Mafunzo ya Maaskofu wapya huko Regina Apostolorum,Roma
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana mjini Vatican, tarehe 8 Septemba 2022 na Maaskofu wanaudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskfou na La Makanisa ya Mashariki. Kwa mijibu wa Taarifa kutoka vyombo vya habari imesema kwamba hawa ni maaskofu ambao kwa siku hizi katika Chuo cha Kipapa cha Regina Apostolorum Roma, wanaendelea na Mkutano wa Mafunzo ya maaskofu wapya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu. Kozi hiyo imeanza mnamo septemba 1, ambayo inaongozwa na Mada: “To Announce the Gospel in the Changing Epoch and After the Pandemic: The Service of Bishop”, yaani “Kutangza Injili katika kipindi kinachobadilika na baada ya Janga: Huduma ya Askofu”.
Baada ya Misa ya ufunguzi iliyoongzwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, walikabiliana na siku za kazi zilizokuwa zinajikita na mada: “ Maana na upendo wa Kanisa la Kisinodi, Elimu katika uongozi wa kisinodi, namna ya kukabili matatizo kwa namna ya pekee umakini wa nyanyaso, Kanisa baada ya janga la uviko, Uzoefu wa kuishi kwa utawala wa jimbo; kuishi katika ulimwengu wa vyombo vya habari zaidi ya dhana ya kiteknolojia, Matashi mawili yaliyoelekezwa na Papa katika mchakato wa safari ya Kanisa: Familia na Udugu wa Ulimwengu, na Utakatifu wa kiaskofu katika umoja wa Kanisa.
Katika hatua ya kwanza, kati ya waliotoa hotuba, walikuwa ni baadhi ya wakuu wa Mabaraza ya Kpapa. Tarehe 8 Septemba Kardinali Marc Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu aliongoza misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, na baadaye, washiriki wamepokelea na Baba Mtakatifu Francisko. Kwa kuwa haikuwezekana kuandaa kozi hiyo katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19, mwaka huu malezi yanafanyika katika vikao viwili: cha kwanza, kinaendelea, ambacho kinahudhuriwa na maaskofu wapatao 150, na cha pili, kwa mada hiyo hiyo, wataanza tarehe 12 hadi 19 Septemba, tena katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Regina Apostolorum ambapo wanatarajiwa kuwapo takriban 170. Vikao vyote viwili vinashuhudia ushiriki wa kundi la Maaskofu wanaotegemea Baraza la Kipapa kwa ajili ya makanisa ya Mashariki ambapo wengine watatendelea na baadhi ya Mikutano iliyoandaliwa na Baraza hilo.