, 16:40