Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Masilo John Selemela kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Masilo John Selemela kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Pretoria, Afrika ya Kusini. 

Askofu Msaidizi Masilo John Selemela Jimbo Kuu la Pretoria

Askofu Msaidizi mteule Masilo John Selemela alizaliwa tarehe 13 Januari 1972 . Tarehe 12 Juni 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Amewahi kuwa: Paroko-usu; Mkurugenzi msaidizi wa Miito na Vijana. Amewahi kuwa ni Mkurugenzi wa Miito Jimbo, Mratibu wa Elimu ya Maisha Kitaifa, Mwenyekiti Msaidizi wa Tume ya Fedha Jimbo pamoja na Baba wa maisha ya kiroho St. Brendan.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Masilo John Selemela wa Jimbo Katoliki la Tzaneen kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Pretoria, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Msaidizi mteule Masilo John Selemela alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya St. John Vianney. Itakumbukwa kwamba, Askofu Msaidizi mteule Masilo John Selemela alizaliwa tarehe 13 Januari 1972 huko Magoebaskloof, Jimbo la Tzaneen. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 12 Juni 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, kama Padre amewahi kuwa: Paroko-usu; Mkurugenzi msaidizi wa Miito na Vijana. Baadaye aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa Miito Jimbo Katoliki la Tzaneen, Mratibu wa Elimu ya Maisha Kitaifa, Mwenyekiti Msaidizi wa Tume ya Fedha Jimbo pamoja na Baba wa maisha ya kiroho katika Shule ya St. Brendan kati ya mwaka 2004 -2006.

Monsinyo Masilo John Selemala, Askofu msaidizi Jimbo kuu la Pretoria
Monsinyo Masilo John Selemala, Askofu msaidizi Jimbo kuu la Pretoria

Kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2011 alitumwa na Jimbo lake kwenda mjini Roma ili kujiendeleza zaidi na hatimaye, akajipatia Shahada ya uzamili na Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana. Askofu Msaidizi mteule Masilo John Selemela ajiendeleza pia na hatimaye, akajipatia Stashahada ya Kanuni za Uongozi wa Kanisa kutoka katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wakleri, kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2011. Aliporejea nchini Afrika ya Kusini, aliteuliwa kuwa mlezi na hatimaye, Gambera Msaidizi wa Seminari kuu ya St. John Vianney. Na kati ya mwaka 2019 akapandishwa cheo na kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya St. John Vianney hadi kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Julai 2022 kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Pretoria, Afrika ya Kusini.

Uteuzi Pretoria
16 July 2022, 14:38