Familia ya Paloni ya watoto 12:Vijana wanahitaji ushuhuda wa familia!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwenye jukwaa la Ukumbi wa Paul VI, Vatican Ijumaa tarehe 24 Juni 2022 walitoa ushuhuda kuhusu mada ya “namna gani ya kurithisha imani kwa vijana leo hii”, ambao walikuwa ni wenzi wa ndoa Massimo na Patrizia Paloni, wazazi wenye watoto 12, ambao walipendekeza kwamba ni "kugundua tena, kupitia kuanzishwa kwa ukristo, na kusimika mizizi katika Injili, kama ilivyokuwa kwa Wakristo wa kwanza katikati ya ulimwengu wa kipagani ”. Wenzi hawa wakiwa wenye asili ya Roma, walikumbatia Njia ya Waneokatekumenali kama wazazi wao, na wamekuwa wamisionari wasafirio huko Uholanzi kwa miaka 18 sasa. Wakiwa wamefuatana katika Mkutano wa X wa Familia Ulimwengu, na watoto wao, wakiume 6 na wa kike 6, ambao wanawafundisha kila siku kuhusiana na Neno la Mungu ili liweze kuangaza maisha yao. Lakini wao walisema ni watoto kama wengine wote, ambao wanafafanuliwa na matatizo yao yanayohusiana na umri wanaopitia. Wakati fulani pia kuna kutoelewana au matatizo katika mazungumzo, lakini nuru ya Injili au mapendekezo na msaada wa familia nyingine huwafungua mafundo na makabiliano yanakuwa ya amani na utulivu tena.
"Tulielekezwa kuwa katikati ya familia kuna altare tatu" walisimulia familia zilizokuwa zinawasikiliza na kwamba altare ya kwanza ni meza ya Ekaristi Takatifu, ambayo Yesu Kristo anatoa dhabihu ya maisha yake na ufufuko wake, na wokovu wetu. Altare ya pili ni kitanda cha ndoa, ambapo Sakramenti ya Ndoa inatimizwa kwa kutoleana na muujiza wa upendo na maisha mapya na hatimaye altare ya tatu ni meza, ambapo familia nzima inakusanyika ili kula chakula, wakimshukuru Bwana kwa zawadi zake. Kwa maana hiyo, kila mlo unakuwa mkutano ambao mada na shida zinazopatikana katika maisha au shuleni hujadiliwa na ambapo kila mtu anashiriki na ushirikiano na umoja unaishi.
Divai mpya ya Yesu katika maisha ya vijana sana, waliokuwa na umri wa miaka 24, 20 kwamba hawakukosa shida. Wao walichagua kufanya familia ya Kikristo yenye nia nzuri zaidi, lakini katika miaka ya kwanza ya ndoa, walipogundua tofauti zao na kasoro zao, walijihatarisha kujitenga kabisa. Baadaye shukrani kwa jumuiya ya Waneokatekumenali ambayo walikuwa wamejiunga, walianza kuzungumza wao kwa wao kwa uaminifu, kuangalia ndani na kutambua makosa yao na nini kilisimamisha njia ya safari yao ya ndoa,na ilikuwa kwao mwanzo mpya, kama katika harusi ya Kana. Kwa mujibu wa shuhuda yao wamebainisha kwamba baada ya kuishiwa na 'divai' ya kupendana na kupenda kulingana na juhudi zazo katika Yesu Kristo aliwapatia divai ya bure mpya na ya kulewesha ya msamaha. Aidha walibainisha jinsi ambavyo waligundua kwamba uwazi wa maisha si sheria yenye kulemea bali ni ukombozi dhidi ya ubinafsi, ambao bila hiyo ndoa inayumba. Kwa mshangao mkubwa, Mungu aliwapatia kutamani kila mtoto ambaye walijaliwa.
Vijana wanahitaji ushuhuda wa upendo wa familia: Kwa uzoefu wao Piloni ambao pia umeripotiwa katika Sinodi ya familia ya 2015wameweza kuthibitisha kwamba hupelekea imani kwa vijana wa ulimwengu wa kisasa ambao ni kazi ya umuhimu mkubwa ambayo inangojea Kanisa lote na kila mbatizwa leo hii. Hasa katika uso wa kupoteza hisia ya Mungu na yote ambayo hutolewa kwa vizazi vipya kwa mfano wa picha mbaya sana za mtandaoni, madawa ya kulevya, kuchanganyikiwa kwa utambulisho. Na kuna wale watoto wanaoishi katika familia za mzazi mmoja kwa sababu wazazi wao wametengana au kwa sababu walizaliwa nje ya ndoa. Kwa maana hiyo msaada na usaidizi wa shule, vijana wengi hujikuta hawana uhakika wowote na kupotea, wamefafanua wanandoa wa Paloni ambao, hata hivyo, wanarejea vikundi vidogo vya vijana ambao hukusanyika pamoja na familia za imani iliyothibitishwa na ya watu wazima, ambao wanatoa ushuhuda wa huduma. “Vijana huvutiwa na familia ya Kikristo ambamo wanaona imani iliyo hai. Katika vikundi hivi, vijana huanza kusoma Neno la Mungu, kutafakari amri kama njia ya maisha, kugundua tena Sakramenti ya Upatanisho na kuwasiliana na maisha ya Kikristo ya familia thabiti.
Lakini kwa upande wa Familia ya Paloni hakuna njia au mbinu ya kufuata katika mukhtasari huo. “Hakuna mtu awezaye kutoa kile ambacho hakukipokea hapo awali... Katika uchungaji wa vijana, ushuhuda wa familia ambazo, baada ya kupokea upendo wa bure wa Kristo na Kanisa, huwakaribisha vijana wa mbali katika upendo huu ni wa msingi, umuhimu wa kuwasilisha jinis gani wanaishi sasa. Nguvu ya kuvutia ya Ukristo inajumuisha kabisa nguvu ya ushuhuda, walihitimisha wanandoa, na ushuhuda wa Wakristo ambao ni upendo wa Kristo aliowafundisha.