Waandishi watakabiliana na suala la utakatifu leo hii katika mafunzo kuanzia 3-6 Oktoba
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuingia katika mazungumzo na ulimwengu wa kisasa ili kuelewa vyema utakatifu ni nini, ndilo lengo la mkutano wenye mada “Utakatifu leo", ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na ambao huko wazi kwa wote, utafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 6 Oktoba 2022 jijini Roma katika Taasisi ya Baba wa Kanisa Augustinianum. Tarehe 19 Septemba mkutano huo umewasilishwa katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, na kwamba ni tayari takriban watu 200 wamejiandikisha.
Utakatifu wa mlango wa karibu ni nini?
Lengo lake ni kutaka kutafakari kwa kina kwa kile ambacho Papa Francisko anakiita utakatifu wa mlango wa karibu, na ndivyo amebainisha Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu wakati wa hotuba yake ya uwakilishi wa mkutano huo na kwamba “ni njia ambayo watu wote wameitiwa na ambayo Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican umeitaja kwamba ni “wito wa utakatifu kwa wote” na inapaswa kuchunguzwa kwa kina. Kiutendaji, katika hali halisi ya sasa, mkutano huo unaohusisha washiriki wa Mabaraza ya kipapa, maprofesa, wasomi, na watetezi wa utamaduni na vyombo vya habari, ambao unataka kutafakari jinsi ya kuwatambua waamini ambao wana sifa ya utakatifu katikati ya watu wa Mungu na juu ya vipengele vinavyopelekea kutangazwa kuwa mtakatifu.
Ushiriki wa masuala ya kiitaalimungu, kisosholojia na mawasiliano
Kardinali Semerero akiendelea na hotuba yake alisema kwamba wanataka leo hii kusisitiza na kuwashirikisha wataalamu wa taalimungu, kiroho, kisosholojia na mawasiliano kwa ajili ya mazungumzo mapana zaidi juu ya masuala yanayoikabili Baraza hili kila siku. Kwa njia hiyo, mikutano inapaswa kufanywa kila mwaka, ili kufanya ujumbe wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu lionekane zaidi, linalolenga kuangazia kazi ya kila siku na uchunguzi juu ya somo la utakatifu, na kuiweka kwa kulinganisha na matakwa ya kiutamaduni, kitaalimungu na kikanisa ya kwa wakati.
Umaarufu wa utakatifu na ushujaa wa Kikristo
Mkutano huu umeongozwa na kile ambacho Francis koaliandika katika Wosia wa Kitume Gaudete et exsultate (furahia na shangilia kuhusiana na wito wa utakatifu na ambao Papa alipendekeza kujaribu kuumwilisha katika mazingira ya sasa, pamoja na hatari, changamoto na fursa zake. Hasa, itahamasisha mada mbili: sifa ya utakatifu na ushujaa wa Kikristo, ambayo ni imani ambayo waamini leo wanayo juu ya utakatifu wa mtu, kwa hivyo mtazamo wa upekee unaoongoza katika maombezi, na tena mazoezi ya fadhila, mauaji ya kishahidi na sadaka ya maisha, ambayo ni kwenda mbele licha ya matatizo. Hii ni kwa sababu kazi ya Baraza la mchakato wa kuwatanagaza Watakatifu ni kutambua utakatifu kwa njia ya awamu maalum na iliyoratibiwa ya utambuzi, Kardinali alifafanua na kuongeza kwamba utakatifu uliotangazwa kuwa mtakatifu, ambao unapendekeza waombezi na mifano ya kuhamasisha Kanisa, lengo la kutambua watu wa mfano, wanaokwenda zaidi ya maisha ya kawaida, kuwaita waliobatizwa kuishi maisha yao ya kila siku kwa njia takatifu".
Ukristo sio jambo rahisi
Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari, kwa mwandishi aliyerejeea wale wanaoitwa watakatifu walio hai na Kadinali Joseph Zen Ze-kiun, askofu mstaafu wa Hong Kong (China), mwenye umri wa miaka 90, chini ya kifungo cha nyumbani tangu Mei kwa tuhuma za kuunga mkono ' upinzani dhidi ya serikali ya Beijing, na ambayo kesi yake bado iko katika mchakato, Kadinali Semeraro alisema kwamba "Kadinali Zen anatuonesha kwamba kuwa Mkristo si jambo rahisi." Mwenyekiti wa Baraza hilo alitumani kwamba Kardinali atatoka nje ya historia na pia akasema wanapzungumza kuhusu sifa ya utakatifu wanarejea “ukweli wa ujumbe unaopitishwa kwetu katika hali fulani za kielelezo halisi”.
Siku za mkutano
Programu ya mkutano inajumuisha hotuba 11, mawasiliano 5 na meza za mduaria 2 za pande zote, ambazo zitafanywa mhutasari wa mada zilizopendekezwa kwa mtazamo wa kimataifa na kwa njia maarufu, pia shukrani kwa uratibu wa mwandishi wa habari. Hadhira pamoja na Papa Francisko imepangwa kufanyika tarehe 6 Oktoba 2022. Kardinali Semeraro alifungua na kuhitimisha kazi hiyo.