Tafuta

2022.08.23 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Kazakhstan 2022.08.23 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Kazakhstan 

Ziara ya kitume ya Papa Francisko Kazakhstan:Mjumbe wa amani na umoja

Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican imewakilisha kwa waandishi wa habari Nembo ya ziara ya kutume ya Papa Francisko nchini Kazakhstani.Kauli mbiu ya ziara hiyo itakayofanyika kuanzia 13 -15 Septemba ni ‘Mjumbe wa Amani na Umoja’.

VATICAN NEWS

Ofisi ya Vyombo vya habari imewakilisha kwa waandishi wa habari nembo ya ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Kaszakhstan inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022. Katika nembo hiyo inawakilisha njiwa akiwa na tawi la mzeituni. Mabawa yana picha ya mikono miwili iliyo ungana pamoja kwa kumaanisha ujumbe wa amani na umoja.

Moyo ulio katikati ya mabawa, unawakilisha upendo, ambalo ni tunda la uwelewano wa pamoja, wa ushirika na wa majadiliano. Tawi la mzeituni, unawawakilisha na picha ya kupambwa vizuri sana, kama utamaduni wa nchi hiyo ya Kazakhstan. Kwenye nafasi ili wazi inaonesha rangi ya blu ya anga, ambacho ni kiini cha makazi ya utamaduni wa watu wa Kazakhstan, na ndani mwake kumecgorwa msalaba wenye rangi  ya majano.

Rangi zilizotumika ya  blu anga na njano ndizo rangi pia za Bendera ya Kazakhstan; wakati huo huo Njano na nyeupe kwa kwaida ni rangi ya Bendera ya Vatican. Kijani cha jani la mzeituni ni ishara ya matumaini. Kauli mbiu ya ziara ya kitume ni: “Mjumbe wa Amani na Umoja ambao uemandikwa juu kwa  lugha ya kikazakhstan, na chini kwa lugha ya kirusi.

NEMBO ZIARA YA KITUME YA PAPA YA NCHINI KASZAKHSTAN
23 August 2022, 14:59