Kujenga wakati ujao wa wahamiaji na wakimbizi:kukua pamoja na Kanisa

Katika Video mpya na mchango wa Papa katika muktadha wa Kampeni ya mawasiliano iliyohamasishwa na Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu,katika mtazamo wa Siku ya 108 ya Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi ijayo.Kwa mujibu wa Papa anasisitiza kwamba:“Wahamiaji na Wakimbizi wanahuisha maisha ya jumuiya”.

Vatican News

Katika ujumbe wa Papa Francisko, katika video ya tano ya Kampeni ya Mawasiliano iliyohamasishwa na Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu, katika matazamio ya Siku ya 108 ya Kimataifa kwa ajili ya Wahamiaji na Wakimbizi inatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 25 Septemba 2022, ambayo inaongozwa na kauli mbiu:“Kujenga wakati ujao na wahamiaji na wakimbizi”, Papa amebainisha kuwa: “Utofauti wa kujieleza wa imani na ibada ni fursa ya kukua kikatoliki.”

Katika video hiyo Papa Francisko anabainisha jinsi gani wahamiaji na wakimbizi wanavyoendelea kuhuisha jumuiya za kikanisa ambazo zinawapokea, Mfano ni Parokia moja ya Mtakatifu Maria wa Ziwa na Mama Yetu wa Lourdes huko Chicago nchini Marekani wenye utajiri wa wahamiaji wa mataifa tofauti, ambao wanaadhimisha misa kwa tamaduni zao hata Sakramenti.

Katika filamu hiyo, wanaparokia wanatoa ushuhuda kwa jinsi gani uwepo wa tamaduni nyingi na tamadumi za kidini zinaruhusu kuhamasisha umoja na kutajirisha imani ya kila mmoja. Papa Franciko kwa maana hiyo katika video hiyo anawauliza wote: Je ni jinsi gani kwa upande wetu mnaweza kuwafanya wahamiaji na wakimbizi washiriki zaidi katika jumuiya zenu?

Katika kujibu swali hilo, inawezekana kabisa kutuma video fupi au picha kwa njia ya:media@migrants-refugees.va

Au kwenda moja kwa moja katika mitandao ya kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi (M&R), cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Hiyo ina maana hata ya kutoa ushuhuda wa maandishi, video au picha ambazo zinaonesha kazi ya pamoja kwa ajili ya kuishi au kufanya uzoefu wa  Mada ya Siku ya Kimataifa ijayo.  Zana zote za Kampeni ya mawasiliano, ikiwa ni pamoja na kit katika lugha mbali mbali kwa kuelekeza Maadhimisho ya Ekaristi, sala, shughuli za vijana na watu wazima inawezekana kazitumia kwa uhuru.

PAPA KWA KAMPENI YA SIKU YA WAHAMIAJI NA WAKIMBIZI
25 August 2022, 06:49