Vatican:Agosti 29-30 utafanyika Mkutano wa Makardinali
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya habari Vatican, iliyotolewa Jumamosi tarehe 27 Agosti inabainisha kuwa Makardinali watakutana mjini Vatican kuanzia tarehe 29 na 30 Agosti 2022 ili kujadili Katiba Mpya ya Kitume 'Praedicate Evangelium', kama alivyokuwa ametangaza Papa Francisko mnamo tarehe 29 Mei iliyopita.
Kwa mujibu wa maelezo ni kwamba mkutano utakuwa na vipindi viwili, ambapo utafanyika kuanzia saa 3.00 asubuhi na mchana kuanzia saa 10.00 kamili jioni baada ya chakula na mapumziko. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika makundi kufuata na lugha mbali mbali kuhusiana na Hati hiyo ikiwa pii ni pamoja na kukabiliana kwa pamoja katika Ukumbi mmoja.
Hadi sasa wamethibitisha ushiriki wa makardinali 197, ambapo miongoni mwake kuna hata Mapatriaki wa nchi za Mashariki, Wakuu, na Makardinali wa Vatican. Jumanne mchana tarehe 30 Agosti 2022, baada ya mkutano wao, saa 11.30 jioni inatarajiwa kufanyika Misa Takatifu itakayoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.