Tuzo ya Nchi ya Hungaria kwa Kardinali Parolin,Katibu Vatican
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tuzo ya Serikali ya Hungaria imekabidhiwa mnamo tarehe 8 Juni 2022, jijini Roma katika Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa ya Hungaria kati ya wengine, waliotuzwa ni pamoja na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano ya Nchi na Mashirika ya Kimataifa. Aliyekabidhi tuzo hizi ni Zsolt Semjén, Makamu waziri Mkuu wa Hungaria.
Katika afla hiyo aliudhuria pia Kardinali Péter Erdő, Mkuu wa Kanisa la Hungaria, Bwana Eduard Habsburg-Lothringen, Balozi wa Hungaria anayewakilisha nchi yake Vatican na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa ya Hungaria.
Tuzo hiyo ni Msalaba wa Heshima kutoka Shirika la Hungaria uliotolewa na Bwana Daniel Pacho, mhusika wa Mawasiliano kwa ajili ya masuala ya Hungaria katika Kitengo cha Mahusiano kwa Makatibu wawili wa Vatican hasa kwa kutambua kazi zao za kuhamasisha uhusiano kati ya Hungaria na Vatican na kuwezesha ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko katika kufunga Misa ya Kongamano la 52 Kimataifa la Ekaristi huko Budapest.