Kardinali Becciu Kardinali Becciu 

Askofu Mkuu Becciu atashiriki Mkutano wa makardinali ujao

Askofu Mkuu Angelo Becciu amebainisha jinsi ambavyo amepokea mwaliko kutoka kwa Papa ili kushiriki katika mkutano wa Makadinali tarehe 27 Agosti.

VATICAN NEWS.

Askofu Mkuu Angelo Becciu atashiriki katika Mkutano ujao wa Baraza la Makardinali ulioitishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya kuunda Makardinali wapya na katika majadiliano ya siku zinazofuata kuhusu mageuzi ya Curia Romana. Habari hiyo ilifunuliwa na Kardinali mwenyewe, ambaye mnamo Septemba 2020 alivua haki za ukardinali, kufuatia mfululizo wa hatua za kisheria. Wakati wa Misa katika mji wa Italia wa Golfo Aranci huko Sardegna, ambako amekuwa likizo, Askofu Mkuu Becciu alisema kuwa alipokea mwaliko wa kushiriki kutoka kwa Papa Francisko.

Vyanzo vya habari kutoka Vatican vimebainisha kwamba, haki za Kardinali hazirejei ushiriki katika maisha ya Kanisa; Wakristo wanaitwa kushiriki katika hilo, kulingana na hali yao. Kwa upande wa makadinali hiyo inaweza kujumuisha mwaliko, wakati mwingine wa kibinafsi  wa kuhudhuria mikutano fulani iliyotengwa kwa ajili yao.

Askofu Mkuu Becciu, mwenye umri wa miaka 74, ni mmoja wa washtakiwa katika mchakato wa kimahakama ulioanzishwa tarehe 27 Julai 2020, katika muktadha wa matukio yanayohusiana na uwekezaji wa kifedha wa Sekretarieti ya London. Mchakato huo utaanza tena tarehe 29-30 Septemba 2022, baada ya mapumziko ya kiangazi, na utaendelea na vikao vingine saba vilivyopangwa kufanyika mwezi Oktoba. Askofu Mkuu huyo anatuhumiwa kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi, na amekuwa akishikilia daima kuwa yeye ni’ mwathirika wa njama dhidi yake’. Wakati wa kesi hiyo, akiwa amechukua msimamo huo mara tatu, amejitetea kwa kusema ni “mashtaka yasiyo na msingi.”

Tarehe 24 Septemba 2020, Askofu Mkuu Becciu aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kama Mkuu wa Baraza la Kipapa la liwayanagaza watakatifu kwa kwa Papa Francisko. Askofu Mkuu huyo alishikilia wadhifa huo tangu 2018, baada ya kuhudumu kama Katibu Msaizidi wa Vatican. Katika mkutano na Papa, Askofu Mkuu Becciu, ingawa alibakisha cheo cha kuwa kardinali, alikataa haki zilizounganishwa na ukardinali.

KARDINALI BECCIU ATASHIRIKI KATIKA BARAZA LA MAKARDINALI AGOSTI 27
23 August 2022, 14:55