Tafuta

Kardinali akiwa ziarani Sudan Kusini Kardinali akiwa ziarani Sudan Kusini 

Parolin anakutana na Salva Kiir:Pambanio pekee la kufanya ni kwa ajili ya amani!

Katibu wa Vatican,tarehe 5 Julai mchana alikuwa Ikulu ya Rais.Nusu saa ya mazungumzo katika kumbukumbu ya mafungo yaliyofanyika mji wa Vatican 2019 na Papa alisema:“Bila amani,hakuna maendeleo”.Mara baada ya mazungumzo hayo Kardinali huyo alikutana na makamu wa kwanza wa rais Riek Machar na kusisitiza nia yake ya kutekeleza mchakato wa amani nchini humo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mapambano pekee ya kufanya ni kwa akili ya  amani na maendeleo. Ni vita vinavyopaswa kupiginiwa wote kwa pamoja. Amani na maendeleo ni vitu viwili vinavyohusiana: bila amani hakuna maendeleo. Na kukosekana kwa amani ni chanzo cha kukosekana kwa utulivu na kutoridhika.  Ni  maneno ya kumbukumbu ya mafungo ya kiroho 2019 katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican kwa viongozi wa Sudan Kusini walioshiriki ambapo Papa, Francisko kwa ishara ya dhati kabisa ambayo haitasahaulika kwa wote alibusu miguu ya viongozi hao. Na ndiyo ilikuwa chanzo cha mazungumzo ya machana tarehe 5 Julai 2022 kwa  nusu saa kati ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican na rais wa Sudan Kusini. Salva Kiir Mayardit.

Kardinali Parolin na Rais wa Sudan Kusini.
Kardinali Parolin na Rais wa Sudan Kusini.

Mkutano huo ulifanyika alasiri  ndani ya Ikulu ya Rais na ndio ilikuwa hatua ya  kwanza rasmi ya safari ya Juba kwa katibu Vatican ambaye tarehe 6 Julai asubuhi  alielekea  katika kambi ya watu waliohamishwa ya Bentiu kaskazini mwa nchi. Kati ya ulinzi  mkali, mkutano na rais, ambaye alionekana kwenye chumba cha mkutano akiwa na kofia nyeusi na miwani, ulifanyika katika hali ya utulivu. Mara kadhaa Salva Kiir amerudia kumwambia Kardinali Parolin na ujumbe wake  “karibu Juba”, akitumaini  kuwa wanaweza kutumia siku zao nchini mwao kwa utulivu. Wazo la kwanza lilikuwa  kwa Papa, afya yake na safari ambayo haikuwezekana kwenda Afrika. Kama ilivyotokea hata  katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Katibu wa Vatican  alisisitizia shauku ya Papa  Francisko kwenda katika maeneo hayo mara tu hali, hasa afya ya  kimwili, itakaporuhusu. “Nina uhakika na ziara ya Papa,” alisema Rais Salva Kiir,  huku akihakikisha kwamba nchi iko tayari kuunga mkono tukio hilo muhimu na kwamba Wakristo wote wa madhehebu mbalimbali wamekusanyika pamoja  ili kumwombea Papa apone haraka.

Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini
Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini

Kwa maana hiyo Kardinali Parolin alimfikishia Rais wa Suda Kusini ujumbe wa Papa.  Ujumbe ambao unaweza kufupishwa kwa sehemu mbili ya “Upatanisho na amani”. Sio mawazo mawili, lakini malengo mawili madhubuti ya kufikiwa. Kumekuwa na maendeleo katika maana hii katika miaka hii tangu kufanyika mafungo katika mji wa Vatican; Kwa hakika, Kardinali Parolin alikiri kwamba, hata na Papa ametambua na kuthamini hatua zilizochukuliwa na serikali. Lakini, katika hotuba yake, alisisitiza hasa kile kinachosalia kufanywa ili kuhakikisha utulivu kwa nchi iliyozindua Mkataba wake wa Amani uliohuishwa, mkataba wa amani unaomalizika mwezi Februari 2023, ambao bado haujatekelezwa. Kardinali Parolin aidha alionesha njia za kusonga mbele, pia kwa kuzingatia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao hasa wa  kukuza umoja wa kitaifa, kuleta utulivu wa nchi, kuanzisha mageuzi ya Katiba, kuhimiza harakati za umoja, ambao ni muhimu kwa maendeleo ya Sudan Kusini.

Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini
Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini

Katika suala hilo, Kardinali aliusoma, akiufanya uwe wake, hasa ile mistari ya mwisho ya hotuba ya Papa kwa washiriki katika siku za sala, mazungumzo na majadiliano katika makao ya Vatican. Mbali na  Rais Salva Kiir, makamu wa rais walioteuliwa Riek Machar na Rebecca Nyandeng De Mabio walikuwepo wakati huo huko Mtakatifu Marta. “Na kwa nyinyi watatu, ambao mmetia saini Mkataba wa Amani, ninawaomba  kama ndugu: kaeni kwa amani. Ninawaomba  kwa moyo wangu. Endeleeni mbele. Kutakuwa na matatizo mengi, lakini msiogope, endeleeni mbele. Tatueni matatizo. Umeanzisha mchakato na ili uweze kuisha vizuri.

Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini
Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini

Salva Kiir pia alitaka kusisitiza katika hotuba yake kuhisiana na  siku mbili za Vatican: “Tulirudi kutoka Roma na hatujapigana tena. Nilisema hakuna kufanya vita vipya. Watu wanaweza kuwa hawajaona maendeleo yoyote, lakini wamesikia ukimya wa bunduki ”. Mpiganaji tangu akiwa kijana, rais wa Sudan Kusini ambaye amerudia mara kwa mara imani yake kwa Mungu alimwambia kardinali kwamba  “Haturuhusu mtu yeyote kuanzisha vita. Sitaki kupigana tena, sasa tunataka amani nchini”. Kwa hivyo, ahadi kwamba kila linalowezekana litafanywa kuzuia ukiukwaji na kulinda watu. Na kwa kujibu Kardinali alisema “Fanyeni kila kitu kwa msaada wa Mungu”. Wakati wa mkutano huo, ambapo mawaziri wawili pia walipewa  nafasi ya neno waliorodhesha, changamoto zinazoikabili Sudan Kusini kwa mtazamo wa ndani na kimataifa. Pia kulikuwa na kutajwa kwa maandalizi ya uchaguzi ujao. “Hatua muhimu sana ni kuimarisha amani na upatanisho” Kardinali Parolin alisisitiza, wakati akiwaaka na kuwahimizai  pendekezo kwamba: “Nguvu zote za kisiasa lazima ziwe katika huduma ya maendeleo na maendeleo ya nchi”.

Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini
Kardinali Parolin ziarani Sudan Kusini

Baada ya  mkutano na Rais Salva Kiir, mkutano na makamu wa kwanza wa rais, Riek Machar, ulifuatia. Akiwa ameketi katika ofisi yake, pia katika kesi hiyo kwa karibu dakika thelathini, Machar pia alikumbuka mkutano na Papa mwaka wa 2019. Kuwasili kwa Papa nchini Sudan Kusini, aliongeza, kungetoa msukumo kwa michakato mbalimbali inayoendelea. Hili lilikuwa tayari likitokea katika miezi iliyotangulia ziara ya upapa: “Tulikuwa tukijiandaa kuonesha matokeo halisi, Machar alisema. Matumaini, kwa upande wake ni kwamba kitu kinaweza kuweka mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya Amani, iliyofufuliwa, kabla ya tarehe ya mwisho. Lengo ambalo hakika si rahisi kufikia. Riek Machar kwa hakika alionesha matumaini kwamba Sudan Kusini haitakosa msaada Vatica

06 July 2022, 17:20