Rais wa PMS kwa maaskofu:Matendo ya utume ni fursa nzuri ya kichungaji
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa yamekuwa na nafasi kubwa katika miaka hii 200 ya maisha katika kusaidia uundaji na maisha ya Makanisa mahalia. Kwa hiyo kazi yao bado ni muhimu sana, alisema hayo Askofu Mkuu Giampietro Dal Toso, Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari (PP.OO.MM), wakati akizungumza kwenye Semina ya Mafunzo kwa Maaskofu wapya walioteuliwa kwa miaka ya karibuni (kutoka Asia, Amerika, Afrika Oceania), iliandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Akiwasilisha Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa (Kazi ya Uenezaji wa Imani, Shughuli za Utoto Mtakatifu, Kazi ya Mtakatifu Petro Mtume na Umoja wa Kimissionari), Askofu mkuu alikumbusha kuwa kunako mwaka 2022, imeadhimisho miaka mia mbili ya Kazi ya kwanza liyoanzishwa chini ya uongozi wa Pauline Jaricot, ambaye alitangazwa kuwa mwenyeheri mnamo Mei 22 iliyopita.
PMS ni Chombo cha kuunga mkono
Askofu Mkuu Dal Toso kwa kuongezea alisema mnamo Mwaka 1922 Papa Pius XI alitaka kuyapatia shughuli za Matendo ya kimisionari cheo cha ‘Kipapa’, na baadaye Papa Pius XII alisema katika Umoja wa Wamisionari, ili kueleza kwamba anatambua karama yao, na kilikuwa kinaanza kuwa chombo chake cha kuunga mkono, kwa sala na sadaka, Utume wa ad gentes ya Kanisa. Tangu wakati huo, Majisterio yote ya utume ya Papa imekuwa ikisisitiza juu ya umuhimu wa Kazi hizi. Kwa sasa kwa sababu ya umuhimu wake kwa Kanisa la Ulimwengu, Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa yameundwa katika ngazi ya Kanisa la Ulimwengu, na uwepo wa mikondo kama pengine hakuna shirika lingine la Kanisa alisema, huku akifafanua kwamba ni vyombo vinavyojitegemea, mtandao uliopangwa katika ngazi ya kitaifa wenye miongozi 120 ya kitaifa, ambayo nayo inakuwa na uwepo katika ngazi ya Kijimbo kwa hiyo “pia maaskofu, kwa maana ya kwamba wamekabidhiwa pia uangalizi wa Maaskofu mahalia.
Matendo ya kitume ni fursa nzuri ya kichungaji
Zaidi ya Kanuni za kisheria, ni muhimu kuona katika Matendo hayo fursa nzuri ya kichungaji, kwa kuwa imani inaimarishwa kwa kuitoa, kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyoandika katika Redemptoris missio, ili kuamsha maana ya kimisionari kwa waamini ina maana ya kufufua hisia ya imani ndani yao. Askofu Mkuu Dal Toso alisema : “Nilivutiwa sana na ukweli kwamba katika nchi mbalimbali Shughuli za Utoto Mtakatifu zimekuwa chombo cha malezi ya kawaida ya kichungaji kwa watoto. Kwa maana hiyo, katika siku za hivi karibuni Matendo hayo pia yanagundua jukumu lao katika huduma ya Kanisa mahalia, na kwa malezi ya kimisionari ”. Askofu Mkuu Dal Toso hata hivyo alibainisha kwamba dhana tatu zinazofupisha karama ya Matendo ni: imani, utume na ulimwengu mzima. Bila imani hakuna utume na mtu anaweza kusadikishwa juu ya maana ya utume ikiwa tu anamwamini Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, aliyemfanya mtu kwa aliji ya wokovu wetu.
Utume unamaanisha kushiriki karama ya imani na kuumwilisha
Utume unamaanisha kushiriki karama ya imani, na hivyo kuimwilisha. Ukamilifu wa Matendo unamaanisha kwamba hakuna mtu anayeamini peke yake, lakini sisi sote tunaunganishwa na imani moja na sakramenti sawa, na kwa hiyo tunatunza kila mmoja. Rais huyo aliwataka Maaskofu kudumisha uhusiano thabiti na Mkurugenzi wa Kitaifa, anayeratibu Kazi katika ngazi ya kitaifa, hasa katika mtazamo wa uhuishaji wa kimisionari, naa badaye akawaomba kwa hakika wasikose kuombea utume na kukusanya sadaka na kuituma katika kitengo cha kitaifa yale makusanyo yanayotolewa wakati wa Siku ya Utume Duniani. Moja ya mambo mazuri sana ya Kazi zetu ni kwamba hata Makanisa maskini zaidi yanachangia”, alihitimisha, huku akikumbuka kwamba PMS, hasa Kazi ya Kueneza Imani inasaidia Makanisa yote ya maeneo ya utume kwa namna usawa. Mnamo 2021, POPF ilisaidia maisha ya Makanisa machanga na mipango yenye thamani ya dola milioni 110. Kwa njia hiyo aliongeza kwamba Matendo hayo yanaruhusu Kanisa mahalia kufunguka kwa Kanisa la kiulimwengu. Hakuna Kanisa lmahalia pasipo na Kanisa la Ulimwengu wote na kinyume chake.